Serikali yalaumiwa kwa ubaguzi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,073
1,250
SERIKALI imetupiwa lawama kuwa inawabagua katika ajira wahitimu wa kozi mbalimbali wanaofaulu vizuri kwenye vyuo binafsi hapa nchini na kuwapendelea wahitimu wanaotoka vyuo vya umma.
Lawama hizo zilitolewa na wahitimu wa Chuo cha Kimataifa cha Shukrani kilichoko mjini Mbeya, wakati wa mahafali ya 14 ya chuo hicho kinachotoa kozi mbalimbali za uhazili, utawala na uongozi, biashara na uchumi.

Wahitimu hao kupitia risala yao iliyosomwa na Christa Mwenda, waliiomba serikali kutowabagua wasomi katika utoaji wa ajira kwa vigezo vya kusoma kwenye vyuo vya umma badala yake utizamwe uwezo wa ufaulu.

Kwa mujibu wa risala hiyo, wanafunzi wanaosoma vyuo binafsi hususan chuo chao hawaajiriwi serikalini kwa madai kuwa chuo hicho hakitambuliwi licha ya kusajiliwa na NACTE.

“Mgeni rasmi, tunaomba kilio chetu ukifikishe kwa wahusika, tumekuwa na wakati mgumu wa kupata ajira serikalini kutokana na chuo chetu kutotambuliwa serikalini… tunashauri kigezo cha mwanafunzi kuajiriwa kiwe kiwango chake cha kufaulu na ubora wa mafunzo aliyoyapata; kigezo kisiwe chuo alichosoma huo ni ubaguzi wa ajira,” alisema Mwenda.

Naye Mkuu wa Chuo hicho, Paulo Mdemu, alisema tangu kilipoanzishwa kimefanikiwa kutoa wataalamu wengi waliokuwa na soko katika sekta binafsi na wengine kujiajiri.

Mdemu, alisema vyuo binafsi vimechangia kwa kiasi kikubwa kukuza elimu na ujuzi katika fani mbalimbali na kuipunguzia mzigo serikali ya kuandaa watalaamu hao hivyo ni jukumu la serikali kuwa na mizania sawa ya utoaji wa ajira.

Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mbeya, Moses Chitama, aliyemwakilisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema ili kukubalika katika soko la ajira, chuo hicho kinatakiwa kutumia mitaala sawa na vyuo vingine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom