Serikali yakiri kuachana na madai ya Tsh. Trilioni 360 za Makinikia

Labda nikuulize jomba..una takwimu za madini tangu mwaka 1995 ambazo zimeibiwa na kufekishwa. Kwenye makinikia..labda tuanzie hapo. Halaf tuambie umesoma mpaka darasa la ngapi..hapo ndio utajua hujui
Elimu ya darasani hii hii ya kukaririshana?
Basi msiuwe watu kujiweka madarakani , hamwezi kuongoza nchi ondokeni msimwage damu na kutia watu vilema baadaye mkaifisidi nchi. Ondokeni tujenge nchi
Anzeni kwanza kujenga walau makao makuu ndio mje tuongee
 
Labda nikuulize jomba..una takwimu za madini tangu mwaka 1995 ambazo zimeibiwa na kufekishwa. Kwenye makinikia..labda tuanzie hapo. Halaf tuambie umesoma mpaka darasa la ngapi..hapo ndio utajua hujui
Do your homework...

Kuhusu Elimu yangu usiifutilie sana. Maana tayari ushajidhihirisha uzumbukuku wako.
 
Hizi si zilikuwa kishika uchumba tu??!
Mpina angemuuliza hilo swali Mwendazake na VP aliyekuwa Waziri wa Fedha na Waziri wa Madini na yule kamishna wa TRA aliyeondolewa ndio wanajua kwa nini hawakuzidai hizo pesa badala yake wakachukua bil.700 tuu..
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa ufafanuzi kuhusu wapi zipo shilingi trilioni 360 zilizopo kwenye mashauri ya madai 1,095.

Waziri Nchemba amesema, kuna jumla ya mashauri 400 katika mabaraza ya rufani za kodi (TRAT) yenye thamani ya shilingi trilioni 4.2 na dola za Marekani milioni 3.04 zinaendelea katika mabaraza hayo.

Hata hivyo Dkt. Nchemba amesema, serikali ilikubali kupokea shilingi bilioni 700 kutoka Barrick baada ya makubaliano baina ya timu ya serikali iliyoundwa na Rais wa serikali ya awamu ya tano Hayati Dkt. John Magufuli kufikia makubaliano ya pande zote na Barrick kuhusiana na madai ya shilingi trilioni 360.

Amesema baada ya makubaliano hayo ndipo ikaundwa kampuni ya Twiga ambayo inamiliki hisa asilimia 16 na Barrick inamiliki asilimia 84 ya kampuni hiyo.

Ufafanuzi huo wa waziri wa Fedha na Mipango unatokana na maswali ya Mbunge wa jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina aliyetaka kufahamu kwa nini serikali imekubali kulipwa shilingi bilioni 700 kutoka kampuni ya Barrick badala ya shilingi trilioni 360 za awali.

View attachment 2365511
WaTanzania tutamwamini vipi huyu Waziri? Ingekuwa enzi ya mwendaZake haya aneliyatamka ?! Hatuna kali zinatakiwa kwa haraka kuokia Taifa hili
 
Hata hivyo Dkt. Nchemba amesema, serikali ilikubali kupokea shilingi bilioni 700 kutoka Barrick baada ya makubaliano baina ya timu ya serikali iliyoundwa na Rais wa serikali ya awamu ya tano Hayati Dkt. John Magufuli kufikia makubaliano ya pande zote na Barrick kuhusiana na madai ya shilingi trilioni 360.
Kitu muhimu sana ni Watanzania have the right to information the basis ya kumsamehe mwizi wetu!.

Kama deni hilo ni bonafide genuine, serikali inapoamua kusamehe, it got to give reasons. Na baada ya hapo TRA watoe taarifa kuwa wamelifuta deni hilo.

Haya mambo akina sisi tuliyasema sana humu, kama mwanzo tulizuia makinikia kwasababu tulihisi tunaibiwa kwasababu hatujui kilichomo!.

Tukafanya uchunguzi tutathibitisha ni kweli tumeibiwa!. Tukapiga hesabu tulichoibiwa, baba mtu mbio kaja na ahadi wamekubali kila kitu na ili kuonyeshea nia njema wakahidi kishika uchumba cha Dila milioni 300!.

Mwisho wa mazungumzo tukasamehe deni lote, na kuruhusu makinikia yaondoke huku mpaka leo mpaka kesho, bado hatujui kilichomo!.

Kama tulizuia makinikia kwasababu tunaibiwa kwa kutojua kilichomo, tukathibitisha tunaibiwa!, Tumeruhusuje makinikia bila kujua kilichomo?, kwanini tulizuia?!

More explanation on this is needed.
P
 
Yaani hata wewe Mayala, uliamini zile hadithi? Ungekuwa na uelewa japo kidogo sana wa biashara ya madini, ungeelewa tangu mwanzo, hata bila ya kuambiwa na mtu yeyote, kuwa zile hadithi za sijui trillion 360, mara Noah 1 kwa kila mtanzania, zilikuwa maalum for the fools.

