Serikali yaliomba radhi Kanisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yaliomba radhi Kanisa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchonga, Jan 4, 2011.

 1. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mussa Mwangoka, Sumbawanga
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameliangukia Kanisa Katoliki nchini, akiomba radhi kutokana kashfa zilizotolewa kwa kanisa hilo wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

  Pinda aliomba radhi jana mbele ya viongoizi wa madhehebu mbalimbali ya dini kwa niaba ya Serikali na CCM, wakati ambao baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki katika Jimbo la Sumbawanga mkoani Rukwa wametengwa kwa tuhuma kwamba 'walilinajisi' Kanisa katika kusherehekea ushindi wa kisiasa.

  Mbali na viongozi wa dini, kikao hicho kilichofanyika jana asubuhi katika Ukumbi wa Libori, pia kiliwashirikisha baadhi ya wazee maarufu wa mjini Sumbawanga.

  Wengi waliotengwa na Kanisa hilo wanadaiwa kuwa wanachama wa CCM waliokuwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi na tuhuma zinazowakabili ni kutoa kauli zilizokinzana na imani za dini zao wakati wa kampeini na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31 mwaka jana.

  Katika kikao hicho, Pinda alisema Uchaguzi Mkuu uliopita hakuwa rahisi kama ilivyodhaniwa, na badala yake ulikuwa na changamoto nyingi ikiwemo tofauti za kimtizamo na kiimani hivyo yasamehewe.

  "Hali hiyo siyo ilijitokeza tu Sumbawanga... najua tulimkwaza Mhashamu Baba Askofu (Damian Kyaruzi), tumekejeli imani ya dini yake, tunaomba radhi, mimi naomba radhi kwa niaba ya CCM na Serikali si hapa tu, lakini ni maeneo mengi nchini kama vile majimbo ya uchaguzi ya Hai na Same ambapo baadhi ya wagombea katika kuomba kura ya ndiyo walilazimika kutumia baadhi ya maneno yanayotumika katika injili ya mateso" alisema Waziri Mkuu Pinda.

  Alisema kuwa kutokana hali hiyo iliyojitokeza chama na Serikali imepata fundisho ambapo katika chaguzi zijazo aliomba viongozi wa dini, Serikali na vyama vya siasa wakae pamoja na kuweka angalizo ili wagombea wajiepushe na kukejeli imani za dini za watu wengine na kuwasihi viongozi hao wa dini nchini nzima kuanza ukurasa mpya ambapo muda mwingi wanapaswa kuutumia kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo.

  Kufuatia radhi aliyoiomba Waziri Mkuu, Mwanachi liliwasiliana na uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga ambao ulisema kuwa "Suala la imani linabaki katika mchakato wa kanisa kwa maana ya watu na imani yao".

  "Mimi kwa bahati mbaya sikuhudhuria kikao hicho maana nilikuwa na kazi nyingine za kijimbo, lakini kama Waziri Mkuu ameomba radhi tunaipokea na inabaki kuwa radhi ya mtu aliyeomba," alisema Padre Modest Katonto ambaye ni Wakili wa Kiaskofu katika Jimbo la Sumbawanga na kuongeza:
  "Suala la toba linawahusu waumini wenyewe, ni suala la muumini na kanisa lake na ni suala la muumini na Mungu wake, hivyo taratibu za kikanisa kwa wale waliotengwa zinafahamika, hakuna kinachoweza kufanywa nje ya taratibu hizo".
  Padre Katonto alisema taratibu za kanisa hilo zinamtaka muumini aone kosa lake na kuamua kutubu mwenyewe na kwamba taratibu hizo hazitoa fursa ya mtu kutubu kwa niaba ya mwingine.

  Kutokana na msimamo huo ni dhahiri kwamba waumini 27 walitengwa na Kanisa hilo na wengine zaidi ya 400 waliwekewa pingamizi kwa mujibu wa sheria namba 1364 ya Kanisa Katoliki, wataendelea na adhabu zao hadi hapo watakapotimiza matakwa ya sheria za kanisa hilo.

  Awali habari za kutengwa kwa waumini hao zilihusishwa sana na purukushani za Uchaguzi Mkuu na ilidaiwa kuwa walitengwa na Kanisa kutokana na kujihusisha na chama tawala cha CCM, lakini Mwananchi ilifanya utafiti na kubaini kuwa waliofungiwa wengi wamegundua kosa lao na sasa wanalijutia.

  Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Sumbawanga mkoani Rukwa umebaini kuwepo kwa vitendo vya kukashifu imani ya Kikristo vilivyofanywa na baadhi ya waumini hao wakati wa kampeni na baada ya kutangazwa kwa matokeo ya ambapo waumini hao walitengeneza jeneza na ndani yake wakaweka mgomba na sanamu ya kanisa na msalaba wake na baadaye kulizika jeneza hilo.

  Tukio hilo lilifanyika katika kijiji cha Chelenganya kilicho umbali unaokadiriwa kuwa ni zaidi ya kilometa 20 kutoka yalipo makao makuu ya Manispaa ya Sumbawanga.
  Lakini waumini hao sasa wanajutia kitendo chao na wengi wanajitetea kuwa walifanya hivyo bila kujua kuwa walikuwa wakifanya kosa kubwa kwa kanisa lao; walifikiri wapo kwenye shamra shamra za kusherehekea ushindi wa mgombea wao.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Pinda alizungumzia Suala la rushwa na kukiri kushamiri kwa vitendo hivyo katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

  Alisema kutokana na hali hiyo,ipo haja ya kuangalia upya mfumo wa uchaguzi kuanzia ndani ya CCM ambayo inajiandaa kwa uchaguzi wa viongozi wake mapema mwakani hivyo kuhakikisha hautatoa mianya ya rushwa na kwamba viongozi wa madhehebu ya dini na wazee hawana budi kukemea kwa nguvu zote vitendo vya rushwa.

  "Rushwa ni rushwa tu hakuna haja ya kusema kuna rushwa ndogo hata mtu anapotaka kutimiza haja zake fulani kwa kutoa kitu kidogo badi ni rushwa..... pia kwa mgombea anapotoa doti ya khanga ili apigiwe kura hilo ni tatizo hivyo naiomba CCM ibadilike, najua ni jambo gumu, lakini lazima tupigane nalo kikamilifu.... wagombea nao tabu tu hasa kwenye chama safari hii tujirekebishe ," alisema Pinda.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo Tanzania mkoa wa Rukwa, Mchungaji Israel Moshi alisema madhebu ya dini yamesamehe na viongozi wanapaswa kusamehewa kwani nao ni binadamu.

  source: Pinda aliangukia Kanisa Katoliki
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mbona ufisadi na wizi wa mali zetu hawaombi msamaha? wanayo dharau sana watu hawa!
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Gazeti la habari leo lilichochea suala hili na kulifanya lionekane ni ugomvi wa mgombea mwilamu na kanisa katoliki kwa upande mmoja na upande wa pili uvutano kati ya kanisa na CCM. wengi tulipinga kwamba kuna jambo si jema walilofanya waumini wa kanisa hilo.

  Kitendo cha waziri mkuu kuomba radhi kinaonyesha kwamba kulikuwa na kuongeza chumvi katika habari ya mwandishi huyo na kwa malengo yake ambayo ni hatari kwa nchi yetu
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Huo ndiyo uungwana.
   
Loading...