Serikali yamuumbua RC Mbeya

LazaroSMtindi

Senior Member
May 6, 2008
100
5
Uamuzi wa Serikali kupeleka chakula cha msaada wilayani Kyela kwa ajili ya waathirika wa mafuriko makubwa yaliyotokea wilayani humo, unamuumbua RC wa Mbeya ambaye kwa mwezi mzima sasa amekuwa akidai kuwa hakuna maafa Kyela na mafuriko yaliyotokea ni ya kawaida tu!

Ingekuwa nchi zingine, kiongozi wa aina hii angefukuzwa kazi kwa kuzuia misaada na kuihujumu Serikali kwa wapiga kura.

Tatizo la Mwakipesile ni kuwa katika miaka 10 ya ubunge wake yametokea mafuriko mengi Kyela na hakuwahi kugawa hata kilo moja ya mchicha kwa walioathirika. Hivyo ameamua kumvurugia Mbunge wa Kyela, Dk. H. Mwakyembe ambaye alipambana naye kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Kyela mwaka 2005, Mwakipesile akashindwa vibaya na sasa anatumia nafasi yake ya ukuu wa mkoa kumrudi mbaya wake.

Lazaros
 
Siasa na uongozi wa chuki hauna nafasi tena. Naamini kabisa Bwana Mwakipesile ni binadamu, hivyo hastahili kuacha watu wafe kwa njaa kwaajili tu ya mahangaiko yake ya kisiasa.
 
Uamuzi wa Serikali kupeleka chakula cha msaada wilayani Kyela kwa ajili ya waathirika wa mafuriko makubwa yaliyotokea wilayani humo, unamuumbua RC wa Mbeya ambaye kwa mwezi mzima sasa amekuwa akidai kuwa hakuna maafa Kyela na mafuriko yaliyotokea ni ya kawaida tu!

Ingekuwa nchi zingine, kiongozi wa aina hii angefukuzwa kazi kwa kuzuia misaada na kuihujumu Serikali kwa wapiga kura.

Tatizo la Mwakipesile ni kuwa katika miaka 10 ya ubunge wake yametokea mafuriko mengi Kyela na hakuwahi kugawa hata kilo moja ya mchicha kwa walioathirika. Hivyo ameamua kumvurugia Mbunge wa Kyela, Dk. H. Mwakyembe ambaye alipambana naye kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Kyela mwaka 2005, Mwakipesile akashindwa vibaya na sasa anatumia nafasi yake ya ukuu wa mkoa kumrudi mbaya wake.

Lazaros

Lazaro,

Karibu JF...
 
Mwakipesile Anathubutu Kuacha Ndugu Zake Wataabike Na Njaa Sababu Ya Utashi Wa Kumuharibia Mwakyembe?jk Huoni Na Huamini Ubaya Uliosemwa Kuhusu Kumuweka Ukuu Mkoa Pale ...huyu Ameshindwa Ubunge Mkoa Huo Huo Unamrudisha Ukuu Pakle Unataka Nini Au Ndio Mtandao??????uvunje Basi Tuone Maana Umesema Hakuna Makundi Wala Mtandao
 
Unajua kaka tatizo la wana siasa wetu wanafanya kazi kwa nidhamu ya woga ili waonekane wanafanya kazi wakati wanaumiza wanachi.Hii inanikumbusha tukio moja mwaka 1999 kule wilaya ya ulanga mkoani morogoro Mkuu mmoja wa wilaya wakati huo kuwa wilaya yake haina upungufu wa chakula ila watu wanakufa kwa kurogana na kipindupindu kumbe mzee njaa imewacharaza watu mpaka basi...Kisa Sumaye alitangaza DC atakayetangaza wilaya yake ina njaa ajue amejifukuzisha kazi mwenyewe....Very stupid sijui yuko wapi yule mzee i guess atakuwa amekufa nae pia..
 
Huyu Mwakipesile hapo amechemsha kabisa kama anamwalibia ili yeye agombee mwananchi gani ambaye atampa kura wakati anaona kabisa anatendewa vibaya.
Tunajua JK amembeba tu huyu Mwakipesile kwa kuulinda mtandao wake wa kumpaliza Mwandosya CCM makundi bado yapo na asipo angalia MWandosya atamzidi kete JK akiamua kuchukua fomu kugombea NEC.
 
Uamuzi wa Serikali kupeleka chakula cha msaada wilayani Kyela kwa ajili ya waathirika wa mafuriko makubwa yaliyotokea wilayani humo, unamuumbua RC wa Mbeya ambaye kwa mwezi mzima sasa amekuwa akidai kuwa hakuna maafa Kyela na mafuriko yaliyotokea ni ya kawaida tu!

Ingekuwa nchi zingine, kiongozi wa aina hii angefukuzwa kazi kwa kuzuia misaada na kuihujumu Serikali kwa wapiga kura.

Tatizo la Mwakipesile ni kuwa katika miaka 10 ya ubunge wake yametokea mafuriko mengi Kyela na hakuwahi kugawa hata kilo moja ya mchicha kwa walioathirika. Hivyo ameamua kumvurugia Mbunge wa Kyela, Dk. H. Mwakyembe ambaye alipambana naye kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Kyela mwaka 2005, Mwakipesile akashindwa vibaya na sasa anatumia nafasi yake ya ukuu wa mkoa kumrudi mbaya wake.

Lazaros

Siasa za chuki hadi lini na kuwaacha wanachi wanateseka na njaa?
Hivi ghalani hakuna hata spea za Ma RC?
 
Niliwahi kusema hii njaa inayokuja hata kama serikali itakuwa na chakula cha hifadhi bado watanzania watakufa kwa njaa kwani viongozi wetu wanatawaliwa na siasa za uongo, hawasemi ukweli kwenye mambo ambayo ni ya msingi kwa nchi yetu.

Wakati Sumaye ni waziri mkubwa aliwahi kuwatisha kuwa kiongozi ambaye mkoa wake au wilaya yake itakumbwa na njaa atawajibika tukaona watu wanakufa magazeti yakiandika viongozi wanasema uongo mpaka hali ilipokuwa mbaya zaidi ndio wanakubali.

Nafikiri labda bado wanaogopa kuwajibishwa kwa kuwa na njaa kwenye eneo lake la kazi.
 
Uamuzi wa Serikali kupeleka chakula cha msaada wilayani Kyela kwa ajili ya waathirika wa mafuriko makubwa yaliyotokea wilayani humo, unamuumbua RC wa Mbeya ambaye kwa mwezi mzima sasa amekuwa akidai kuwa hakuna maafa Kyela na mafuriko yaliyotokea ni ya kawaida tu!

Ingekuwa nchi zingine, kiongozi wa aina hii angefukuzwa kazi kwa kuzuia misaada na kuihujumu Serikali kwa wapiga kura.

Tatizo la Mwakipesile ni kuwa katika miaka 10 ya ubunge wake yametokea mafuriko mengi Kyela na hakuwahi kugawa hata kilo moja ya mchicha kwa walioathirika. Hivyo ameamua kumvurugia Mbunge wa Kyela, Dk. H. Mwakyembe ambaye alipambana naye kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Kyela mwaka 2005, Mwakipesile akashindwa vibaya na sasa anatumia nafasi yake ya ukuu wa mkoa kumrudi mbaya wake.

Lazaros

Mkuu,

Hii si kweli kwani mkuu wa mkoa Mwakipesile ameshiriki ipasavyo kutoa misaada ya maafa kule Kyela.

Labda tofauti tu Mwakipesile hajaenda kwenye TZ au radio kutamba katoa nini au kasimamia nini.

Kama unataka naweza kukupatia simu ya mkuu wa wilaya ya Kyela ambaye ndiye anasimamia misaada yote na ukapata ukweli.
 
tumekushtukia na wewe.....hakuna lolote tupatie namba za sim za wananchi walioathirika ili tuwapigie kwa mahojiano na utafiti wa kina...siasa ya kyela hakuna asie ijua bwana...tafadhari mkuu watu wanakufa kule tuache ubinafsi na chuki
 
Ukinishutukia mimi wala hainipi shida wala kuninyima usingizi. Nimekuambia ninachojua na wala hata sihitaji mtu wa kuniamini.

Kama unaelewa Kyela kuna njaa basi peleka misaada na wengine ndivyo tulivyofanya. Na sio kuleta maneno ya bure na siasa hapa.

Misaada yote inasimamiwa na mkuu wa wilaya, sasa unataka simu za walioathirika zitakusaidia nini? Uongozi wote pamoja na watu wa Kyela wanajua Kyela kuna maafa na wanahitaji kila aina ya misaada.

Hili la kwamba mkuu wa mkoa anakwamisha ni uongo mkubwa. Mimi sina mapenzi
yoyote na Mwakipesile lakini pia siko tayari kumchafua mtu kwasababu tu simpendi. Mnaotaka hizo siasa endeleeni nazo.

Ukitaka simu za viongozi wa wilaya nitakupatia wakiwemo Mbunge, mkuu wa wilaya na hata DAS. Vinginevyo mimi simo.
 
Acha jazba jaribu kua mtaratibu, by the way mie pia nimetoa mtazamo wangu so hakuna haja ya kubishana lakini.....ukweli unaumwa+messege sent
 
Tatizo la Mwakipesile ni kuwa katika miaka 10 ya ubunge wake yametokea mafuriko mengi Kyela na hakuwahi kugawa hata kilo moja ya mchicha kwa walioathirika. Hivyo ameamua kumvurugia Mbunge wa Kyela, Dk. H. Mwakyembe ambaye alipambana naye kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Kyela mwaka 2005, Mwakipesile akashindwa vibaya na sasa anatumia nafasi yake ya ukuu wa mkoa kumrudi mbaya wake.

