Serikali yakusanya mapato zaidi ya matumizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yakusanya mapato zaidi ya matumizi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kupelwa, Sep 1, 2012.

 1. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  NA Tausi Mbowe | Mwananchi - Sept 01, 2012

  TANZANIA imeweza kukusanya mapato yaliyozidi matumizi kwa zaidi ya asilimia tatu kwa mara ya kwanza tangu mtikisiko wa uchumi uikumbe dunia.

  Akizungumza katika ufunguzi wa Mfumo wa Dhamana ya Serikali kwa njia ya mtandao, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu alisema kuwa hadi kufikia Juni 30 mwaka huu, Serikali kupitia vyanzo mbalimbali imeweza kukusanya mapato ya zaidi ya Sh7.2 tirioni.

  Gavana Ndullu alisema pamoja na makusanyo hayo makubwa Serikali imeweza kutumia Sh6.9 tirioni pekee kama matumizi yake ya kawaida tofauti na miaka iliyopita ambapo matumizi yalikuwa makubwa ukilinganisha na mapato yaliyopatikana.

  "Hii ni mara ya kwanza kwa miaka mitatu mfululizo tangu msukosuko wa uchumi utokee, Serikali ilikuwa hafikii lengo la makusanyo na matumizi, mara zote mapato yalikuwa madogo ukilinganisha na matumizi. Serikali ilikuwa ikitumia zaidi ya mapato inayoyapata lakini sasa imeweza kutumia kidogo ukilinganisha na mapato yaliyopatikana," alisema Profesa Ndullu.

  Alisema kwa sasa Serikali imeweza kugharamia matumizi yake ya kawaida lakini pia imeweza kuchangia bajeti yake yenyewe.

  Akizungumia mfumuko wa bei, Profesa Ndulu alisema, kasi ya ongezeko la bei imeanza kuteremka na kufikia asilimia 15.7 kutoka 19.8 za awali.

  Alisema ni matarajio ya Serikali kuwa kasi hiyo itazidi kuteremka kutokana na viashiria vingi kuonyesha wazi bei za bidhaa mbalimbali zinashuka ikiwemo bei ya mafuta.

  Kwa upande wa thamani ya shilingi, Professa Ndulu alisema, kuanzia Januari mpaka sasa thamani ya shilingi imekaa katika sehemu nzuri ambapo kwa sasa Dola ya Marekani inanunuliwa kati ya Sh1,575 mpaka 1,590.

  "Kwa kipindi kirefu pesa yetu ilishuka na kufikia Sh1,825 lakini tangu kuanza kwa mwaka huu imeweza kupanda na kubaki hapo hapo," alisisitiza Ndullu.

  Kuhusu mfumo huo mpya, Ndullu alisema, utasaidia kufanya mnada na hati fungani za Serikali kwa kutumia mtandao wa kompyuta ambapo kila mshiriki ataweza kutumia mtandao huo pale alipo na kuileza BoT na taarifa hizo zitafika.

  Alisema Tanzania ni nchi ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki kuwa na mfumo huo ambapo tayari wadau mbalimbali wataruhusiwa kushiriki ikiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo kwa sasa si lazima wapitie katika mabenki au wakala.

  Alisema mfumo huo umekamilishwa na Watanzania wenyewe wakiwemo wataalam kutoka BoT hivyo kuokoa fedha za walipa kodi ambazo zingetumika kununua kutoka nje ya nchi.
   
 2. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Siamini takwimu za ki hivyo kbs mwaka jana TRA walivuka lengo la makusanyo,na hali ndiyo ikazidi kuwa jiwe, leo tena wamekuja na songi lilelile, waambie bado uongo ule wa last year unanuka vilivyo.
   
 3. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Nitaamini hilo siku nikisikia walimu na madaktari hawana madai kwa serikali....vyenginevyo. huu ni ush.uzi wa kobe.
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Kumbe amesema Ndulu! Takwimu za makaratasi na kwenye makabati.
   
 5. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Uwongo mtupu, mzee anajidhalilisha na taaluma yake...

  Budget inaeleza wazi kila mtu aliona bungeni jinsi ilivyo kiduchu... Hata spika alivyosaidia kupitisha haraharaka budget mbovu haina kiwango cha kuinuwa uchumi Tz, hata rais kathibitisha hana pesa ya kuongeza mshahara kwa watumishi
   
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  sasa fikirieni mapato hili taifa linaloingiza na hapo bado TRA,TPA na wezi wengine bado wanatuibia...fikirieni kila kodi inayotakiwa kulipwa ingekua inalipwa leo hii tusingekua tunahitaji pesa za wafadhili kutoka nje..na hapo bado gesi na mafuta hayajaanza kazi..TANZANIA ni nchi tajiri sana ni vile tu tuna viongozi wezi na wabovu lasivyo tungekua mbali sana
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Yako wapi hayo makusanyo sasa?
   
 8. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kama wanakusanya zaidi ya makadirio KWANINI fedha inayopelekwa kwenye wizara zetu pamoja na Halmashauri ni kidogo? Fedha nyingine inakwenda wapi? au labda ndo mambo ya Uswisi au maandalizi ya 2015. Wahusika tunaomba majibu.
   
 9. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni wangapi wanaweza kuthibitisha hizi takwimu?
   
 10. a

  alfazulu JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 735
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SASA MBONA CT SCAN MUHIMBILI HAINUNULIWI, AHAAAAAAAAAAAAAAAAAA, NDO UMESEMA MNABANA MATUMIZI EH!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!duh............
   
 11. M

  Maseto JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 721
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Kweli kwa pamoja tumpe pole pr. Ndulu kwa kutoa takwimu za uwöngo.kwa mfano,ktk halmashauri pesa ya matumizi ya utawala haikutolewa kabisa.pesa hii huitwa fidia ya vyanzo vya kodi vilivyofutwa.na ruzuku kwa ujumla kwenye halmashauri ilitolewa chini ya 40%.ni ajabu anaposema makusanyo yalizidi matumiz
   
 12. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  sasa watupe sababu nyingine ya kuwa na madeni kwa walimu, polisi kuwa na magari yasiyo na mafuta, hospitali kukos adawa muhimue etc.
   
 13. K

  Kuchayaa Senior Member

  #13
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  usanii wa mchanamchana huo.kama kweli serikali imekusanya mapato zaidi ya matumizi hiyo pesa wanaipeleka wapi?mbona kuna wadogo wetu ambao wako vyuo vikuu bodi ya mikopo imeshindwa hata kuwapa fedha kwaajili ya kujikimu kipindi cha field imewaambia wajitegemee, serikali inapeleka wapi hiyo ziada ya mapoto?
   
 14. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Ben Ndulu na timu yake ya mafisadi. Wao wamekaa kuwakumbatia Barclays na benki za kifisadi kutoka nje wakati nchi zilizoendelea zinawafikisha mahakamani kwa wizi wa wazi wazi. When will this governor take decisive measures to curb proliferate of these banks in Tanzania?
   
 15. a

  afwe JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Wasanii tu hawa!
   
 16. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  we're getting tired to here same song every day, we want to see our East African former employees getting their retirement money. We wannna see Our Teachers receive their long time pay back salaries.
  Prof Ndulu is another "Weapon of mass distruction" He says what JK wants to hear, to keep his bread
   
 17. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Mbona hizi takwimu hazikutolewa wakati bunge la budget linaendelea limetolewa baada ya bunge kuisha.

  Mbona bunge liliambiwa ni kiasi cha 46% ya fedha za budget tu ndio zilizotumiwa Mwaka wa fedha 2011/12, je Ndulu anataka kutuaminisha kitu gani?????
   
 18. m

  mwabakuki JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kamw hii ni kweli sasa inakuwaje kila wizara na kila halmashauri inalalamika kwamba hazikupata pesa zilizobajetiwa kwa mwaka wa fedha ulioishia June 30; 2012. takwimu za bunge zinaonesha kwa kadri ya majadiliano ya bunge la bajeti lillloisha kuwa Halmashauri nyingi sana nchini zilipata pesa chini ya asilimia 50% ya bajeti zao kwa mwaka huu...hali hiyo ilijitokeza tena ktk wizara zote isipokuw labda ofisi ya mkuu wa kaya.....sasa haya anayotueleza Beno Ndulu ni kitu gani hiki...inawezekanaje serikali ikakusanya mapato yanayozidi matumizi iliyoyapanga huku taasisi zikilia kuwa hazina pesa....seriously outrageous...Lakini hii ndiyo Tanzanja..
   
 19. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  As Walter Mondale said (when he was running against Ronald Reagan)! "There are cook books and cooked books"! Ndulu's books seem to have been in the kitchen a long time!

  Iweje Mkuu wa Kaya aseme hatuna fedha za kutosha kuwalipa zaidi madaktari na Gavana wake atangaze tuna fedha shilingi bilioni 300 za ziada?

  Kama ni kweli kuna ziada, basi tunaomba Ndulu achunge isiibiwe na kupelekwa tena Uswizi. Maana alikuwa Makamu wa Gavana wakati wa wizi wa EPA.
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Inaonesha huelewi tofauti ya kuvuka lengo la makusanyo na kutumia chini ya makusanyo. Unaweza kuvuka lengo la makusanyo lakini matumizi yako yakawa makubwa kuliko makusanyo lakini kwa sasa wanaweza kuwa wamevuka malengo ya makusanyo na matumizi yakawa chini ya makusanyo, na pia inawezekana kuwa hawajavuka malengo ya makusanyo lakini matumizi yakawa chini ya makusanyo. Funguka kidogo.
   
Loading...