Serikali yaleta wataalamu kutoka China kudhibiti mitandao ya kijamii kama YouTube, Facebook

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Serikali ya Tanzania imelata wataalamu kutoka China kuisaidia kudhibiti mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Youtube, WhatsApp na nyingine kama ambavyo China imeweza kuidhibiti mitandao hii nchini mwao, ambapo haipatikani nchini China bali mitandao ya kijamii ya kichina.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani alivyokuwa akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, wadau wa mitandao na wataalamu kutoka China.

Amesema japo sisi hatuwezi kuwa na mitandao yetu ya kijamii na tunatumia mitandao ya kijamii ya Marekani ila wataangalia namna ya kufanya ili mtu anayeandika kwenye mtandao awajibike na anachokiandika maana mitando hii imekuwa ikitumika kuharibu nchi kama ilivyotokea kwenye nchi za Kiarabu

Je, mitandao hii wataidhibitije?

 
Back
Top Bottom