Serikali yakiri matumizi mabaya ya fedha zake

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Serikali yakiri matumizi mabaya ya fedha zake




Posted Decemba7 2013




Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Fedha Janeth Mbene, alipokuwa akijibu maswali ya nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu Ritha Kabati ,(CCM) na Hamad Rashid Mohamed (Wawi- CUF).

Serikali imekiri kuwa na nidhamu ‘mbovu' katika matumizi ya fedha, jambo linaloyumbisha bajeti zake mara kwa mara.


Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Fedha Janeth Mbene, alipokuwa akijibu maswali ya nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu Ritha Kabati ,(CCM) na Hamad Rashid Mohamed (Wawi- CUF).


"Ni kweli kama nilivyotangulia kusema hapo awali kuwa pamoja na mambo mengine, nidhamu ya matumizi yetu katika fedha ni mbovu, hivyo tunatakiwa kurekebisha pamoja na hali hiyo," alisema.


Katika swali la nyongeza Kabati alitaka kujua ni kwa nini Serikali isifikirie kuwa na mfumo wa ‘Capital Budget' badala ya Cash Budget kama ilivyo sasa.


Hamad alihoji matumizi mabaya ya Serikali na kutumia kiasi ambacho hakipo kwenye bajeti akitaka kujua inasemaje kwani limekuwa ni tatizo sugu.


"Angalieni mfano mzuri tu ni katika bajeti safari za nje. Serikali ilipanga kutumia Sh25 bilioni, lakini hadi leo zimeshatumika zaidi ya Sh28 bilioni. Serikali inatuambia nini ," alihoji Hamad.


Katika swali la msingi Neema Hamid (Viti Maalumu-CCM) alitaka kujua ni kwa nini fedha zinazopitishwa katika Bajeti ya Serikali hazipelekwi kwa wakati na kusababisha matatizo makubwa kwa wananchi.


Naibu Waziri alisema Serikali haiwezi kutumia mfumo wa Capital Budget kutokana na ukweli kuwa bado Serikali ya Tanzania ni tegemezi katika bajeti yake.


Alisema tatizo la kutoa fedha pungufu na kuondoa malalamiko litakwisha pale Serikali itakapoweza kutimiza malengo yake.

source:Mwananchi news paper

MY NOTE: MBONA HIKI NI KILIO CHA MIAKA YOTE NA MAJIBU NI HAYA HAYA? YAANI TUBAKI NA KUKUBALI MAJIBU HAYA KILA SIKU HUKU TUKISIKIA NA MAJIBU YA "PESA ZIKIPATIKANA" KILA MWAKA.
 
Back
Top Bottom