Serikali yamuonya Cyprian Musiba kuacha kuhusisha harakati zake na Serikali au kuwa Rais anamtuma. Musiba ajibu yupo tayari kukamatwa

Nimesikia waziri mwenye dhamana alisema Musiba hajatumwa na serikali ila anajifanyisha. Musiba hajawahi tamka kuwa katumwa na mtu.

Sikuzote anasema ni mwanaharakati huru anayezikubali kazi za jpm. Sasa shida iko wapi? Anachokifanya ni kuwataja watu ambao kwa mtizamo wake wako kinyume na jpm. Sasa Kama kumtetea jpm ni kosa mbona wanaomkosoa iweje waachwe?

Mtu kusema kuna mtu kapiga hela nssf Kuna shida gani? Mbona wao wanasema Kuna 1.8trln imeyoyoma na tuko kimya?

Kumbuka tuko wengi tunaomtetea jpm na wala hatuhitaji atutume.
Wazo jema sana
 
Lugola ni mnafiki kabisa.
Watanzania wanataka kusikia majibu ya haya maswali makubwa manne.

1/Kwanini Musiba hakamatwi, haojiwi wala kushtakiwa kwa taarifa zake za uchochezi na kuchafua watu?

2/Kwanini muda wote huo, serikali imekuwa kimya wakati Musiba akiropoka madudu yake?

3/Kwanini magazeti ya Musiba yanayotumika na Musiba kuchafua na kuchochea hayaonywi wala hayafungiwi?

4/Kwanini mpaka leo hii bado serikali ya awamu ya tano inatumia magazeti ya Musiba kutoa matangazo yake, huku ikilipa pesa nyingi na sote tukijua ni magazeti yasiyosomwa na watu wengi na yanatumika kwa uchochezi?

Sote tunajua wazi kuwa Musiba alikuwa anatumwa na watawala, kazi yake imeshakwisha, hivyo haitajiki tena, labda atapewa kazi nyingine ya kufanya.
 
Tutaona na kusikia mengi mwaka huu!
Lugola limemfika hapa. Hana jinsi. Tusubiri jibu la Musiba. Musiba alishajipambanua long time kuwa yeye hatumwi na Serikali. Iweje leo Lugola amwambie Musiba kuwa aache kujisema anatumwa na Serikali. Lugola kama hujafanya chochote jimboni jiandae kulitema jimbo.
 
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
Naona Diwani hacheki na kimaa
Musiba ni Spika ambayo umeme wake unatoka moja kwa moja kwenye Transfoma.

Lugola ajiangalie
kwani Lugola kaagizwa na nani?!
 
Hata CAG Assad pia akiandika tuhuma nzito dhidi ya huyo kubwa la majizi kuhusu kupotea 1.5 trillion za walipa kodi, kuhusu kuchota trillions hazina na kuzitumia atakavyo bila kuidhinishwa na Bunge, kuhusu kugomea ukaguzi wa pesa za walipa kodi na uchunguzi wa 1.5 trillion pia HUMUELEWI.

Huwa siwaelewi. Kigogo wa Twitter akiandika tuhuma ni shujaa, anasifiwa. Mange akiandika tuhuma ni shujaa wa Taifa. Musiba akizungumza tuhuma, anachafua nchi ni mhuni.
 
Kuna kitu naanza kukiona,, ni wazi kuwa kuna janga linakwepwa hapo, Musiba hajaanza kuongea upuuzi Jana wala leo Mh Kangi Lugola haianza idara yake leo wala Jana kwanini tamko liwe leo ni kweli walikuwa hawalioni siku zote ni mangapi ameongea ya uchochezi hajawahi hata kuulizwa wala kukemewa, kuna nini? Dhahiri kuna janga linamkaribia Musiba sasa wanataka kujiosha kuwa hawafamu utendaji wake,, nilitaka nione alikamatwa na kifunguliwa kesi halali za uchochezi tofauti na zakina Mbowe, Lissu, Mdee, Zitto na wengine,, ni wazi kuwa ngao inayomlinda ndiyo inaendelea kumlinda asishitakiwe zaidi anaonywa tu kama vile kafanya mambo ya kawaida sana,, tufikie kipindi wa tz tuelewe watu na dhamira zao ili iwe rahisi kuwatupilia mbali muda ukifika
Wanabodi mabadiliko TISS sasa yanaonekana, Musiba apewa onyo kali Leo na kangi lugola

Kila kitu na zama zake, Sasa ni zama za Musiba.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema kwamba


''Nimuonye huyu Cyprian Musiba kuacha kuhusisha harakati zake na Serikali au kuwa Rais anamtuma. Serikali hatuwezi kufanya kazi kwa kuwatuma wanaharakati kutusemea. Imefikia wakati viongozi wa dini wanaandika waraka wakidhani Serikali inabariki mambo yake.''

 
Musiba ni kama kondom,baada ya matumizi Sasa inatupwa.
Tamko limechelewa mno kutolewa damage kubwa zilishanyika kubwa mno za kutisha
Musiba aweza kutolewa Kama mbuzi wa kafara chap chap.Damage aliyofanya Ni kubwa mno.Wenyewe watakuwa wameona sotuation imeshakuwa out of control .Muda mchache mambo ni mengi .Cost ya kurepair na KU manage damage ngumu na muda hautoshi .Ni zima Moto approach ambayo kila kitu kinawekana kikiwemo Musiba kutolewa kafara Kama strategy ya KU manage crisis walau in short time period.Lakini naona Kama Ni too late .Anyway let us wait and see how far this short time strategy will work and what will be the size of the results .
 
Lugola limemfika hapa. Hana jinsi. Tusubiri jibu la Musiba. Musiba alishajipambanua long time kuwa yeye hatumwi na Serikali. Iweje leo Lugola amwambie Musiba kuwa aache kujisema anatumwa na Serikali. Lugola kama hujafanya chochote jimboni jiandae kulitema jimbo.
Ni kweli! Muda wote watu wanatukanwa na kudhalilishwa alikuwa wapi kukemea? Why leo?
 
Back
Top Bottom