Mwenye akili ukiambiwa kuna mtu kakamatwa na mahindi ya wizi tani 1,000 akiwa ameyabeba kwenye bajaji, utajua ni hadithi. Huwezi hata kupoteza muda wako kuulizia yaliwekwa kwenye magunia mangapi.

Wakati wa hadithi za makinikia ndiyo nilitambua kuwa kumbe nchi yetu ina idadi kubwa ya wajinga kuliko nilivyokuwa nikifikiria awali. Maana hata pale ilipohitajika basic reasoning, haikuwepo, bahati mbaya zaidi hata wale wenye degree nao hawakuwa tofauti na wasioenda shule hata darasa moja.

Mtu anajiita engineer, alithubutu kusema kuwa ndani ya container kulikuwa na makinikia ambayo yana dhahabu 90!! Very stupid. Hivi huyu ina maana hajui hata gravity ya dhahabu? 90% dhahabu, imejaa kwenye container, anaelewa litakuwa na uzito wa tani ngapi? Litabebwa na gari gani? Maana hilo moja, uzito wake utakuwa karibia sawa na containers 9 za mchanga. Hata ukifanikiwa tu kulinyanyua, litafumuka na kuchanika. Lakini wajinga waliamini.

Habari ya makinikia, nadhani marehemu alitaka kwa haraka kujua nchi ina kiwango gani cha ujinga.
 
Hizi si zilikuwa kishika uchumba tu??!

..mimi nashauri wachangiaji wachukue calculators zao na kudadavua 300 milion ni sehemu gani ya 191 billion.

..tu assume barrick watalipa 300 million kila mwaka, je itawachukua miaka mingapi kumaliza deni la 191 billion?
 
Kina plopesa soro wanaasemaje? Lissu alishauri akapata shda kamazote leo ndipo wanashtuka!!
Waziri wafedha enzi hizo atufafanulie imekuaje tulidai Noah leo hata baskeli hatupati???
 
Mimi mtanzania wa kawaida mpaka leo sijaelewa kuwa tuliaminishwa kuwa tunawadai trillion 320 mwisho wa siku tukaambulia billion 700 na 16% .Enzi za mwenda zake ilikuwa haramu kujadili lakini leo hayupo tujulishane ukweli
Kimsingi kusimama nao mahakamani wangeishia kutushinda.

Katika kufanya Negotiation kuna kitu kinaitwa "rejecting constructively"! Hii ndio Magufuli alifanya, unawakataa kijanja lengo ni kuwarudisha mezani mkubaliane upya. Kwa hicho walichokuwa wamekubaliana ni aheri kuliko ujinga uliokuwa unafanyika mwanzoni.
 
Kitu muhimu sana ni Watanzania have the right to information the basis ya kumsamehe mwizi wetu!.

Kama deni hilo ni bonafide genuine, serikali inapoamua kusamehe, it got to give reasons. Na baada ya hapo TRA watoe taarifa kuwa wamelifuta deni hilo.

Haya mambo akina sisi tuliyasema sana humu, kama mwanzo tulizuia makinikia kwasababu tulihisi tunaibiwa kwasababu hatujui kilichomo!.

Tukafanya uchunguzi tutathibitisha ni kweli tumeibiwa!. Tukapiga hesabu tulichoibiwa, baba mtu mbio kaja na ahadi wamekubali kila kitu na ili kuonyeshea nia njema wakahidi kishika uchumba cha Dila milioni 300!.

Mwisho wa mazungumzo tukasamehe deni lote, na kuruhusu makinikia yaondoke huku mpaka leo mpaka kesho, bado hatujui kilichomo!.

Kama tulizuia makinikia kwasababu tunaibiwa kwa kutojua kilichomo, tukathibitisha tunaibiwa!, Tumeruhusuje makinikia bila kujua kilichomo?, kwanini tulizuia?!

More explanation on this is needed.
P
Hahahahaaaaa.....Labda mwisho suala la makinikia ilitembea kama ile ' pre bargain' ya DPP' watu wakapata chao.......... Jamani tukubali yaishe.....
 
Magufuli aendelee kuungua moto mkali huko aliko. Hizi takwimu za UWONGO alizopika na Prof Mruma ndizo alizotumia kumjeruhi Tundu Lisu. Magufuli aliwaaminisha watu kuwa tunawadai ACACIA USD 190 billion kutokana na ASUMPTION kuwa container moja la 20ft la MAKINIKIA lina 7Kg za dhajabu wakati ukweli ni kwamba lina 0.7Kg. Akawapa matumaini hewa Watanzania na kwa jinsi WATANANIA wengi walivyo wajinga wakamuona ni shujaa au mkombozi au MZALENDO.

Hizo Tsh 360 Trillion au USD 190 Billion kwa exchange rate ya wakati ule hazipo popote. Ni UJUHA tu kuamini taarifa kama hizo. Magufuli alikuwa anadanganya mpaka Shetani anaogopa
Chuki binafsi tu, hakuna unachoelewa,Watanzania siyo wajinga kama wewe.
 
Back
Top Bottom