Serikali yakiri udhaifu wa polisi kazini

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
SERIKALI imekiri wazi kuwa, Jeshi la Polisi nchini linakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa makazi bora jambo ambalo limesababisha kushuka utendaji kazi, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwingulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alipokua akizungumza na maofisa wakaguzi wa Jeshi la Polisi pamoja na askari wa vyeo mbalimbali katika Mkoa wa Dodoma.

Amesema, tatizo la makazi kwa askali wa Jeshi la Polisi ni changamoto kubwa inayotakiwa kutatuliwa kwa haraka ili kuwafanya askari kuwa na moyo wa kufanya kazi ya kulinda raia na mali zao kwa kuzuia uhalifu.

“Tutahakikisha tunatengeneza makazi rafiki wa askali wetu ili waweze kuchapa kazi kwa kwa ufanisi zaidi na kupambana na wahalifu wa aina yoyote, ”amesema Nchemba.

Amesema, kutokana na tatizo hilo serikali itatumia njia mbadala ya kuhakikisha linatatua tatizo la makazi kwa jeshi la polisi kama sio kulimaliza kabisa .

Aidha ametoa rai kwa askali hao kuzingatia miiko yao ya kazi na wanapofanya kazi kama walivyofundishwa vyuoni na kuapa pindi walipoingia kazini.

“Endapo mtazingatia miiko ya kazi yenu haitatokea siku ambayo nitakuwa na mashaka na utendaji kazi wa jeshi la polisi.

“Muhakikishe mnatenda haki kwa kila mtu na msiwe na tabia ya kuwakandamizi wanyonge kama baadhi ya askali wengine wanavyofanya,nyie mnatakiwa kuhakisha mnawatetea wanyonge kuweza kupata haki zao za msingi,”amesema Nchemba.

Pia amewataka kutumia nguvu kubwa katika kuhakisha wanalinda usalama wa nchi na raia ili kuwafanya wananchi kuwa na imani na jeshi la polisi.

Hata hivyo amesema serikali ya amwamu ya tano inamikakati ya kuboresha maslahi ya askali wote .

Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma amesema, hana shaka na askali wake kwani wanachapa kazi usiku na mchana kwa kuzingatia maagizo kutoka makao makuu na anyotoa yeye.

“ Tunafanya kazi kwa weredi kuhakikisha nchi inakuwa shwari kupitia wizara ya mambo ya ndani ya nchi,” amesema kamanda Mambosasa.
 
Serikali gani ilikuwa haitaki kuboresha masilahi ya hao asikari? Hiv bado tu mna mawazo ya uongo uongo tu!
 
kwani si wanalipwa mshahara kama wengine wanaofanya serikalini, nao wakapange tu,
 
kwani si wanalipwa mshahara kama wengine wanaofanya serikalini, nao wakapange tu,[/QUOT
UNAJUA FALSAFA YA ASKARI KUKAA KAMBINI?? AU UMETOA MAWAZO YAKO BILA KUJUA UMUHIMU WA FALSAFA YA ASKARI KUKAA KAMBINI AU KATIKA KOTA???
 
Askari kukaa KAMBINI au KUKAA KOTA n FALSAFA MUHIMU SANA KATIKA UTENDAJI WA MAJUKUMU YAO NA "NATURE" ya KAZI yao, tusiwe na USHABIKI KATIKA MASWALA YA ULINZI WA TAIFA LETU,, ASKARI HAWALALI,ASKARI WANATULINDA USIKU NA MCHANA, JUA NA MVUA VYOTE VYAO,, tunahitaji BUSARA YA MAWAZO tunapojadili issue ya Askari wetu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom