Serikali yamwaga mashangingi: Hatujifunzi tu kutoka Rwanda jinsi Kagame anavyotawala? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yamwaga mashangingi: Hatujifunzi tu kutoka Rwanda jinsi Kagame anavyotawala?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Iga, Dec 23, 2008.

 1. I

  Iga Senior Member

  #1
  Dec 23, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WAKATI Bw. Kagame huko Rwanda kafunga soko la serikali kuhodhi magari yanayokula mabilioni ya fedha za umma bila kuwa na manufaa ya moja kwa moja kwa raia wa kawaida ila tu kwa wale wanaoyatumia na jamaa zao, hapa Tanzania magari ya kifahari zaidi ya 700 ndio kwanza yanapakuliwa bandarini.

  Je, huu si unafiki kulalama mzigo anaobebeshwa mwananchi wa kawaida anayeteseka kwenye usafiri wa umma usio na heshima wala taadhima usiku na mchana, akienda na kutoka kazini au hospitali au shule au kwenye shughuli zake nyingine na kisha kuwa wasanii kwa kuthubutu bila aibu kuwaambia watu kuwa huu ni mzigo wa mwisho wavumilie tu.

  Magari hayo mia saba kwa bei za haraka haraka ni kwambwa yameigharimu serikali shilingi bilioni 70. (Tshs. 70,000.000,000/=). Magari haya yakiuzwa kwa watu na mashirika binafsi kwa hiyo yanaweza kuipatia serikali fedha za kuwalipa wastaafu wa EAC na kuondokana na maapizo na laana zao kwa Watanzania wote na vile kumaliza kabisa matatizo madogo madogo ya walimu.

  Nilulize swali moja, je, serikali ya awamu ya nne inaona ugumu gani kuwauzia au kuwakopesha magari hayo watumishi wa serikali ili angalau tupunguziwe mzigo wa pettroli na spea pati? Au hii ndio tabia na hulka yake halisi ya kusema maneno tofauti na kile inachokiamini kama vile kutudanganya sisi ni wajamaa na kumbe nchi ni ya kibepari?

  Ingawa gharama ya kununua magari hayo ni kama bilioni 70 lakini gharama za kuyajaza mafuta na kuyahudumia kiufundi ni bilioni 200 kwa mwaka. Hivi tunataka kuwakomboa Watanzania au tunawafanyia usanii kwa namna hii?

  Hivi kweli tutashangaa Rwanda inaelekea kwenye GDP per capita ya dola 3,000 sisi tunaogelea ogelea kwenye dola 600 kwa miongo kadhaa sasa?


  Na wakubwa hawajui jinsi tunavyoila Krismasi ya mwaka huu, mwaka mpya wa Kiislamu na mwaka mpya wa Kikirsto kwa taabu na dhiki kubwa ajabu?
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Labda Serikali inataka kuiokoa Toyota katika mtikisiko huu wa hali ya kifedha duniani. Manake haiingii akilini ununue mashangingi 700 wakati unafunga shule hakuna chakula, hospitali watu wanalala chini nk.
   
 3. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na hapo ndo ujuha unaanzia! Mambo ya msingi yanawekwa pembeni wanarukaruka na maslahi yao binafsi. nadhani hawana team work hata kidogo. Kila mmoja hukurupuka na lake asubuhi. Pinda anasema magari tupunguze bandarini yanaletwa 700. Ni katika ufujaji kama huu wanatuambia tuwe wazalendo na kuipenda nchi yetu!
   
 4. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hongera sana ndugu yangu kwa taarifa hii,umeiandika kwa hisia, nadhani inatoka rohoni.Tuko pamoja.
   
 5. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  VX 700? - Kweli Tz ni TAJIRI bali WaTz ni maskini! Shame on our "Viongozi"!
   
 6. P

  PanguPakavu Amy Senior Member

  #6
  Dec 23, 2008
  Joined: Jul 7, 2007
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  halafu jitu linasimama kwenye jukwaa na kusema linaipenda tanzania na linampango wa kuiendeleza.jiiiiiiiiiiiiiiz...,
  these guys are there for the money...,nothing else..,
  till something changes abruptly we are gon be poor forever...,atleast us "walalahoi"
  2 them big shots in the government...,recession my **s!
   
 7. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Watanzania tuache kulalama bila sababu za msingi.tunadai kuwa watumishi serikalini hawaendi vijijini kuhimiza maendeleo.tunataka viongozi waende vijijini kusimamia maendeleo sasa unataka waende kwa kutumia punda.haya magari munayoita ya gharama gari gani ambalo sio gharama siku hizi landrover seris three hazipo siku hizi mbona watu wanakuwa hawaelewi chochote na kujifanya kujua hebu nieleze gari lililorahisi ni lipi ukilinganisha na ukubwa wa nchi hii ubovu wa barabara za vujijini nk.
   
