Serikali yakanusha tuhuma Wakimbizi kulazimishwa kuondoka nchini. Zaidi ya 7,000 wamejiandikisha kwa hiari kurejea Burundi

Bandamwagaz

Member
Feb 19, 2020
18
36
SERIKALI imekanusha tuhuma zilizotolewa na Waziri anayeshughulika na masuala ya Wakimbizi Nchini Uganda, kuwa Tanzania inawalazimisha Wakimbizi walipo katika kambi mbalimbali Nchini kurejea Burundi bila ridhaa yao.

Akizungumza katika warsha ya maandalizi ya uandishi wa kitabu cha historia ya hifadhi ya wakimbizi nchini, iliyofanyika katika hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha, Simbachawene amesema Tanzania inauzoefu mkubwa na ina historia kubwa katika kuwahifadhi na kuwatunza wakimbizi hivyo tuhuma hizo sio sahihi.

“Nimemsikiliza Waziri anayeshughulika na masuala ya wakimbizi wa Uganda katika kipindi cha BBC Dira ya Dunia akiwa anailaumu Tanzania kwamba inawafukuza wakimbizi na kuwalazimisha waingie Uganda, jambo hilo ni tuhuma nzito, Tanzania inauzoefu mkubwa na ina historia kubwa katika kuwahifadhi na kuwatunza wakimbizi, Tanzania haijawahi kufanya oparesheni wala shughuli yoyote kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda kuwarejesha au kufanya vyovyote vile,” alisema Simbachawene na kuongeza kuwa;

“Tunamshangaa huyu Waziri mwenzangu wa Uganda amelichukua wapi jambo hilo na kulisema kwenye vyombo vya habari vikubwa linatushangaza na kuonyesha masikitiko yetu na kama kulikuwa na njia nyingine tungewasiliana kwanza kwasababu tunafnaya kazi kwa pamoja kuliko hiki alichokifanya, sisi Tanzania ni wazoefu tumehifadhi sio tu wanaotoka nchi nyingine hata Wauganda wenyewe tuliwahifadhi, sasa leo hii sisi tuliowahifadhi wenyewe tukawe watu wabaya katika ukanda huu.”

Aidha, Simbachawene alisema, zaidi ya wakimbizi elfu saba kutoka nchi ya burudi wamejiorozesha kurudi nchini kwao kwahiari na taratibu za kuwarudisha katika nchi hiyo zinaendelea kufanyiwa kazi.

Simbachawene alisema Tanzania ina historia ya yakupokea wakimbizi nchini kwa zaidi ya miaka 60, na zaidi ya wakimbizi elfu tisini tayari walisharudi nchini mwao na hao wengine elfu saba tayari wameshajiorozesha kurudi nchini mwao kwa hiari na si kwakulazimishwa.

“Tanzania imekuwa ikipokea wakimbizi kabla ya Uhuru na baada ya uhuru na yote ni kusema nchi hii ina usalama na ulinzi mzuri kwa wakimbizi kwani takribani wapigania uhuru wa nchi za SADC walijihifadhi katika nchi ya Tanzania,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa, Tanzania ilipokea wakimbizi zaidi ya milioni 1.2 huku wakiwa na kambi 14 za kuhifadhi wakimbidhi hao katika miaka ya 1990, na hadi sasa makundi mengi ya kuhifadhi wakimbizi yamekuwa yakiwatoa wakimbizi katika makazi na kuwapeleka katika makambi maalumu kwa ajili ya usalama zaidi.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Dignity Kwanza, Janemary Ruhundura, ambayo ndiyo Taasisi iliyoandaa warsha hiyo, alisema dhumuni la kuandika kitabu hicho ni kuonyesha kuwa nchi ya Tanzania imekuwa kimbilio kwa wakimbizi hivyo kuna umuhimu wa kutambua nyakati zote za kuhifadhi wakimbizi.

Hata hivyo amesema kuwa mwaka 2003 nchi ya Tanzania ilitoa kibali Cha urai kwa wakimbizi 3000 pia wamatambua mchango mkubwa wa Rais wa Awamu ya Kwanza Mwalimu Julius Nyerere kwani mwaka 1993 alipata tunzo kubwa ya kupokea na kuhifadhi wakimbizi nchini.

“Tunaandika kitabu hicho ili kuendelea kuwakumbusha wananchi pamoja na mataifa mbalimbali wajue nchi ya Tanzania ilivyopokea wakimbizi na inavyoendelea kuwapokea kwa usalama kwa muda mrefu,” alisema Ruhundura.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR), Antonio Canhandula, alisema nchi za Afrika Mashariki wakimbizi waliopo ni milion 4.2, hivyo nchi hizo zimekuwa na ushirikiano mkubwa katika kuwahifadhi Wakimbizi.

“Jukumu la kuwahudumia wakimbizi sio la Watanzania peke yake bali ni la Jumuiya ya Kimataifa ambapo michango mingi imetolewa na Jumuyiya hiyo kupitia taasisi, mbalimbali za kimataifa ikiwemo Shirika la UNHCR,” alisema Canhandula.

*MWISHO*
PIX%201.JPG
PIX%203.JPG
PIX%206.JPG
 
Hii hoja ya Tanzania imekuwa kimbilio la Wakimbizi kwa miaka 60 sidhani kama inatosha kuonyesha kwamba sasa hivi hawafurumushwi.
 
Back
Top Bottom