Serikali yamsimamisha Kazi Mkurugenzi MSD

Hakuna uwajibikaji kutoka kwa waziri ambaye anatakiwa awe alama ya uadilifu, uwajibikaji kwa wizara yake. Kinachofanyika ni kutafuta kafara ili waziri aendelee kutetea ugali wake. Aibu tupu.
 
Sijui kama ni lazima kuwa na Hussen Mwinyi na Nchimbi ktk baraza la mawaziri?

Kila aendako Mwinyi anaonekana kuwa ni failure. Wizara ya afya, Ulinzi kote ni hvyo tu. Hata ukimuangalia usoni haonyeshi kuwa mtu anayeweza kufundishika.

BAdo anapewa wizara kama hii? Get this hell out of our way!
 
Huyu waziri kweli ni janga hakuna mahali ameonyesha kufanikisha shughuli hata moja. Hebu check milipuko ya mabomu Mbagala na Gongo la mboto. Huyu jamaa uwezo wake no duni fuatilieni kwa watu wake wa karibu watawambieni juu ya uwezo wa huyu jamaa
 
Huyo mkurugenzi hana jina?
mr.mgaya mmarekani mwenzako,kabeba sana mabox huko!jee mmiliki wa TPI kada wa ccm madabida kakamatwa?maana hilo ni deal sii bahati mbaya ka rebag dawa toka india!pia md wa TFDA vipi hajasimamishwa maana hula 2% ktk kila dawa ya msd
 
Kwa watu ambao tayari wametumia dawa ambazo ni chini ya kiwango, haki zao ziko wapi? Hapa kuna haja ya wahanga wa hizi dawa feki kuungana na kuweka wakili ili wapeleke mashitaka kunakostahili. Bila hivyo watu watageuza maisha ya watanzania kuwa biashara.
Kama Mh. Dr Nchimbi na Polisi walivyojidhihirisha wauaji wa Davidi Mwangosi!
 
Biashara ya madawa imeingiliwa na majambazi, juzijuzi nilikunywa vidonge vya amoxillin lakini cha ajabu nikakuta nikienda haja ndogo sipati ile harufu kali ambayo kwa kawaida ukinywa dawa hizo lazima utaisikia nikahisi tayari hili changa!
 
Ni kwa nini kamati ya Nchimbi imeendesha uchunguzi huku watuhumiwa wakiwa kazini? hii ni serikali Double standard.

Like!
Hali ilivyo sasa ni kwamba tume za uchunguzi zinaundwa na watuhumiwa na kusomwa mbele ya watuhumiwa au watuhumiwa wenyewe huku zikiwasafisha.
Tumeona ya Nchimbi na sasa hii ya Wizara ya Afya.
 
Hapo aliyetakiwa kuwajibika ni Waziri mwenyewe, then hatua nyinginezo zichukuliwe kwa watendaji wa chini.
 
Waziri wa Afya Dr Hussein Mwinyi ametangaza kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD pamoja na vigogo kadhaa wa idara hiyo kufuatia sakata la dawa bandia hasa ARVs.

Taarifa iliyotolewa idara ya Maelezo ni hii:

Serikali imewasimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD) ,Mkuu wa kitengo cha Udhibiti na Ubora na Afisa Udhibiti Ubora wa bohari hiyo ili kupisha uchunguzi dhidi yao kufuatia kuruhusu kusambazwa kwa dawa bandia za kupunguza makali ya UKIMWI aina ya TT –VIR 30 katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya nchini.

Aidha imepiga marufuku usambazaji na matumizi ya dawa aina ya TT –VIR 30 toleo na 0C .01.85 inayotengenezwa na kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) kufuatia dawa hiyo kutengenezwa chini ya kiwango na kutofaa kwa matumizi ya binadamu.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa mara baada ya kubaini kuwepo kwa dawa bandia ya kupunguza makali ya Ukimwi katika hospitali ya wilaya ya Tarime kufuatia ukaguzi uliofanywa na Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA).

