Serikali yakiri kushtakiwa na makampuni ya Pangea Mineral Limited na Bulyanhulu Gold Mining

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Serikali imekiri Bungeni juu ya uwepo wa kesi hizo ambazo zote zilifunguliwa tarehe 03/07/2018 huko London katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara ambapo Waziri wa Sheria, Prof.Kabudi alikuwa akijibu maswali ya Zitto alietaka kujua tuna kesi gani kama nchi katika mahakama za kimataifa.

Prof.Kabudi amezitaja kesi hizo kuwa ni shauri Na:LCIA Arbitration UN 173686 na shauri na: UN 1736867 ambapo amesema serikali imeshawasilisha utetezi wake mahakamani.

Maswali yote ya Zitto kwa kirefu kuhusu kesi hizi na majibu ya waziri kwa maandishi utayapata kupitia ukurasa wa twitter wa Zitto Kabwe.

Chanzo:Akaunti ya twitter ya Zitto
 
Lissu aliwaambia tutashitakiwa Lumumba mapovu yakawatoka eti hakuna kitu kama hicho.
Sasa tatizo likwapi? Wacha tushtakiwe utata ukaishe kama kushinda tushinde kama wao washinde tujue moja
 
walimpiga risasi bure Mh Lissu, T. A.
Lissu alionya juu ya uwezekano wa kushtakiwa kwa kutoheshimu mikataba ambayo CCM wenyewe bila kulazimishwa wakiwa na akili timamu waliisaini..
Uingereza walishawahi kututukana kwamba tunaongozwa na MKOSA MAARIFA anayeongozwa na mihemko !
 
Ma trilioni tutakayodaiwa hapo c mchezo. Tulijifunga wenyewe kny mikataba mibovu, madini yetu wamechukua, na ma-trilioni tutawalipa kufidia usumbufu
 
Mwanzo walikuwa wanasema uchumi unapaa na Tanzania inaongoza kwa uchumi wake kupanda barani Afrika, juzi Dr Mpango amekiri wazi kuwa uchumi wa nchi unaporomoka.

Walikuwa wanakataa serikali haijashitakiwa kwenye mahakama ya usuluhishi ya kimataifa, leo Dr. Kabudi kasema ni kweli makampuni ya Pangea Mineral Limited na Bulyanhulu Gold Mining yameishitaki serikali.

Kwa trend hii kuna siku serikali itakuja kukiri wazi kuwa inawajua wasiojulikana, inajua waliko Ben na Azory, inawajua waliomteka MO nk.

Wakati ni mwalimu mzuri sana tega sikio.
 
Mwanzo walikuwa wanasema uchumi unapaa na Tanzania inaongoza kwa uchumi wake kupanda barani Afrika, juzi Dr Mpango amekiri uchumi wa nchi unaporomoka.

Walikuwa wanakataa serikali haijashitakiwa kwenye mahakama za usuluhishi za kimataifa, leo Dr. Kabudi kasema ni kweli makampuni ya Pangea Mineral Limited na Bulyanhulu Gold Mining yameishitaki serikali.

Kwa trend hii kuna siku serikali itakuja kukiri kuwa inawajua wasiojulikana, aliko Ben, na Azory, inawajua waliomteka MO nk. Tega sikio.
Sote tutanena lugha moja siku moja.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom