Serikali yalipa Sh5 bilioni wafanyakazi hewa 10,000 ndani ya miezi mitano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yalipa Sh5 bilioni wafanyakazi hewa 10,000 ndani ya miezi mitano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Jun 10, 2012.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Serikali yalipa Sh5 bilioni wafanyakazi hewa 10,000

  Serikali yalipa Sh5 bilioni wafanyakazi hewa 10,000


  SERIKALI imepoteza zaidi ya Sh5.4 bilioni kutokana na kulipa mishahara kwa wafanyakazi hewa 9,949 katika kipindi cha miezi mitano iliyopita.Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema vitendo hivyo vimekwamisha utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo ambayo ingegharamiwa kwa fedha hizo.

  Kauli ya Dk Mgimwa imekuja ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu Rais Jakaya Kikwete alipotoa agizo la kudhibiti wafanyakazi hewa katika wizara na idara za Serikali.

  Machi mwaka jana, Rais Kikwete aliamuru kufanyika kwa ukaguzi katika idara zote za serikali kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba kiasi cha Sh9 bilioni kilikuwa kimelipwa kama mishahara kwa wafanyakazi hewa katika wizara tatu tu za Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katiba na Sheria na Afya na Ustawi wa Jamii.
  Rais alisema wahusika wa vitendo hivyo walipaswa kubainishwa ikiwa ni hatua ya kukomesha mara moja wizi wa fedha za umma kupitia mishahara hewa na kwamba Serikali haipaswi kuwaruhusu watu ambao wameiibia Serikali fedha kuendelea kufanya kazi za umma.

  Lakini jana akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha lililofanyika Dar es Salaam, Dk Ngimwa alikiri kuwapo kwa tatizo hilo, mwaka mmoja tangu kutolewa kwa agizo hilo la Rais Kikwete.
  Kutokana na hali hiyo, alisema Serikali imechukua hatua za kukabiliana na ufisadi huo kwa kuweka utaratibu wa orodha ya wafanyakazi kupitiwa kila mwezi.Aliwataka wafanyakazi wenye tabia hiyo kuiacha mara moja akisema Serikali iko makini na itawachukulia hatua kali wahusika wote.

  Alisema wiki ijayo itasomwa Bajeti ya Serikali 2012/13 ambayo imezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na imelenga ukuaji wa uchumi wa kiwango cha kati, hivyo suala la udhibiti wa mapato ya Serikali halitakuwa na mjadala.

  “Tunataka kuleta hali bora ya maisha ya wananchi. Lengo la Serikali ni kila mmoja kupata wastani wa pato la Dola za Marekani 3,000 (Sh3.8 milioni) kila mwezi ifikapo mwaka 2025,” alisema.
  Alisema bila udhibiti wa tatizo la mishahara ya wafanyakazi hewa, ni vigumu kufikia lengo hilo hivyo kuwataka wafanyakazi wa wizara hiyo kujipanga vizuri ili lengo hilo lifikiwe.

  Alisema wafanyakazi wa Hazina ndiyo wanaobeba jukumu hilo wakati Serikali inajitahidi kupambana na mtikisiko wa kiuchumi hususan kipindi hiki cha kuelekea bajeti.Alisema Serikali imeomba nguvu ya kujiongezea uwezo kutoka mashirika ya kimataifa, nchi za Mashariki ya Kati na Asia.

  Awali, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Ramadhan Khijjah alisema kuna tatizo la wafanyakazi wa wizara hiyo kuogopa kuzungumza katika vikao vya baraza hilo.

  “Watu waoga huogopa kuzungumza. Wanawahofia wakuu wao wa idara jambo ambalo halijengi,” alisema.
  Alisema hali hiyo inachangiwa na walio wengi kuogopa kuchukiwa na mabosi wao jambo ambalo alilipinga na kuwatoa hofu akiwataka wawe wazi.

  Alisema mabaraza hayo ndiyo sehemu ya kukosoa, kuelekeza na kubainisha kasoro zilizopo ili hatua zichukuliwe na kujenga mshikamano kwa manufaa ya Taifa na jamii kwa ujumla.  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  KIla ofisi kuna daftari za mahudhurio ambayo hubainisha nani anafanya kazi na nani hafanyi kazi. Mahudhuria hayo pia hubainisha watoro kazini, na idadi ambazo wafanyakazi wamehudhuria kazini mwao. Kila mwezi kabla ya mishahara kutolewa taarifa hazo kwa kawaida humfikia afisa utumishi na kisha kuziweka wazi kwa mhazini.

  Hizo takwimu za mahdhurio na utendaji wa watumishi wa umma ni mtindo wa kuzoeleka tu kuwepo ofisini au unafanyiwa kazi. Na kama utaratibu huo unafanyiwa kazi iweje kutokee malipo ya watumishi hewa? Kama kosa linatokea mwezi mmoja katu haliwezi kuendelea kwa mwezi mwingine kwa vile takwimu zingeonyesha dhahiri nani yuko kazini na nani hayuko kazini. Siku hizi kuna database nashangaa kama hilo linatokea.
   
 3. N

  Njaare JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii haiwezi kwisha maana wanaotumwa kwenda kuhakiki wafanyakazi ndo waliochomeka majina ya wafanyakazi hewa au wanashirikiana na waliochomeka.
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Amefanyaje kazi za mbunge kabla hajaapa kuwa mbunge? naamini hili litazua sarakasi bungeni, mtaona mimacho itakavyowatoka lukuvi, wasira, mwanasheria mkuu, nnkuchika . . . . wakijaribu kuweka mambo sawa bila mafanikio! chadema itawadhihirishia watz jinsi ccm isivyotii sheria na katiba.
   
Loading...