Amesema kuwa ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara dhidi ya dawa hiyo isiyokidhi viwango ulibainia kuwa nyaraka zilizopo kuhusiana na dawa hizo unaonyesha kuwa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) waliiuzia Bohari ya Dawa (MSD) dawa hiyo bandia toleo namba 0C. 01. 85 iliyotengenezwa nchini mwezi Machi 2011 na kuonyesha mwisho wa matumizi yake mwezi Februari 2013.

Amefafanua kuwa dawa hiyo bandia ilikua na dawa zenye rangi mbili tofauti njano na nyeupe na kuwa na viambata tofauti vilivyopaswa kuwepo aina ya Efaverenz badala ya Niverapine, Lamivudine na Stavudine na kuongeza kuwa vidonge vilivyokutwa kwenye vifungashio vya dawa husika vilikua tofauti na vifungashio vilivyosajiliwa na TFDA.

Dkt. Mwinyi amesema kuwa serikali inahakikisha kuwa dawa zenye ubora unaotakiwa za kupunguza makali ya UKIMWI zinaendelea kupatikana katika vituo vya kutolea huduma kote nchini na kuwaagiza waganga wakuu wa mikoa, wilaya na kamati za dawa na Tiba katika vituo vya huduma za afya kuhakikisha kuwa zinapokea, kuhakiki na kusimamia kikamilifu ubora na matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba nchini.

Kuhusu upatikanaji wa dawa hizo amewatoa hofu wananchi na kuwahakikishia kuwa dawa za kutosha zenye viwango stahili zitaendelea kupatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini na kuwataka wananchi kutoa kushirikiana na mamlaka husika kwa kutoa taarifa pale wanapobaini kuwepo kwa dawa zenye ubora wenye mashaka au uvunjifu wa sheria inayosimamia ubora na usalama wa dawa.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

Maoni yangu:
Uongozi wetu bado haujazingatia dhana nzima ya Dhamana ya Uongozi na Uwajibikaji.
Suala hili na lile la Nchimbi yalikuwa yanamesababishwa na sehemu kubwa ya Uongozi (Systemic), na sio watendaji wachache.
Kwa hiyo watuhumiwa walikuwa ni mawaziri wenyewe.
Cha kushangaza ni kuwa watuhumiwa ndio wameendesha uchunguzi na kutoa majibu.

Uandishi wa hovyo huuu! Hao waliosimamishwa majina yao ni kina nani? Isitoshe mfumo mzima wa ukaguzi wa Dawa wizarani ni mbovu. Wa kwanza alikuwa waziri ajiudhulu kupisha uchunguzi wa kina na haki

I hate Tanzania....mzaha kuanzia kwa raisi wamawaziri kila mtu mzaha mzaha tu
 
Wanaojua jinsi MSD imekuwa inaendeshwa mbona hatua dhidi ya huyu kiongozi zimechelewa sana? na kwanini MSD wapewe monopoly ya kusambaza dawa nchini wakatu uwezo hawana.

Obudsman mimi sioni tija katika utendaji wala mfumo wa namna ya MSD zaidi ya kuongeza ukiritimba sawa na na kuwa na TANESCO (moja) ambayo haikidhi haja za wananchi. Kampuni za kitanzania zenye sifa waombe vibali na waruhusiwe angalau makampuni kama matano makubwa na washindane kuboresha huduma zao kwa kusambaza dawa kwenye vituo vya afya na watanzania kwa ujumla.
 
Mkuu mimi hawa msd wamewahi nifanya vibaya kituoni kwangu nimeorder dawa zinazowafaa wagonjwa wangu wao wameniletea bbe wakati sikuorder wala sina wagonjwa wa scabies wala ukurutu.
 
Tetesi ya ufisadi huu ilianza mwaka 2011 mwezi june likapamba moto sana ktk mgomo wa madaktari wengi wetu hatukuchangia kulisemea kwa kujiona hatuhusiki! Sasa mmelisikia mpaka masikio yanawasha nani anajua waliokufa kipindi chote hiki hawakuchangiwa kupata vifo vya mapema kutokana na kutumia dawa hizi fake! ? lakini wakati ule walionekana KM na dhs wa MOHSW tu!! Bado wengi watapatikana.
 
