Serikali yakwama Mahakama Kuu

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
848
1,212
Siku ya leo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam chini ya Jaji Augustino Shangwa imetupilia mbali mapingamizi yote yaliyofunguliwa na Medical Council of Tanganyika kupitia Mawakili wa Serikali.

Ni kwamba mnamo Mwezi Aprili 2013 Medical Council ilinifutia usajili wangu na hivyo kutokuruhusiwa kujihusisha na kazi za kutibu.

Kutokana na maamuzi hayo mnamo Julai 2013 kupitia kwa Prof Abdalah Safari tulikata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu hiyo. Siku chache baadae Mawakili wa Serikali waliweka pingamizi kwa hoja kuwa rufaa yetu ilikosa vigezo vya kisheria.

Kupitia maamuzi ya leo Mahakama imepanga kuwa kesi ya msingi kuanza kusikilizwa tarehe 10 Februari. Nawasiliaha. Dr. Godbless. C.M
 
Angalia wale uliokuwa unawatetea leo hii wapo wapi? Naona kama wamekuacha peke yako ukipambana na kesi ilihali ulikuwa na kundi kubwa likikusapoti. Usikate tamaa hii ndiyo Tanzania WANAFIKI KIBAO.
 
Angalia wale uliokuwa unawatetea leo hii wapo wapi? Naona kama wamekuacha peke yako ukipambana na kesi ilihali ulikuwa na kundi kubwa likikusapoti. Usikate tamaa hii ndiyo Tanzania WANAFIKI KIBAO.

Mkuu hajaachwa peke yake hata gharama za kufuatilia kesi pamoja na wakili zimesaidia kuchangiwa na madaktari wenzake. Hata Dr.Godbless ataweza kuthibitisha hili. Sio uungwana kumwachia peke yake jambo lililopo mbele yetu. Hakuwa anapigania maslahi binafsi.
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli kabisa fedha zote kwa ajili ya kugharamia kesi zimetokana na michango ya madaktari. Nadhani hii ndio ilikuwa hatua muhimu sana.
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kabisa fedha zote kwa ajili ya kugharamia kesi zimetokana na michango ya madaktari. Nadhani hii ndio ilikuwa hatua muhimu sana.

Utarudishwa tu daktari, Serikali bado inakutaka sana na nijuavyo hiyo ilikuwa ni namna tu ya kukupooza yaani umewekewa speed humps.
 
I remember you Godbless Charles...the brother of me at Tabora School....
 
Kamanda pole,mambo yataenda fresh..nakuaminia ila ULIMBOKA kawaangusha watanzania.
 
Back
Top Bottom