Serikali yakiri kuachana na madai ya Tsh. Trilioni 360 za Makinikia

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
7,410
12,276
Wewe unajua container la 20ft linafananaje kweli!
Yaani na wewe unaamini kabisa kuwa kwe copper concentrate (makinikia) ndani ya 20ft container kuna 0.7kg, seriously!!
Kwaiyo kwa akili yako ndogo unaona dhahabu 7kg ni nyingi ndani container la 20ft🤣🤣🤣.Hii nchi CCM itatawala miaka mingi sana,nchi imejaa watu wa ovyo, kwaiyo unaamini hesabu za mwizi kuliko za wataalaamu wetu.Hivi ata wakina Nyerere,Mandela,Nkrumah et al,wangekuwa wanasikiliza mawaidha ya mzungu kuwa hamuwezi kujitawala tungekuwa hapa tulipo.
Ata kama mnapewa bahasha,ni vyema mkawa mnaficha Upuuzi wenu ukouko!
Wewe butron pumbavu Mkubwa hujui kitu wewe. Hizo calculations alizibadili Magufuli baada ya kusoma draft report ya Prof Mruma.
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,024
30,670
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa ufafanuzi kuhusu wapi zipo shilingi trilioni 360 zilizopo kwenye mashauri ya madai 1,095.

Waziri Nchemba amesema, kuna jumla ya mashauri 400 katika mabaraza ya rufani za kodi (TRAT) yenye thamani ya shilingi trilioni 4.2 na dola za Marekani milioni 3.04 zinaendelea katika mabaraza hayo.

Hata hivyo Dkt. Nchemba amesema, serikali ilikubali kupokea shilingi bilioni 700 kutoka Barrick baada ya makubaliano baina ya timu ya serikali iliyoundwa na Rais wa serikali ya awamu ya tano Hayati Dkt. John Magufuli kufikia makubaliano ya pande zote na Barrick kuhusiana na madai ya shilingi trilioni 360.

Amesema baada ya makubaliano hayo ndipo ikaundwa kampuni ya Twiga ambayo inamiliki hisa asilimia 16 na Barrick inamiliki asilimia 84 ya kampuni hiyo.

Ufafanuzi huo wa waziri wa Fedha na Mipango unatokana na maswali ya Mbunge wa jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina aliyetaka kufahamu kwa nini serikali imekubali kulipwa shilingi bilioni 700 kutoka kampuni ya Barrick badala ya shilingi trilioni 360 za awali.

View attachment 2365511

TAZAMA MBUNGE NUSRAT HANJE ALIVYOMWAMBIA WAZIRI "ACHANA NA HIZI WEWE, UTAPATA LAANA"​


 

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,612
2,788
Kumwuliza Mwigulu kuhusiana na hadithi za marehemu kuwa kulikuwa na pesa ya kumnunulia kila mwananchi Noah, ni kumwonea.

Mpina ni mnafiki. Mbona wakati Rais Magufuli akiwa hai hakuthubutu kuuliza hilo swali.

Mwigulu aulizwe na kukabwa vizuri kuhusiana na tozo,siyo makinikia.
 

mambucha

JF-Expert Member
Sep 23, 2013
261
127
Hawa maprofesa wa Makinikia wanatakiwa kuchunguzwa kama waliipotosha serikali na ripoti yao, kwani ripoti ya makinikia ilileta madhara makubwa ikiwemo maelfu ya watu kupoteza kazo, uwekezaji kusuasua kwenye sekta ya madini, serikali kupoteza mapato n.k
@ Mruma na Usoro hatuwezi kuwa na watu wanapotosha serikali na kufanya maamuzi kupitia taarifa ambazo sio sahihi...
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
49,948
86,115
Huyo Mpina anatengeneza mvutano fake na wanaccm wenzake. Lengo ni kucheza na akili za watanzania ili waendelee kuwa na Imani ya kuokoteza kwa CCM. Anadhani bado kuna watu wanaamini tena hayo maigizo ya wanaccm.

Ifahamike kuna mpango wa kutengeneza chama fake cha kujifanya kupambana na ccm, hii ni baada ya watanzania wengi kuonekana kulipuuza box la kura. Hivyo wanataka kutengeneza upinzani fake kwa kutembea na kauli ya Nyerere kuwa upinzani imara utatoka CCM. Lakini baada ya uchaguzi wote watarejea CCM. Tuwe makini na hayo maigizo ya kina Mpina, Mwigulu nk.
 

