Ni wangapi wanaweza kuthibitisha hizi takwimu?
Prof ndulu jua kua watz tunashida sana na maisha yetu yapo hatarini san,kwa ivyo punguza utani acha kuzidi kuaminisha watu kua mnawaibia mpendavyo
Blaah Blaah tuNA Tausi Mbowe | Mwananchi - Sept 01, 2012
TANZANIA imeweza kukusanya mapato yaliyozidi matumizi kwa zaidi ya asilimia tatu kwa mara ya kwanza tangu mtikisiko wa uchumi uikumbe dunia.
Akizungumza katika ufunguzi wa Mfumo wa Dhamana ya Serikali kwa njia ya mtandao, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu alisema kuwa hadi kufikia Juni 30 mwaka huu, Serikali kupitia vyanzo mbalimbali imeweza kukusanya mapato ya zaidi ya Sh7.2 tirioni.
Gavana Ndullu alisema pamoja na makusanyo hayo makubwa Serikali imeweza kutumia Sh6.9 tirioni pekee kama matumizi yake ya kawaida tofauti na miaka iliyopita ambapo matumizi yalikuwa makubwa ukilinganisha na mapato yaliyopatikana.
"Hii ni mara ya kwanza kwa miaka mitatu mfululizo tangu msukosuko wa uchumi utokee, Serikali ilikuwa hafikii lengo la makusanyo na matumizi, mara zote mapato yalikuwa madogo ukilinganisha na matumizi. Serikali ilikuwa ikitumia zaidi ya mapato inayoyapata lakini sasa imeweza kutumia kidogo ukilinganisha na mapato yaliyopatikana," alisema Profesa Ndullu.
Alisema kwa sasa Serikali imeweza kugharamia matumizi yake ya kawaida lakini pia imeweza kuchangia bajeti yake yenyewe.
Akizungumia mfumuko wa bei, Profesa Ndulu alisema, kasi ya ongezeko la bei imeanza kuteremka na kufikia asilimia 15.7 kutoka 19.8 za awali.
Alisema ni matarajio ya Serikali kuwa kasi hiyo itazidi kuteremka kutokana na viashiria vingi kuonyesha wazi bei za bidhaa mbalimbali zinashuka ikiwemo bei ya mafuta.
Kwa upande wa thamani ya shilingi, Professa Ndulu alisema, kuanzia Januari mpaka sasa thamani ya shilingi imekaa katika sehemu nzuri ambapo kwa sasa Dola ya Marekani inanunuliwa kati ya Sh1,575 mpaka 1,590.
"Kwa kipindi kirefu pesa yetu ilishuka na kufikia Sh1,825 lakini tangu kuanza kwa mwaka huu imeweza kupanda na kubaki hapo hapo," alisisitiza Ndullu.
Kuhusu mfumo huo mpya, Ndullu alisema, utasaidia kufanya mnada na hati fungani za Serikali kwa kutumia mtandao wa kompyuta ambapo kila mshiriki ataweza kutumia mtandao huo pale alipo na kuileza BoT na taarifa hizo zitafika.
Alisema Tanzania ni nchi ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki kuwa na mfumo huo ambapo tayari wadau mbalimbali wataruhusiwa kushiriki ikiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo kwa sasa si lazima wapitie katika mabenki au wakala.
Alisema mfumo huo umekamilishwa na Watanzania wenyewe wakiwemo wataalam kutoka BoT hivyo kuokoa fedha za walipa kodi ambazo zingetumika kununua kutoka nje ya nchi.