 8. E

  Endaku's JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2008
  Joined: May 25, 2007
  Messages: 322
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  These leaders once they got any professional carrier its for marketing themselves for various political posts ,thats why they fully politicians they even forget what is to be done to achieve economic development for TANZANIA they are just talking blabla !!!! Dr ,Prof going to do politics its
  not bad but are they fully utilising themselves for their country benefits or
  just happy to receive handsome payments only and readings nice reports and
  plugging the figure that per capital income is growing what a nonsense go to the real life and see how difficults things are !! Sometimes i just wish to do ............................... for sure !
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Mkuu Iga asante kwa taarifa muhimu sana.

  Wakuu ni dhahiri kabisa serekali yetu imeshindwa kutoa kipaumbele kwa mambo muhimu yanayoweza kulisaidia taifa letu kupiga hatua zaidi,kwakuwa wananchi walio wengi mambo kama haya hawajui kwamba yanauhusiano wa moja kwa moja na umasikini unaowazunguka.
  Tsh 70 bilioni zingetumika kununua matrekta zaidi ya 1800 ambayo kila mkoa ungeweza kupata mgao wa matrekta 82.Hivi tunahitaji wataalamu kutoka nje kutuambia tuache kununua magari ya kifahari !!!!.

  Mwl J Nyerere aliwahi kusema ili nchi iendelee inahitaji watu,viongozi bora,siasa safi na ardhi.
  Tanzania ina watu miloni 40,ina ardhi yenye ukubwa wa 364,900 sq miles.
  Tanzania ina mito mikubwa na maziwa makubwa ambayo kama tungeamua kuwekeza katika kilimo tu leo hii tungekuwa na uwezo kuilisha Afrika.Kenya inategemea kupata chakula kama mahindi,maharage na nk kutoka Tanzania.Pengine Kenya wamegundua watanzania hawaitumii ardhi yao vizuri ndiyo maana wanataka ardhi iwe huru kwa wananchi wa EAC.
  Hakuna ubishi tene kwamba Tanzania imekosa siasa safi na uongozi bora.
  Viongozi tulionao hawana vision na mission ya kuliondoa taifa katika umaskini.
  Viongozi wetu waliofanikiwa kukwea hadi ngazi za juu wana sifa zifuatazo majungu,fitna,ufisadi,uongo na ubinafsi.
  Policies nyingi zimebaki kwenye vitabu bila utekelezaji,MKUKUTA,MKURABITA na nk ni mfano mzuri wa namna wanasiasa walivyo waongo hasa kipindi cha kampeni.
   
 10. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2008
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni zile 10% za D.T Dobie na International Motors... wenyewe wanaziita "commision" kwa kuwaletea biashara. The higher the deal, the higher the commision.
   
 11. Companero

  Companero Platinum Member

  #11
  Dec 23, 2008
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mheshimiwa Waziri Mkubwa ameshatoa msimamo wa Sirikali kuhusu kupunguza matumizi ya mashangingi. Msiwe na haraka kuliko upesi. Vuteni subira. Utekelezaji wa maagizo ya Serikali unakwenda hatua kwa hatua. Mathalani:

  - Kupunguza semina kulianza kwa hatua ya kuwa na semina kuhusu kupunguza semina
  - Kupunguza matumizi ya magari kumeanza na hatua ya kumalizia kwanza manunuzi
  - Kutekeleza maazimio ya Kamati ya Richmond bado kuko kwenye hatua ya hatua
   
 12. Modereta

  Modereta Senior Member

  #12
  Dec 23, 2008
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu wewe WATANZANIA sio Mbumbumbu, hayo magari yanayokwenda vijijini tunayaona na hapa mjini yakipeleka watoto shule na kuchukua majani ya ngombe tunayaona si kwamba watu hawajui. Ukumbuke wngine hao wanayoyatumia ni ndgu zao na wanajua matumizi ya hayo magari. Hebu tuache kutetea vitu ambavyo viko wazi. Nasikia kule kwa Kagame hakuna vijiji!!!!!!!!!!!
  Mwenzetu angalia hata alama za nyakati, kwako wewe ni sawa tu wagonjwa mwananyamala, amana, temeke na hospitali zote za serikali wanakosa dawa ni sawa?????????
   
 13. m

  mti_mkavu Senior Member

  #13
  Dec 23, 2008
  Joined: Dec 23, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Nimepita Muhimbili Hospitali leo ni balaa tupu! Kuna tatizo la umeme vipimo havifanyiki. Jamani hizi hela mngewanunulia majenereta.

  Ni aibu tupu!!!!
   
 14. Companero

  Companero Platinum Member

  #14
  Dec 23, 2008
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kuna kitu kinaitwa mistari ya bajeti, hii huwa haivukwi hivi hivi tu.
   
 15. m

  mti_mkavu Senior Member

  #15
  Dec 23, 2008
  Joined: Dec 23, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kweli halipitwi lakini ni wangapi wanaletewa bajeti kama walivyoomba. Angalia tangazo la haki elimu.

  hela hazifiki kaka
  sijui lakini!!!
   
