Serikali yakanusha Rais Magufuli kupiga marufuku nguo fupi

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Habari wakuu,
Itakumbukwa kuna taarifa zilizagaa hasa kwenye vyombo vya kimataifa kuhusu Magufuli kupiga marufuku nguo fupi kama njia za kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya ukimwi.

Leo wizara ya mambo ya nje imekanusha kuhusu agizo hilo na kulishutumu gazeti la Kenya kwa kueneza uvumi huo likisema ni kukosa umakini katika kazi yao.

"Wakati serikali ikifurahishwa na taarifa nzuri za utendaji kazi wa Rais Magufuli katika vyombo vya habari vya Kenya na ulimwenguni kote, Wizara ya Mambo ya Nje imekerwa na utoaji wa taarifa potofu na zisizo makini kama hii ihusuyo sketi fupi," Ilisema sehemu ya taarifa hio.

Serikali kupitia balozi zake za Kenya na Afrika ya kusini kwa kushirikiana na nchi husika zinafanya uchunguzi ili kuwabaini watu waliozusha taarifa hizo na sheria kali zitachukuliwa juu yao.
 
wangepiga tu marufuku mana mademu sasa wanezidi sana na wangepiga marufuku na ile mitight yao
wanakela sana
 
Sera ya Taifa ya Utamaduni inapiga marufuku nguo fupi, zinazoonesha maungo na zisizo na staha. Hata hivyo kwenye majengo na ofisi za umma, nguo za aina hiyo haziruhusiwi na nimeshuhudia kwa macho yangu watu wakikatazwa kuingia kwa kigezo cha mavazi.
Serikali inataka kusema inatangaza rasmi kukiuka kanuni zake yenyewe? Kama huyo mvumi akisema anaegemea Sera ya Utamaduni akihamasisha mavazi ya staha?
 
Tamko la kanusho tumelipokea, nini msimamo wa serikali kuhusu hizo nguo fupi?
 
Back
Top Bottom