Ugm bin champion

JF-Expert Member
Dec 11, 2018
1,374
3,388
Habari za hii nchi ni takataka kabisa, yaan ukianza kufuatilia mambo kuhusu maendeleo ya hili taifa inafika muda unakufuru tu, nchi tajiri lkn bado ina wananchi masikini choka mbaya, resources zipo za kila aina lkn bado maisha mabaya.

Kwa rasilimali zilizopo nchini zingeifanya hii nchi kuwa tishio la uchumi duniani hapo bila kutegemea tozo na kodi za kijambazi.

Just imagine tril360 kutoka kwa madini tu zilishpigwa kitaambo na wahuni wasioitakia nchi mema kwa kupitisha mikataba ya kishenzi kwa faida za familia zao.

Je kwa rasilimali zingne tunaweza kujua ni kiasi gani kilipigwa?
Huwa nasema siku zoote hii nchi huenda ina mabilionea wengii east afrika nzima, na mabilionea hawa hawajulikan na hawataki kujulikana maana utajiri wao ni ushenzi mtupu wa kuhujumu mali za taifa.

Hao wanasiasa ndio mabilionea hata akina mo na bakhresa hawaingii ndani, bisha ubishavyo ndivyo ilivyo, pesa zao huficha ktk mabenki nje ya afrika huko USA na Ulaya ambako hawawezi kuchunguzwa chanzo cha mapato Yao.

Kama tungefanikiwa kurudisha hasara waliyotuingiz wanasiasa wetu basi ili taifa kingeweza hata kuzipita nchi tajiri za Asia, ulaya na marekani.

Kushabikia Siasa za afrika ni upumbavu, huo muda bora kuutumia kuangalia pornograph uenda hata ukapata style za kumlizisha mpenzi wako au hata huo muda utumie kufanya mambo yakupayo furaha.

Ukiangaika na hili taifa unapoteza muda wako bure, jipambanie mwenyewe, kumpambania mtu mweusi ni kama laana, hatojari mapambano yako, atakudharau na kumuheshim yule amtesaye
 

Fasta fasta

JF-Expert Member
Feb 15, 2011
1,125
725
Mpina angemuuliza hilo swali Mwendazake na VP aliyekuwa Waziri wa Fedha na Waziri wa Madini na yule kamishna wa TRA aliyeondolewa ndio wanajua kwa nini hawakuzidai hizo pesa badala yake wakachukua bil.700 tuu..
Mwendazake kaondoka na lkulu, wizara husika, serikali yake na chama chake.

Aliyekuwa makamu, waziri mkuu, mwanasheria nao hawapo ili kujibu hoja za wananchi?
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
26,815
46,451
Ukweli upi haliouelezea Lissu,kuwa Serikali hisiwaguse wazungu Maana madini yote yakwao,tukiwagusa tutashitakiwa MIGA,.

..alieleza kwamba ripoti zilikuwa na walakini.

..pia alieleza kwamba tutashtakiwa, na hilo lilitokea baada ya acacia kutushtaki mahakama ya kimataifa.

..tulitakiwa tuandae ripoti ambazo tunaweza kuzitumia kuwashtaki acacia / barrick ndani ya Tz au nje na tukashinda.
 

IDEGENDA

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,289
4,993
Wale maprofesa walimwingiza mwendazake cha kike naye akajaa. Eti Trilion 370! Mwisho wa siku wakapewa 700m na kusema ahsante na kufumba mdomo...
Sasa si bora wamepewa hizo biloni 700 pamona na kuundwa kwa mkataba mpya?

Haya niambie sasa hizi takataka zako zitafanya chochote kwenye madini yetu kweli?

Au ndio zitaruhusu yawe yanaondoka tu?
 

chasuzy

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
591
202
Mimi mtanzania wa kawaida mpaka leo sijaelewa kuwa tuliaminishwa kuwa tunawadai trillion 320 mwisho wa siku tukaambulia billion 700 na 16% .Enzi za mwenda zake ilikuwa haramu kujadili lakini leo hayupo tujulishane ukweli
 

kina kirefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
7,432
7,007
Mpina angemuuliza hilo swali Mwendazake na VP aliyekuwa Waziri wa Fedha na Waziri wa Madini na yule kamishna wa TRA aliyeondolewa ndio wanajua kwa nini hawakuzidai hizo pesa badala yake wakachukua bil.700 tuu..
Taarifa zinakua wizarani mwigulu ndo anajua anatakiwa kujibu Mana hakuna namna yeye ndo mshika fedha zetu
 
6 Reactions
Reply
Top Bottom