Lazaros

Lazaros,

Aliyekuambia hizo habari hajakuambia ukweli. Hakujawahi kuwa na mafuriko makubwa Kyela tokea mwaka 1978.

Hivyo katika kipindi cha Mwakipesile kuwa mbunge hakuwahi kupambana na balaa la mafuriko kama ilivyotokea mwaka huu.

Kabla ya 1978 kulikuwa na mafuriko karibu kila mwaka, baadaye ikasimama ukiachia yale ya kawaida ambayo kwa ujumla hayawi na madhara zaidi ya kuwasumbua wanachi kwa siku.

Mambo mengine mnayoandika ni kuendelea kuchochea vurugu Kyela bila sababu za maana.
 
Acha jazba jaribu kua mtaratibu, by the way mie pia nimetoa mtazamo wangu so hakuna haja ya kubishana lakini.....ukweli unaumwa+messege sent
Ama kweli nyani haoni kundule.... Hivi wewe staili yako ya kuchangia mada hapa JF unaijua? Posti zako zote zimekaa kijazba na kichuki, ukifahamishwa unakimbilia kulia lia..
 
Hivi ni mkoa gani mwingine ambapo Mkuu wake wa Mkoa ni mwenyeji wa mkoa ule ule?

Mwanakijiji,

Mimi ni katika niliolaani hii ya kumwacha Mwakipesile kule Mbeya baada ya kushindwa ubunge.

Lakini ilipofikia lazima viongozi wetu wakubali kufanya kazi na watu wasiowapenda na hiyo inaweza kuwa motivating factor.

Hii ya kuzunguka kwenye magazeti na kutumia wapambe kuendeleza vita, haiwasidii wao na wala haiusaidii mkoa.

Kadri muda unavyoenda binafsi naona jitihada za wazi zinazofanywa ili kuonyesha Kyela na Mbeya kuna matatizo makubwa ya viongozi kugombana, na hata kukomoana.

Mbunge ana majukumu yake na mkuu wa mkoa ana ya kwake. Yeyote kati yao akishindwa ni kwasababu hana uwezo wa ku deliver na sio kwa visingizio vya kukwamishwa na mtu.

Watu badala ya kuchapa kazi wanahangaika tu na kujaribu kukuza mgogoro ili
wakiulizwa mbona Kyela ina matatizo kila mtu apate sababu ya kusingizia.

Mimi natoka Kyela na niko tired na hizi tuhuma za kila siku ambazo nyingi hazina maana kabisa.

Kwenye hili la maafa kuna watu wengi sana ambao wanasaidia, wengi wao hata hawahitaji kujitangaza. Kwa mfano hadi leo kuna kikosi cha JWTZ kiko kule kimejichimbia kikijenga madaraja na barabara ambayo imebomolewa. Sijasikia Mwamunyange akitamba sehemu jinsi alivyosaidia. Tunataka watu kama hao, chapa kazi, sifa itakuja baadaye.
 
Ama kweli nyani haoni kundule.... Hivi wewe staili yako ya kuchangia mada hapa JF unaijua? Posti zako zote zimekaa kijazba na kichuki, ukifahamishwa unakimbilia kulia lia..

nashukulu kwa kunikosoa....hujanirudisha nyuma hata kidog,,ila unasaidia kunijenga kifikra...ama kweli "mtu hajijui sifa zake ni watu ndio huzijua" ni wakati wako na wewe kuzijua sifa zako
 
maneno mazito hayo; tatizo ni kuwa siasa za Kyela zinahistoria ambayo watu wengi kitaifa hawazijui na hazijapata exposure kama siasa za Upareni na Dayosisi ya Arusha.

Siamini kuwa masuala ya kisiasa ya Kyela ni ya siasa tu na hakuna elements nyingine hasa baada ya sakata la dayosisi ya Rungwe???

Binafsi naamini itakuwa vizuri sana kuleta mkuu wa mkoa mwingine kabisa Mbeya itasaidia sana kuzima haya baadhi ya maneno kwani siyo tu yameingilia siasa za wilayani (Kyela) bali pia za mkoani na ambazo zinanukia hadi kwenye Taifa.
 
Matatizo yanakuwa makubwa pale kiongozi wa mkoa anakuwa anatoa mkoani hapo. Mfano: Daniel Ole Njolay alipokuwa Arusha migogoro ilikua mingi. Mzee Mashishanga alipokuwa Mwanza matatizo kila kukicha, na sasa huko Mbeya n.k

Chanzo cha matatizo ni wivu kwamba kwa nini niendeleze Mbozi wakati kwetu Tukuyu hakujaendelea

Sababu ingine inaweze kana ni kutaka kujiona yeye ni Rais wa mkoa so na yeye ni bora kuliko wengine(watu wa kabila au mkoa wake)na anaweza kuwaamulia jinsi anavyojisikia so vyote vinachangia kuwa na migogoro katika mikoa hiyo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom