Serikali yakiri kuwepo kwa dawa ya kuongeza nguvu za kiume ambayo haina kemikali

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Serikali imekiri kuwepo kwa dawa ya kuongeza nguvu za kiume ambayo haina kemikali, lakini ikasema haijatangazwa rasmi.

Kauli hiyo imetolewa leo, bungeni, Aprili 29,2019 na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Ulanga (CCM), Godluck Mlinga.

Katika swali la nyongeza, mbunge huyo alitaja orodha ndefu za dawa za kuongeza nguvu za kiume kisha akahoji kama zina madhara kwa watumiaji.

Awali, mbunge wa viti maalumu (Chadema), Suzan Lyimo alihoji kama kuna madhara kwa wanaume wanaoongeza maumbile yao pindi wafanyapo mapenzi.

Akijibu, Dk Mwinyi amesema sababu za watu kupungukiwa nguvu za kiume ziko nyingi ikiwemo ugonjwa wa kisukari na msongo wa mawazo, lakini akasema Serikali ilishabaini uwepo wa dawa kwa ajili ya wanaume ambazo hazina kemikali.

Hata hivyo, ameonya matumizi ya dawa ambazo hazijafanyiwa tafiti kuwa si salama kwa matumizi.

Kuhusu dawa za kuongeza maumbile ya uume, Dk Mwinyi amesema zipo taarifa nyingi za aina hiyo, lakini jambo jema ni kuongeza uelewa wa wananchi ili kutumia dawa zilizothibitishwa.

Chanzo: Mwananchi
 
,huyo analinda kila kitu ndoo mana ukikatwa huo mhogo polisi lazima waje. xo lzm auzungumzie ulinzi wake
 
Imekuwaje Waziri wa Ulinzi akazungumzia mambo ya Nguvu za kiume?
... Serikali ni moja; huyu Mh. alishawahi kuwa waziri wa afya nadhani; so ana uzoefu mkubwa wa haya mambo na pengine "nature" ya swali lilimshinda Ummy kulijibu so kamwomba Kaka yake mwenye uzoefu na wizara hiyo amsaidie au pengine anakaimu kama alivyodkeza member mmoja hapo juu. Kawaida sana hiyo.
 
Back
Top Bottom