Serikali yamlipa mkandarasi anayejenga uwanja wa ndege wa kimataifa wa JNIA (terminal 3) fedha zote

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
WIZARA YA FEDHA YAMLIPA MKANDARASI ANAYEJENGA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE (TERMINAL 3) FEDHA ZOTE ANAZODAI.
5.jpg

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza na Wanahabari kuhusu Wizara yake ilivyotekeleza Agizo la Rais Dkt. John Magufu kuhusu kumlipa Mkandarasi ayejenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3).

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Doto James, Wizara ya Fedha na Mipango imemlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa upanuzi wa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(Terminal 3) Kampuni ya BAM International kiasi cha Euro Milioni 9.5 sawa na zaidi ya Tsh. Bilioni 22 za Kitanzania mara baada ya kuhakiki madai hayo.

Katika Hatua nyingine Wizara ya Fedha inaandaa Malipo ya awali (Advance Payment) kiasi cha Tsh. Bilioni 300 kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Kutumia Umeme na Mafuta(Standard Gauge) katika awamu ya kwanza itakayoanzia kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro katika awamu yake ya kwanza ya Ujenzi huo.
 
Hii Serekali ya kisanii sana!! Haiaminiki kabisa! Wazabuni na makandarasi wanaoidai ili wapate pesa yao au kujibiwa madai yao lazima kwanza walalamike kwenye vyombo vya habari!! Hii serekali ni mufilisi na hapo ukute kapigwa biti Tulia tunaenda kusema tumekupa kiasi hichi mambo mengine tutamalizana! Nakwambia hii serekali Haiaminiki kabisa hata na mtoto wa primary!!
 
Kumbe tatizo lilikuwa ni kutokulipwa pesa?
Kumbe ukitaka kulipa deni unatafuta kwanza namna ya kupata kick
Sasa apo ni kipi cha kusifia? Maana ni lazima hela kulipwa na sio hisani ya mkuu

Au mlitaka hiyo project aliyoikuta imeshaanzwa na hela zimeshatoka ifie njiani?

Sio kila kitu cha kupatia kick
 
Hii sio habari nzuri kwa wenzetu wa upande ule ambao wamegeuka "bad news maker"
 
Hii Serekali ya kisanii sana!! Haiaminiki kabisa! Wazabuni na makandarasi wanaoidai ili wapate pesa yao au kujibiwa madai yao lazima kwanza walalamike kwenye vyombo vya habari!! Hii serekali ni mufilisi na hapo ukute kapigwa biti Tulia tunaenda kusema tumekupa kiasi hichi mambo mengine tutamalizana! Nakwambia hii serekali Haiaminiki kabisa hata na mtoto wa primary!!


Umeandika kwa msisistizo kweli na kwa hamaki inaonyesha jinsi ulivyokuwa umewekeza kwenye hili kwamba ulitaka uwanja wetu mpya ubakie magofu ili uje kusema ulivyosema pole sana, Ujenzi unaendelea na uwanja utaisha!
 
Kama pesa ilikuwepo kwaninu isilipwe katika utaratibu wa kawaida bila kusubiri shinikizo la mkandarasi kusitisha ujenzi na kupelekea agizo ka Rais?! Kama kila kitu kitasubiri personal intervention ya Rais basi tunakwenda kukwama korongoni !! God save my country!
 
Huyu ndiye baba na mtoto tutaona mengi awamu hii"

Wanapanga pesa za matumizi kwa jinsi wanavyotaka bila bunge wala nini.......

Masikini Tanzania elimu, elimu, elimu.....
wewe ni mchawi........HIVI KAMA WASINGEKUWA WAMELIPWA UNGESEMA VIPI KWENYE UZI HUU???.......
 
Back
Top Bottom