Serikali yakanusha kuzuia watumishi wa umma kukopa SACCOS,VICOBA na BANK

Serikali haijazuia mikopo bali benki ndoo zimesimamisha kukopesha.
Benki ni taasisi huru na zinajiendesha kibiashara.

Benki haziwezi kusimamisha mikopo labda useme zimesimamisha baadhi ya mikopo au zimebadilisha utaratibu wa kuchambua maombi ya waomba mkopo.
 
Mpaka sa hivi sielewi nishike lipi... hili nipigo tulionufaika na heslb mpaka mkopo ukatwe wote tutanyooka..
 
Huyu aliyekanusha kakanusha nn? mbona kwene andiko lake hajazungumzia point ya msingi ambayo,ni mnufaika wa wa heslb kama bado anadaiwa hatakopeshwa? binafsi naona kakurupuka hajajibu hoja ya msingi.
 
Serikali ya awamu hii kiboko
Matamko na makanusho take ndo miradi ya maendeleo
 
Huyu D.A. Kabungo ni nani yeye? Dokezo sabili ndiyo nini Waungwana? Serikali ya makanusho kila kukicha!

Kwa hiyo hii ni uongo! Kabungo ni nani? Achukuliwe hatuka kali kuchonganisha watu na serikali yao
fcd0443cb26b55ac1538e6665a7d6298.jpg
 
Kilichokanushwa ni tafsiri na si walaka. Ni vyema tukipewa iliyo sahihi. Pia kwenye mistari miwili ya mwisho wa ule walaka km vile kuna kakichaka. By the way VAT ya vocha za simu na miamala ya an bank na simu ninalipa japo nakumbuka km vilikanushwa vile! Anyway muda huwa ni hakimu mzuri Sana.
 
Halfan Mshana 23:57 habari , matukio
Kumekuwa na taarifa inasambazwa katika mitandao ya kijamii, makundi ya ‘WhatsApp’, ‘Facebook’ na majukwaa mbalimbali ikieleza kuwa Serikali imepiga marufuku watumishi wa umma kukopa Benki,SACCOS,VICOBA na Taasisi mbalimbali za kifedha.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Desemba 2016 na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeeleza kuwa taarifa inayosambazwa, ambayo imetafsiri mawasiliano ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni ya kupotosha, hivyo watumishi wote wa umma wanaombwa kuipuuza.

Vilevile watumishi wa umma wametakiwa kuzingatia kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali HAINA mamlaka ya kuzuia wala kuruhusu mtumishi yeyote wa Serikali kukopa au kutokopa katika Taasisi yoyote ya Fedha nchini.

Watumishi wa umma pia wamekumbushwa kuwa mikopo yote ya watumishi wa umma katika Taasisi za Fedha hutolewa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo ili mradi mtumishi awe ametimiza vigezo.

Aidha, watumishi wa umma wameaswa kuacha tabia ya kusambaza taarifa zisizo za kweli na ambazo zina mamlaka husika ya kuzitoa ikiwa ni pamoja na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

g.jpg
 
Back
Top Bottom