Serikali yamcharukia mwekezaji Mwadui yasitisha mauzo ya hisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yamcharukia mwekezaji Mwadui yasitisha mauzo ya hisa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 2, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,886
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Date::10/2/2008
  Serikali yamcharukia mwekezaji Mwadui yasitisha mauzo ya hisa
  Na Kizitto Noya
  Mwananchi

  SERIKALI imesitisha mauzo ya hisa za Kampuni ya Willcroft kwa kampuni ya Petra Diamonds katika Mgodi wa Williamson Diamonds limited (Mwadui) uliopo mkoani Shinyanga.

  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, mauzo ya hisa hizo ni batili kwa kuwa yamekiuka mkataba wa uchimbaji katika mgodi huo, uliotiwa saini baina ya Serikali na Kampuni ya Willcroft Oktoba 19, 1994.

  Alisema katika mkataba huo, mbia hatakiwi kuuza hisa zake bila kumjulisha mwenzake ambaye anatakiwa kupata fursa ya kwanza kununua na Kampuni ya Willcroft haikuijulisha serikali na kuipa fursa hiyo kama mkataba huo unavyotaka.

  "Willcroft hawajauza hisa zao na wala Petra Diamonds hawajanunua hizo hisa ndani ya mgodi wa (WDL) kwa kuwa Serikali haikupewa fursa yake ya kimkataba kununua hisa hizo kwa dola za Marekani 10 milioni," alisema.

  Septemba 9, mwaka huu kampuni ya Willcroft ilitangaza kupitia mtandao kuwa imeuza hisa zake ambazo ni asilimia 75 ya hisa zote za mgodi wa Williamson Diamonds kwa Kampuni ya Petra Diamonds.

  Kwa mujibu wa tangazo hilo, kuanzia tarehe hiyo mali na madeni yote ya Kampuni ya Willcroft vimekuwa vikirithishwa kwa Kampuni ya Petra Diamonds iliyochukua kampuni hiyo.

  Lakini Waziri Ngeleja jana alieleza kuwa tangazo hilo ni batili kwa kuwa limekiuka kifungu cha 6.1 cha mkataba wa ubia wa uendelezaji wa mgodi huo baina ya Serikali na Kampuni ya Willcroft kinachomtaka mbia anayetaka kuuza hisa zake ampe fursa ya kwanza mwenzake kuzinunua.

  "Kwa kuwa Willcroft hawakufuata wala kuzingatia utaratibu ulioainishwa kwenye mkataba wa ubia kati yake na Serikali, ni dhahiri kwamba hawajauza hisa zao," alisema.

  Alifanunua kuwa kuwa kilichofanyika ni kwamba Willcroft ambayo ni kampuni tanzu ya De beers ya Afrika Kusini, ndiyo iliyonunuliwa na Petra Diamonds kitendo ambacho hakihalalishi moja kwa moja uuzwaji wa hisa ndani mgodi wa WDL.

  Alisema ingawa serikali ilikuwa na taarifa za awali za kampuni ya Willcroft kutaka kuuza hisa zake, lakini hazikutolewa kiofisi wala kutoa fursa kwa serikali kuzinunua hisa hizo.

  Alifahamisha kuwa Machi, mwaka huu Serikali iliunda Kamati ya kisekta kufanya majadiliano na kampuni ya Willcroft kuhusu hatima ya mgodi wa WDL baada ya mgodi huo kukabiliwa na matatizo ya fedha za uendeshaji.

  Alisema wakati majadiliano hayo yanaendelea, Kampuni ya Willcroft iliwasilisha mapendekezo kwa serikali kuelezea nia yake ya kuuza hisa zake ambazo ni asilimia 75 kwa mwekezaji mwingine.

  "Serikali ilikubali ombi hilo na kuelekeza kwa barua kuwa uuzwaji huo ufanyike kwa kuzingatia kifungu namba 6.1 cha Mkataba wa ubia wa Oktoba 19, 1994 kinachomtaka mbia kumpa kwanza mwenzake fursa ya kununua kabla ya kuuza," alieleza.

  Ngeleja alieleza kuwa tangazo la kampuni ya Willcroft kwamba imeuza asilimia 75 ya hisa zake kwa Kampuni ya Petra Diamonds kwa kuwa kampuni hiyo ndiyo iliyonunua madeni na hisa za Willcroft duniani kote sio sahihi kwa kuwa limekiuka mkataba wa mwanzo wa kuendesha mgodi huo.

  Alibainisha kuwa hakuna kosa wala tatizo kwa Kampuni ya Petra Diamonds kununua kampuni ya Willcroft, lakini kampuni hiyo mpya haiwezi kuendesha mgodi wa Mwadui bila kufuata taratibu za mkataba uliosainiwa baina ya serikali na kampuni ya Willcroft.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nashindwa kumwelewa Ngeleja... seemu moja anasema hisa zimeuzwa bila serikali kujulishwa... sehemu nyingine anasema walijadiliana kuhusiana na matatizo ya kifedha ya WDL na Willcroft ikasema inauza hisa zake kwa kampuni nyingine. Sasa inakuwaje aseme sewrikali haina taarifa na kuuzwa kwa hisa hizo?
  Na kama Willcroft imeuzwa, kwa nini hiyo kampuni mpya isiwe na haki ya kumiliki hisa za Willcroft huko WDL?
   
 3. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hapa serikali inajichanganya kidogo. naona kama vile walijadiliana wote kuhusu kuuza
   
 4. Sabasaba

  Sabasaba Member

  #4
  Oct 3, 2008
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Hii habari nimeshindwa kuelewa kabisa!, Huyu waziri anachanganya fact za international business na local politics za CCM, i am total lost on his comments. je biashara ya hisa imefanyika bila wote kujadiliana kuhusu hisa?,

  jamani wanasheria hapo mnasemaje?, tuna wataalamu wa madini humu jamani?
   
 5. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ukila na kipofu usimshike mkono. hapa serikai yetu inaonekana kipofu na wanashtuka baada ya mauzo kupita
   
 6. m

  mgirima Member

  #6
  Oct 3, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya masuala yanahusu mambo ya Holding Companies, Minority Interests, Merger & Amalgamation etc. Ni mambo ambayo ni magumu na yanahitaji wanasheria waliobobea kwenye sheria za merger and the like. Majibu ya kijuu juu aliyoyatoa Ngeleja hayajibu hoja kuwa mgodi wa Mwadui haujauzwa.

  Tukumbuke 2010 haiko mbali. Madudu mengi tu yataibuka!
   
Loading...