Serikali yamng'ang'ania Msaidizi wa Sabaya

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Kesi ya Unyang’anyi wa kutumia Silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro ,Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili Leo imeshindwa kuendelea baada ya mabishano makali ya kisheria kuzuka mahakamani hapo pale Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali,Tumaini Kweka kunukuu maelezo ya mshitakiwa wa kwanza aliyoyatoa polisi baada ya kukamatwa mw 27 mwaka huu akiyatumia kumhoji mshtakiwa wa pili Silvester Nyegu hatua hiyo ilipingwa vikali na mawakili wa utetezi kuwa ni kinyume na sheria .


Wakati akiongozwa na wakili Silvester Kahunduka,Mshitakiwa wa pili,Silvester Nyegu{27} alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi ,Odira Amworo kuwa hakuwahi kuhojiwa,kutoa maelezo wala kujulishwa kosa alilokamatiwa mahali popote ikiwemo kituo cha Polisi Arusha au Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa {TAKUKURU} Upanga Jijini Dar es Salaam hadi alipofikishwa mahakamani Arusha kujibu mashitaka yanayomkabili juni 4 mwaka huu.

Wakili Kahunduka alidai kuwa Mwendesha Mashitaka wa Serikali amekosea kisheria kwani maelezo anayoyanukuu katika taarifa ya maelezo ya aliyoyatoa polisi mshitakiwa wa pili sio kielelezo cha ushahidi katika kesi hiyo hivyo alimtaka Hakimu kumzuia kufanya hivyo mara moja kwani ni kinyume cha sheria.


Akijibu hoja hiyo ,Kweka alionyesha kushangazwa na uelewa wa mawakili wasomi Kahunduka na Edmund Ngemela wanaomtetea mshitakiwa wa pili na kudai kuwa kwanza hajaiwasilisha nyaraka hiyo na pili bado anainukuu nje ya uwanja kwa mujibu wa sheria namba 154 ya sheria ya jinai ya ushahidi.


Kweka alisema alichofanya ni kunukuu taarifa binafsi za mshitakiwa au shahidi wa upande wa utetezi na kama atataka kuiwasilisha nyaraka hiyo atafuata sheria lakini kwa sasa hawezi kufanya hivyo kwani anajua sheria na miongozo ya mahakama.

Baada ya malumbano hayo yaliyochukuwa takribani dakika 60 Hakimu Amworo alihairisha kesi hiyo hadi agosti 23 mwaka huu ndipo atakapotoa uamuzi mdogo wa mabishano hayo ya kisheria.





Awali kabla ya kuhairishwa kwa kesi hiyo,Nyegu alidai mahakamani hapo kuwa hakuwahi kuhojiwa polisi wala Takukuru na alidai kuwa yeye sio Msaidizi binafsi wa Sabaya lakini akiri kumfahamu Sabaya kama Mkuu wa Wilaya ya Hai.


Akihojiwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali ,Baraka Mgaya,Nyegu alikumbushwa kuwa wakati akisomewa maelezo ya awali{Ph} alikiri kuwa yeye ni Msaidizi binafsi wa Sabaya lakini wakati anahojiwa alikataa wadhifa huo na kuulizwa kama ana tatizo la kupoteza kumbukumbu, mtuhumiwa huyo alidai kuwa yuko vizuri na hana shida


Akihojiwa na wakili Kweka aliuzwa kama anajua adhabu ya shitaka linalomkabili Mahakamani iwapo atatiwa hatiani ,Nyegu alidai kuwa ni kifungu Cha Maisha au kifungu Cha miaka 30 jela


Kweka alimuuliza Nyegu kuwa kama anajua madhara la kutoa ushahidi wa uongo Mahakamani na shahidi alidai anajua madhara yake Ila yeye anasema ukweli kwa sababu anamwamini mungu na ameapa kwa Bibilia kusema ukweli mtupu.p


Alipokuwa akijianda kununukuu sehemu ya taarifa ya maelezo yake aliyoandika polisi baada ya kukamatwa mei 27 mwaka huu Upanga Jijini Dar es Salaam ndipo wakili wa Mshitakiwa, Silvester Kahunduka alipinga na kudai kuwa kielelezo hicho hakipo kisheria. Kesi inaendelea agosti 23 mwaka huu.






FB_IMG_1629347302879.jpg
 
Kumbe serkali wamejipanga kushindwa.
Mtu yuko polisi halafu ushahidi alioutoa polisi unauwasilisha mahakamani je kamq alikuwa anautoa kwa vipigo na vitisho?
 
Back
Top Bottom