Serikali yakata Rufaa kupinga kuachiwa huru kwa Sheikh Ponda

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Uhuru wa Sheikh Issa Ponda umeingia katika sura nyingine kufuatia uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro, ulioumuachia huru kiongozi huyo wa dini aliyekuwa anakabiriwa na mashataka ya uchochezi.

Hatua hiyo imetangazwa jana na Mwanasheria mwandamizi wa Ofisi ya DPP, Bernard Kongola, mwanasheria huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa tayari upande wa mashtaka umeomba nakala ya hukumu na nyaraka za mwenendo wa shauri hilo ili waweze kukata rufaa Mahakama Kuu.

Hata hivyo, alieleza kuwa bado upande wa mashtaka haujapewa nakala ya hukumu hiyo ingawa wameanza kuiomba muda mrefu uliopita, kitu ambacho amedai kinawashangaza.

“Hatujui kuna tatizo gani, maana tunapoomba kupatiwa nakala ya hukumu, hakimu amekuwa anatuambia kwamba bado hawajamaliza kuichapa, kwa kweli hii inashangaza,” Alisema.

Sheikh Ponda na wenzake waliachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Novemba 30 mwaka jana baada ya kutowakuta na hatia katika makosa ya uchochezi na kukiuka amri ya mahakama. Kesi ambayo ilianza kusikilizwa tangu Mwaka 2013.

Chanzo: Dar 24
 
Last edited by a moderator:

Hatua hiyo imetangazwa jana na Mwanasheria mwandamizi wa Ofisi ya DPP, Bernard Kongola. ,wamasheria huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa tayari upande wa mashtaka umeomba nakala ya hukumu na nyaraka za mwenendo wa shauri hilo ili waweze kukata rufaa Mahakama Kuu.

Huu ni Ubaguzi Mwingine na Dhulma dhidi ya Waislam ... Inasikitisha sana matendo anayofanyiwa Sheikh Ponda ...

Hata hivyo, alieleza kuwa bado upande wa mashtaka haujapewa nakala ya hukumu hiyo ingawa wameanza kuiomba muda mrefu uliopita, kitu ambacho amedai kinawashangaza.

“Hatujui kuna tatizo gani, maana tunapoomba kupatiwa nakala ya hukumu, hakimu amekuwa anatuambia kwamba bado hawajamaliza kuichapa, kwa kweli hii inashangaza,” Alisema.

Sheikh Ponda na wenzake waliachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Novemba 30 mwaka jana baada ya kutowakuta na hatia katika makosa ya uchochezi na kukiuka amri ya mahakama. Kesi ambayo ilianza kusikilizwa tangu Mwaka 2013.

Chanzo: Dar 24
 
Sheikh ponda wanamuogopa sana sjui kwanini mbona hana jeshi wala kitengo ila mnamuogopa
 
Kwanza Sheikh Ponda Ndiye Anayestahiki Kufungua Kesi Ya Madai, Kwa SERIKALI KUMUWEKA Rumande Kwa Miaka 2 .3 Pasipo Na DHAMANA!! Kwa Kesi Isiyo Na Kichwa Wala Miguu! Eti Kusema "MANENO YENYE KUUMIZA IMANI YA DINI NYINGINE, NA KUHAMASISHA WATU KUTENDA JINAI NA KUKIUKA HUKUMU YA KUTOTENDA MAKOSA, AKIWA NA KIFUNGO CHA NJE " Mahakama Ya KISUTU Ikaitupa Na Ile Ya Moro Ilishapokea Ushaidi Usio Na MASHIKO Na HAKIMU Alikuwa Anarusha Tarehe Tu Za Kumuachia Sheikh Ponda Kitambo!! Kama SERIKALI Ilikuwa Na Maslahi Na Hiyo Kesi Ya Sheikh Na Wanamlalamikia Hakimu, Mbona Wkt Akichelewesha Uendeshaji Wa Kesi Hiyo Kwa Miaka 2 .3!! Hawakumlalamikia!!!?? Ila Wao Kupata Mwenendo Na Hukumu Ya Kesi Ndio Wanalalama!! WATANZANIA Wangapi Leo Wanaosota Kupata Mienendo Na Hati Za Hukumu Zao MAHAKAMANI!!!!!?? KAMA SERIKALI Inaweza TUNAHITAJI Rufaa Ya Kuachiwa Huru Kwa ABDALAH ZOMBE NA WENZAKE, Mbona Miaka Imekata Hatuisikii!!!??? Je, Kesi Ipi Ina Maslahi Kati Ya ZOMBE NA WENZAKE Au SHEIKH PONDA!!!!??
 
Naoina amani ikichokonolewa sana na hii serikali ya ccm, wameanza na HIZBU, leo tena bara tunakuja kufukua makaburi, yaliyopita si ndwele jamani huyu ponda kesi zote kashinda chokochoko za nini? Hawa wanaochokozwa moto wao haujawahi kuzimwa duniani, watuache tuishi kwa amani na wao watawale kwa amani.
 
Mwachen shekhe wa watu aendelee na maisha yake jaman, kama mahakama imemwachia hur yann malumbano tena, serkali mwogopen mngu nanyi ni binadam kama mlivo nyie mnawafunga mpaka mashekhe mngu atawalaan

ISITOSHE washamuweka ndani zaidi ya miaka miwili
 
Kweli ukitaka umuue Mbwa mwite jina baya,,,,mauwaji yanayo fanywa na wamerekan hata BBC hawayatangaz ila ila kutwa kuwaaminisha watu juu ya alshabab,,IS, wamwache mzee wawatu apumzke
 
Uhuru wa Sheikh Issa Ponda umeingia katika sura nyingine kufuatia uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro, ulioumuachia huru kiongozi huyo wa dini aliyekuwa anakabiriwa na mashataka ya uchochezi.

Hatua hiyo imetangazwa jana na Mwanasheria mwandamizi wa Ofisi ya DPP, Bernard Kongola, mwanasheria huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa tayari upande wa mashtaka umeomba nakala ya hukumu na nyaraka za mwenendo wa shauri hilo ili waweze kukata rufaa Mahakama Kuu.

Hata hivyo, alieleza kuwa bado upande wa mashtaka haujapewa nakala ya hukumu hiyo ingawa wameanza kuiomba muda mrefu uliopita, kitu ambacho amedai kinawashangaza.

“Hatujui kuna tatizo gani, maana tunapoomba kupatiwa nakala ya hukumu, hakimu amekuwa anatuambia kwamba bado hawajamaliza kuichapa, kwa kweli hii inashangaza,” Alisema.
watawakwaza sana waislamu, sasa hivi waislamu wanahisi wanabaguliwa na kunyanyaswa na mfumo kristu, sasa wakiendelea kumuandama huyu jamaa si ndio kuongeza

Back
Top Bottom