Serikali yamnyang'anya Tibaigana gari linalotuhumiwa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,098
Date::8/11/2008
Serikali yamnyang'anya Tibaigana gari linalotuhumiwa

Na Mwandishi Wetu
Mwananchi

SAKATA la mauaji yenye utata ya vijana wawili, wakazi wa Dar es Salaam, Mine Chomba na Hija Shaha Salehe, yaliyotokea mwaka 2006, limechukua sura mpya baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrance Masha, kuagiza magari yote yaliyohusishwa na mauaji hayo, likiwamo analomiliki Kamanda wa zamani wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, kurudishwa ili uchunguzi ufanyike upya.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Waziri Masha, zinaeleza kuwa, magari hayo tayari yamesharejeshwa kwa ajili ya kufanyika uchunguzi kuhusiana na jinsi yalivyochukuliwa.

Inaelezwa kwamba, magari hayo yanayodaiwa kuwa mali ya marehemu Chomba, yalikamatwa na Polisi kwa muda mrefu, yakidaiwa kuwa ni ya wizi kabla ya kuuzwa kwa njia ya utata.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu juzi, Waziri Masha alisema kuwa, magari hayo yote yamesharudishwa kama alivyoagiza.

"Kama mlisikia wakati wa hotuba ya bajeti yangu bungeni, niliagiza magari yote yarudishwe na tayari yamesharudishwa," alisema Waziri Masha.

Kati ya magari hayo yaliyopaswa kurudishwa ni pamoja na Toyota RAV 4 ambalo lilinunuliwa kwenye mnada wa hadhara na Tibaigana.

Hata hivyo, habari zilizopatikana kutoka kwa ndugu wa marehemu Mine, zinaeleza kuwa, tayari walishakwenda kumwona Waziri Masha kujua hatima ya suala la ndugu yao.

Mmoja wa ndugu hao, ambaye hakupenda kutajwa jina lake, alisema kuwa, walikwenda hivi karibuni kumwoma Waziri Masha na kwamba alisema ameshalishughulikia suala hilo kwa kuagiza magari hayo yarejeshwe.

Hata hivyo, Tibaigana aliwahi kukaririwa na vyombo vya habari huko nyuma, akisema kwamba, gari hilo alilinunua kwa njia ya halali kupitia mnada wa hadhara.

Mine aliuawa Januari 13, mwaka 2006 katika baa ya Meeda, Sinza, Dar es Salaam, mauaji ambayo yanadaiwa kufanywa na Hija, ambaye aliuawa Januari 16 mwaka huo huo katika eneo la Kimara Temboni.

Baada ya kutokea mauaji hayo, ndugu walilalamikia mazingira ya vifo hivyo, wakidai kuwa yalifanywa na Polisi, madai ambayo yalimlazimu aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Raia, Harith Bakari Mwapachu, kuunda tume ya kuchunguza mauaji hayo.

Hata hivyo, ripoti ya uchunguzi huo haikutolewa hadharani na badala yake Mwapachu aliipeleka Ikulu kwa ushauri zaidi kutokana na kuhusisha majina ya baadhi ya vigogo wa polisi.

Utata huo, pia ulifanyika katika Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) na Mwapachu mwenyewe kuunda tume, kwa kuwa, Hija, ambaye aliuawa kinyama kifo chake kilitokea akiwa katika mikono ya polisi, lakini baadaye akaelezwa aliuawa na wananchi wenye hasira huku Mine akidaiwa kuuawa na Hija, lakini ndugu wanakataa wakidai wahusika ni polisi.

Hata hivyo, juhudi za Mwananchi kumpata Tibaigana kuzungumzia suala hilo jana hazikufanikiwa na hata alipopigiwa simu zake mbili za mkononi, zote zilikuwa zimezimwa.
 
Kwa watu wote waliokuwa karibu na marehemu Mine wanaujua ukweli kwamba Kamanda Tibaigana alihusika katika Mauaji ya Mine....Yale Magari yalipochukuliwa nyumbani kwa Mine (Mwenge) watu walijua pia kuwa yatakwenda kwa Mzee Tbaigana.Marehemu Mine alikuwa mshiriki wao katika biashara za Uizi....Hakuna asiyemfahamu Mine toka Mwenge,Sinza,Survey mpaka Mikocheni..Huyu Jamaa pamoja na uizi wake,lakini alikuwa mtu wa watu katika matukio yote,iwe Harusi hata Misiba.Na ndio maana msiba wake uliwagusa watu wengi.

Waziri Masha anaujua ukweli,kwa sababu alipokuwa University of Dsm (USDM) wakati wa masomo yake ya Masters alikuwa kwa wakati tofauti anakutana na Mine na alijua wazi Mine ni nani katika maeneo ya Mwenge,Sinza na Makongo.Huyu Jamaa alikuwa ana-hang na wanafunzi wa Chuo Kikuu kwa wakati wingi,akitumia cover la Ufanyabiashara kwenye kampuni ya Saba Auto Spares.Hata alipokwenda TOL Waziri Masha alikuwa bado anamjua Mine kutokana na kunywa Maryland na Namanga kwa Kimicho.Mauaji yake yalishtua watu wengi,kwa sababu yalimuhusisha rafikiye Mkubwa Hija...kila mtu alijua kuwa kutakuwa na tofauti kwenye mgawanyo wa biashara zao,ilishtua zaidi Hija alipouawa na Mapolisi huko Kimara.....Kwa watu wa karibu walidai kuwa Hija ameuwawa kwa amri ya Mzee Tibaigana ambaye alikuwa kwenye Chain hiyo..

Kila mali ya Mine ilichukuliwa na Mapolisi na kumuacha mkewe Margreth bila kitu...huyu Dada alikuwa hamjui vizuri Mine,kwa sababu hakuwa mtoto wa mjini,alikwenda kuolewa huko Moshi,na kwa uhakika hakujua kazi za Mine alikuwa anamjua kana kwamba ni mmiliki wa Saba Auto Spares....Ndugu wa Mine wanaujua ukweli,ni miaka karibu mitatu sasa toka Mine afariki kinyama......Ni wazi Waziri kwa kutumia makachero wake wataangalia kwa undani uhusiano wa Marehemu na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la polisi Dsm Mzee Tibaigana...Kwa kuwa sasa hana madaraka serikalini ,Tuiache sheria ichukue mkondo wake,wale Polisi wote wanaohusika na vitendo vya Ujambazi wawajibishwe....Hongera sana Muheshimiwa Waziri,lakini juhudi zako zisiishie hapo...kuna matatizo mengi kwa watendaji wako...haswa hao Polisi,walio wengi ni majambazi.....
 
Huko Kimara kulikoni wafanya biashara wengi nimesikia wameuwawa Kimara; akiwamo Said Siwa aliyekuwa na Dalala nyingi jijini Dsm na Duka la Jumla pale JKN Airport. Zombe naye wale wafanyabishara si aliwapeleka Kimara??!!!
 
Kazi kweli kweli hilo ndio jeshi la polisi linalotegemewa kuwalinda WTZ.
 
Hata hivyo, ripoti ya uchunguzi huo haikutolewa hadharani na badala yake Mwapachu aliipeleka Ikulu kwa ushauri zaidi kutokana na kuhusisha majina ya baadhi ya vigogo wa polisi.

Yale Yale.....
 
Back
Top Bottom