Serikali yamsimamisha Kazi Mkurugenzi MSD | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yamsimamisha Kazi Mkurugenzi MSD

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Goodrich, Oct 10, 2012.

 1. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Waziri wa Afya Dr Hussein Mwinyi ametangaza kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Joseph Mgaya, pamoja na vigogo kadhaa wa idara hiyo kufuatia sakata la dawa bandia hasa ARVs.

  Taarifa iliyotolewa idara ya Maelezo ni hii:

  Serikali imewasimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD) ,Mkuu wa kitengo cha Udhibiti na Ubora na Afisa Udhibiti Ubora wa bohari hiyo ili kupisha uchunguzi dhidi yao kufuatia kuruhusu kusambazwa kwa dawa bandia za kupunguza makali ya UKIMWI aina ya TT –VIR 30 katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya nchini.

  Aidha imepiga marufuku usambazaji na matumizi ya dawa aina ya TT –VIR 30 toleo na 0C .01.85 inayotengenezwa na kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) kufuatia dawa hiyo kutengenezwa chini ya kiwango na kutofaa kwa matumizi ya binadamu.

  Akizungumza leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa mara baada ya kubaini kuwepo kwa dawa bandia ya kupunguza makali ya Ukimwi katika hospitali ya wilaya ya Tarime kufuatia ukaguzi uliofanywa na Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA).

  Amesema kuwa ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara dhidi ya dawa hiyo isiyokidhi viwango ulibainia kuwa nyaraka zilizopo kuhusiana na dawa hizo unaonyesha kuwa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) waliiuzia Bohari ya Dawa (MSD) dawa hiyo bandia toleo namba 0C. 01. 85 iliyotengenezwa nchini mwezi Machi 2011 na kuonyesha mwisho wa matumizi yake mwezi Februari 2013.

  Amefafanua kuwa dawa hiyo bandia ilikua na dawa zenye rangi mbili tofauti njano na nyeupe na kuwa na viambata tofauti vilivyopaswa kuwepo aina ya Efaverenz badala ya Niverapine, Lamivudine na Stavudine na kuongeza kuwa vidonge vilivyokutwa kwenye vifungashio vya dawa husika vilikua tofauti na vifungashio vilivyosajiliwa na TFDA.

  Dkt. Mwinyi amesema kuwa serikali inahakikisha kuwa dawa zenye ubora unaotakiwa za kupunguza makali ya UKIMWI zinaendelea kupatikana katika vituo vya kutolea huduma kote nchini na kuwaagiza waganga wakuu wa mikoa, wilaya na kamati za dawa na Tiba katika vituo vya huduma za afya kuhakikisha kuwa zinapokea, kuhakiki na kusimamia kikamilifu ubora na matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba nchini.

  Kuhusu upatikanaji wa dawa hizo amewatoa hofu wananchi na kuwahakikishia kuwa dawa za kutosha zenye viwango stahili zitaendelea kupatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini na kuwataka wananchi kutoa kushirikiana na mamlaka husika kwa kutoa taarifa pale wanapobaini kuwepo kwa dawa zenye ubora wenye mashaka au uvunjifu wa sheria inayosimamia ubora na usalama wa dawa.

  Na. Aron Msigwa –MAELEZO.


  Maoni yangu:
  Uongozi wetu bado haujazingatia dhana nzima ya Dhamana ya Uongozi na Uwajibikaji.
  Suala hili na lile la Nchimbi yalikuwa yanamesababishwa na sehemu kubwa ya Uongozi (Systemic), na sio watendaji wachache.
  Kwa hiyo watuhumiwa walikuwa ni mawaziri wenyewe.
  Cha kushangaza ni kuwa watuhumiwa ndio wameendesha uchunguzi na kutoa majibu.

   
 2. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Na yeye anasubiri nini?Magamba bwana,yanawaza kunenepeana na kula hela za kodi basi,sio kuwajibika!
   
 3. k

  kisimani JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 553
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Haya, kweli CDM imefanya kazi kubwa...
   
 4. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Hata waziri mwenyewe alipaswa kujiuzulu.
   
