.....Naomba Mbowe na jeshi lake (Zitto,Slaa),hawa nawaamini,fuatilieni hili.Wandishi wa habari fuatilieni na andikeni hili.......
Tarehe 13,Jan,2009 katika mzani wa Kihonda Morogoro,Ezekiel Paschal (incharge) aliruhusu gari lenye namba za usajili T395AMC/T387ASC mali ya ndugu Benedict John Mberesero lililozidi tani 19.1 na kustahili faini ya Tsh.5 million,ambazo ziliandikwa ktk kitabu cha faini (TFN No.5060489).Katika hali ya kutia shaka gari hilo liliruhusiwa kuondoka bila kulipa faini.Habari hizo zilifika kwa Manager Tanroads Morogoro (Mr.Madinda)ambaye aliwasiliana na Technician Kattani (mlokole) aliyekuwa msimamizi wa mizani ambaye aliamua kulifuatilia hilo gari hadi Dumila na kuliamuru lirudi,hata hivyo dereva alikataa na kutishia kumwua Kattani hali iliyopelekea kuagizwa mzani wa kuhamishika uletwe Dumila ili wapime upya.Habari zilipofika Kihonda,Ezekiel Paschal kwa kushirikiana na mhasibu waliharibu mzani na kuandoka na baadhi ya sehemu zake hadi Dumila.Hivyo zoezi la kurudia upimaji halikufanikiwa na gari likapelekwa polisi na usiku kwa hali ya kutia shaka tena mzigo (mbao) ulifaulishwa.Paschal anatuhuma nyingine ya rushwa kwa gari lililokuwa na Abnormal load lenye namba T476AHL/T261ADM liloandikwa kwenye kitabu TFN. No 5060489.Yeye alifuta na kuchukua rushwa kisha akaruhusu gari.
Baada ya hatua kadha wa kadha,tarehe 19 jan 2009,baraza husika liliamua kumsimamisha kazi KWA MASLAHI YA TAIFA.Waliohusika na na kikao hicho ni pamoja na:
HoE. Eng.Tano Massaba,
HoPl.Eng.Benedicto Kinjoli,
HoA & Adm. Athuman Kambi,
Tech.Musa Kattani.
Waliandaa barua ili wamkabidhi Paschal hata hivyo hakupatikana hata kwa simu.
Tarehe 23jan2009,siku 3 tu baada ya kufukuzwa Paschal ambaye ni kibarua,Chief Executive wa Tanroads Ndg.Ephraim Mrema aliandika barua yenye Kumb no.TRD/HQ/E/01 na kichwa cha barua STAFF TRANSFERS yenye kuhamisha baraza lote lililohusika na kumfukuza kazi Ezekiel Paschal.
Hapa kuna kila dariri za rushwa! Kati ya Paschal na CE. Mrema,Serikali imekosa mil 5 kwa mkono wao.Kwani hata hivyo Paschal kanunua magari mawili ya kutembelea ndani ya mwaka mmoja kitu kinachotia shaka kwani mshahara wake ni Tsh 160,000/= tu.
Na uhamisho huu nimeutazama kama ni wa adhabu kwa WAFANYAKAZI WAAMINIFU KWA MASLAHI YA WACHACHE WASIOWAMINIFU japo ni kawaida kwa mfanyakazi kuhamishwa.Nawaita waminifu kwa sababu hata mmoja wao Musa Katani alishapewa jina (nick name) Mlokole kwa sababu hataki rushwa...Haki iko wapi??
Haya sasa wale watu wangu "ANTUFISADI" shughulikieni hili.Na nyie wandishi nendeni ofisi za Tanroad Dar na Moro mpate habari muandike,tupigeni kelele hadi ufisadi utokomee.Na nyie PCCB fanyeni kazi hapo kwani nimewapa vielelezo.