 16. Companero

  Companero Platinum Member

  #16
  Dec 23, 2008
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hela hazifiki zikifika zinaliwa zisipoliwa hazitoshi zikitosha hazitumiwi zikitumiwa hazibaki zikibaki zinarudishwa zikirudishwa hazisaidii zikisaidia...
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  Serikali yetu haina vipaumbele kabisa. Wakati mahospitali yetu hayana vitanda, madawa na vifaa muhimu, wakati mashule yetu hayana vyumba vya madarasa vyenye hadhi ya kuitwa madarasa, vyoo, walimu, na vifaa muhimu vya mashuleni, wakati wasomi wanaomaliza katika vyuo vikuu mbali mbali hawana ajira, wakati umeme wetu bado ni wa kubahatisha, wakati maji safi bado ni adimu mno cha muhimu walichokiona wao ni kwenda kununua magari ya kifahari ambayo hayaongezi tija yoyote na kuleta maendeleo kwa Watanzania. Halafu bila haya hata aibu 2010 watarudi kwa wananchi kuomba tena kupewa awamu nyingi ya kuebdelea kuiangamiza Tanzania. Shame on you JK na serikali yako!!!
   
 18. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #18
  Dec 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Najua Zitto anaujua undani wake na Malecela ndiye kapelekwa Mbeya kuchukua jimbo .Wacha tusikie wananchi wa Mbeya ni waelewa wa namna gani na Jimbo watampa kuna issues nzito na hizi Mbeya ni sehemu yake .Mchungaji kumbe ana lake jambo .Mie nilitaka kushangaa aina ya Lwakatare kuingia CCM na huku hawaachi Makanisa maana yake nini .Wacha tusikilizie wakati Brussels hawana heating system magari yanamwagwa ? Jamani duh!!
   
 19. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Watu wanagombea nafasi mbalimbali, na kutaka vyeo mbalimbali serikalini na kwenye idara nyingine kutokana na kutaka kuyatumia magari hayo. Ndio maana itakuwa vigumu sana kwa serikali(yaani wanaoataka madaraka ili watumie magari hayo) kupiga marufuku kabisa matumizi ya magari hayo. Naona badoi ni politics tu. Hatuwezi kujilingansha sisi na Rwanda, Rwanda tayari wako steps ahead of Tanzania. Wana uwezo mkubwa wa ku-manage nchi yao na ku-manage raslimali zao, sisi ni kinyume kabisa na Rwanda, labda tulinganishwe kidogo na Somalia, ingawa sisi hatuna vita na hatuuani kama wenzetu Somalia.
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  Madarasa yakosesha maelfu sekondari
  Merali Chawe, Mbeya
  Daily News; Tuesday,December 23, 2008 @21:15

  Zaidi ya wanafunzi 20,000 kati ya 41,017 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mkoani Mbeya, wamekosa nafasi ya kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa na mabweni.

  Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Kaponda aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanafunzi 77,072 waliandikishwa na kati ya hao waliofanya ni 74,518 wakiwamo wasichana 37,926 na wavulana 36,592 sawa na asilimia 97.

  Hata hivyo, kiwango cha ufaulu kimeshuka kutoka asilimia 63 mwaka jana hadi asilimia 55 mwaka huu huku kukiwa na mahitaji ya vyumba 620 vya madarasa ili waliobaki waingie katika awamu ya pili.

  Alisema kati ya wanafunzi 41,017 waliofaulu wakiwamo wasichana 18,206 na wavulana 22,811, waliochaguliwa katika awamu ya kwanza kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza ni 16,236 na wametengewa nafasi 234 za bweni huku wanafunzi 16,002 wakisoma shule za kutwa.

  Naye John Mhala anaripoti kutoka Arusha kuwa wanafunzi 4,525 waliofaulu mtihani mwaka huu, watakosa nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa shule za sekondari.

  Ofisa Elimu wa Mkoa wa Arusha, Raymond Mapunda alisema hilo linatokana na pamoja na sababu nyingine, ongezeko la ufaulu mwaka huu ambako watahiniwa 22,738 walifaulu kuingia kidato cha kwanza kati ya 40,884 waliofanya mtihani. Kiwango hicho ni sawa na asilimia 66.5 ya ufaulu na kwamba wastani wa kufaulu umeongezeka kutoka asilimia 85.15 mwaka jana hadi asilimia 115.3 mwaka huu.

  Huko Songea, Juma Nyumayo, anaripoti kuwa wanafunzi 19,085 wamefaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu mkoani Ruvuma wakiwamo wasichana 8,688 na wavulana 10,397 sawa na asilimia 50.2 ya wanafunzi 38,013 waliofanya mtihani mkoani hapa. Mwenyekiti wa Kamati ya Uteuzi Mkoa wa Ruvuma, Saleh Pamba alitangaza matokeo hayo jana na kusema kuwa matokeo hayo hayaridhishi ingawa kuna ongezeko la asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 43.5 ya mwaka jana.
   
Loading...