 5. m

  mwamola Senior Member

  #5
  Oct 10, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zamu waziri wa fedha nawe simamisha watumishi wako kwakutolipa salary arreas za wafanyakazi wa higher learning institutions kufuatia promotions zao
   
 6. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,970
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Kiwanda chenyewe mwenye nacho ni mwana magamba,unategemea nini?angetakiwa mwenyekiwanda nae asweke lupango tu,kwani ni muuaji,ingekuwa china wote huyu wa MSD na mwenyekiwanda wote shaba tu
   
 7. josefast

  josefast JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  system yote ni corupt dawa yao 2015
   
 8. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Usentee uliotukuka. Huyo Waziri anafanya nini bado kazini!? Kila anakopelekwa ni majanga tuuu! Nchi hii!?
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa watu ambao tayari wametumia dawa ambazo ni chini ya kiwango, haki zao ziko wapi? Hapa kuna haja ya wahanga wa hizi dawa feki kuungana na kuweka wakili ili wapeleke mashitaka kunakostahili. Bila hivyo watu watageuza maisha ya watanzania kuwa biashara.
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,271
  Trophy Points: 280
  Ni kwa nini kamati ya Nchimbi imeendesha uchunguzi huku watuhumiwa wakiwa kazini? hii ni serikali Double standard.
   
 11. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa kweli alikua ameupata ukurugenzi akiwa mdogo tena sehemu nyeti, lakini tena si unajua vijana kwa kujisahau they give him an inch then he wanted the whole yard
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo walikuwa wanamtafuta huyo MD/DG wa MSD maana zile dawa za Bil 9 zilioza ndani ya bohari wakati watanzania wanakufa kwa kukosa dawa...ni kashfa nzito sana,wakamtafutia soo ameingia line.
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hivi jk kwa nini naye asijuuzuru kupisha uchunguzi
   
 14. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kuwafukuza kazi tu? Nani anajua kuwa wakati wanafanya hiyo dili walilijua hilo na walishapima kufukuzwa kazi na rushwa waliyopewa kwenye hiyo wakaona hata wakifukuzwa kazi watakuwa wameshafaidika sana tu? Kwanini wasifunguliwe Mashtaka na kama ushahidi wa kutosha upo wafungwe ili iwe fundisho kwa wengine?
   
 15. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Hii ndiyo tatizo ya wataalamu wa kitanzania badala ya kujikita ktk mambo ya maana kwa jamii na taifa wako busy na siasa uchwara! Ningetarajia Ramadhan Madabida na mkewe Zarina Shamte wangetumia muda wao mwingi kusimamia kiwanda chao,lakini wako busy na mipasho ya CCM. Sitashangaa kama hiyo ilikua ni hujuma toka wafanyabiashara wenzao wenye asili ya Asia!
   
 16. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Pambafu kabisa, kupisha uchunguzi gani wakati madawa yapo mtaani na yamefahamika, kusimamishwa kazi(likizo ya malipo siyo?) waziri angekuwa na akili sawasawa na kujua mamlaka yake huyo mkuu wa msd na tfda ni wa kufukuzwa mara moja na kufikishwa mahakamani mara moja, ushahidi ni madawa yaliyo mtaani ,adhabu yao iwe kifo wakanyongwe hadharani mnazi mmoja au msimbazi center ili liwe onyo kali sana
   
 17. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Uandishi kanjanja huu. Huwezi kuandika mtu amefukuzwa kazi halafu hata jina lake hutaji??? Huyo aliyefukuzwa anaitwa nani?
   
 18. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Tanzania tunahitaji kiongozi kichaa kimaamuzi otherwise hao sisiemu watatutia hadi vidole vya macho....Hao watu sio wakusimamisha ni kuwekwa lupango tu!!!
   
 19. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,096
  Likes Received: 1,714
  Trophy Points: 280
  Hii ndio raha ya Tanzania,ni mwendo wa unafiki tu! Kama vipi na tume iundwe! Shame on them!
   
 20. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu alishawahi sema Tanzania inahitaji Rais mwenye mkono wa chuma yaani yeye adhabu zake ni vyuma kama sio nondo za jela basi shaba
   
Loading...