Waziri wa Afya Dr Hussein Mwinyi ametangaza kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD pamoja na vigogo kadhaa wa idara hiyo kufuatia sakata la dawa bandia hasa ARVs.

Taarifa iliyotolewa idara ya Maelezo ni hii:

Serikali imewasimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD) ,Mkuu wa kitengo cha Udhibiti na Ubora na Afisa Udhibiti Ubora wa bohari hiyo ili kupisha uchunguzi dhidi yao kufuatia kuruhusu kusambazwa kwa dawa bandia za kupunguza makali ya UKIMWI aina ya TT –VIR 30 katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya nchini.

Aidha imepiga marufuku usambazaji na matumizi ya dawa aina ya TT –VIR 30 toleo na 0C .01.85 inayotengenezwa na kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) kufuatia dawa hiyo kutengenezwa chini ya kiwango na kutofaa kwa matumizi ya binadamu.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa mara baada ya kubaini kuwepo kwa dawa bandia ya kupunguza makali ya Ukimwi katika hospitali ya wilaya ya Tarime kufuatia ukaguzi uliofanywa na Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA).

Amesema kuwa ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara dhidi ya dawa hiyo isiyokidhi viwango ulibainia kuwa nyaraka zilizopo kuhusiana na dawa hizo unaonyesha kuwa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) waliiuzia Bohari ya Dawa (MSD) dawa hiyo bandia toleo namba 0C. 01. 85 iliyotengenezwa nchini mwezi Machi 2011 na kuonyesha mwisho wa matumizi yake mwezi Februari 2013.

Amefafanua kuwa dawa hiyo bandia ilikua na dawa zenye rangi mbili tofauti njano na nyeupe na kuwa na viambata tofauti vilivyopaswa kuwepo aina ya Efaverenz badala ya Niverapine, Lamivudine na Stavudine na kuongeza kuwa vidonge vilivyokutwa kwenye vifungashio vya dawa husika vilikua tofauti na vifungashio vilivyosajiliwa na TFDA.

Dkt. Mwinyi amesema kuwa serikali inahakikisha kuwa dawa zenye ubora unaotakiwa za kupunguza makali ya UKIMWI zinaendelea kupatikana katika vituo vya kutolea huduma kote nchini na kuwaagiza waganga wakuu wa mikoa, wilaya na kamati za dawa na Tiba katika vituo vya huduma za afya kuhakikisha kuwa zinapokea, kuhakiki na kusimamia kikamilifu ubora na matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba nchini.

Kuhusu upatikanaji wa dawa hizo amewatoa hofu wananchi na kuwahakikishia kuwa dawa za kutosha zenye viwango stahili zitaendelea kupatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini na kuwataka wananchi kutoa kushirikiana na mamlaka husika kwa kutoa taarifa pale wanapobaini kuwepo kwa dawa zenye ubora wenye mashaka au uvunjifu wa sheria inayosimamia ubora na usalama wa dawa.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

Maoni yangu:
Uongozi wetu bado haujazingatia dhana nzima ya Dhamana ya Uongozi na Uwajibikaji.
Suala hili na lile la Nchimbi yalikuwa yanamesababishwa na sehemu kubwa ya Uongozi (Systemic), na sio watendaji wachache.
Kwa hiyo watuhumiwa walikuwa ni mawaziri wenyewe.
Cha kushangaza ni kuwa watuhumiwa ndio wameendesha uchunguzi na kutoa majibu.

Mbona sioni ni hatua gani wamechukuliwa hawa Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI)? Waziri amekiri kuwa wamehusika kusambaza hayo madawa feki.
 
Uandishi wa hovyo huuu! Hao waliosimamishwa majina yao ni kina nani? Isitoshe mfumo mzima wa ukaguzi wa Dawa wizarani ni mbovu. Wa kwanza alikuwa waziri ajiudhulu kupisha uchunguzi wa kina na haki

I hate Tanzania....mzaha kuanzia kwa raisi wamawaziri kila mtu mzaha mzaha tu

This is a reporting.
Uandishi ni wa idara ya habari Maelezo.
 
Back
Top Bottom