Serikali yakanusha kuzuia watumishi wa umma kukopa SACCOS,VICOBA na BANK

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,162
2,000
Kumekuwa na taarifa inasambazwa katika mitandao ya kijamii, makundi ya ‘WhatsApp’, ‘Facebook’ na majukwaa mbalimbali ikieleza kuwa Serikali imepiga marufuku watumishi wa umma kukopa Benki,SACCOS,VICOBA na Taasisi mbalimbali za kifedha.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Desemba 2016 na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeeleza kuwa taarifa inayosambazwa, ambayo imetafsiri mawasiliano ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni ya kupotosha, hivyo watumishi wote wa umma wanaombwa kuipuuza.

Vilevile watumishi wa umma wametakiwa kuzingatia kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali HAINA mamlaka ya kuzuia wala kuruhusu mtumishi yeyote wa Serikali kukopa au kutokopa katika Taasisi yoyote ya Fedha nchini.

Watumishi wa umma pia wamekumbushwa kuwa mikopo yote ya watumishi wa umma katika Taasisi za Fedha hutolewa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo ili mradi mtumishi awe ametimiza vigezo.

Aidha, watumishi wa umma wameaswa kuacha tabia ya kusambaza taarifa zisizo za kweli na ambazo zina mamlaka husika ya kuzitoa ikiwa ni pamoja na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

TAARIFA YA KUKANUSHA0001.jpg
 

kilokiki

JF-Expert Member
May 3, 2016
1,366
2,000
Ni hatari niliamua kukaa kimya maana ingekuwa ni kweli ingekuwa ni kichekesho cha mwaka.
Natamani kuwaona wale waliokuwa wanatetea
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,386
2,000
Swala hapa ni taarifa hiyo ipo au haipo maana inawezekana ipo ila tu imetafsiriwa vibaya.

Yaana mbona hawajaikana hiyo document moja kwa moja na badala yake wanaonekana kukana jinsi document ile ilivyotafsiriwa?

Kama ni upotoshaji ni wazi ulikuwa kwenye heading ya ile thread tu na si vinginevyo

Hapa binafsi wameniacha na maswali.
 

DAFU NA NDIMU

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
3,456
2,000
Kama ingekaa vile vile kusingekuwa na shida pia na kama ni uongo bado ni kosa wa aliyeileta
Kungekuwa na shida kubwa sana ktk nyanja nyingi . Kubwa zaidi ni ukiukaji wa sheria za kazi ambao ungeshusha zaidi morali ya kufanya kazi. Pia ungeyumba kiasi fulani.
Ushabiki hata kwa vitu vinavyoonekana kukiuka kanuni na sheria za kazi hunipa shida kuelewa uelewa wa watz ktk kufikiri.
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,230
2,000
Ile taarifa ya jana iliyoletwa hapa nilitoa angalizo na kusema, kichwa ha habari cha mleta taarifa kilikuwa kinapotosha kwa sababu maudhui ya taarifa yalikuwa tofauti na kichwa cha habari.

Mbaya zaidi, Watanzania wengi huwa wanasoma kichwa cha habari/mada na kuanza kutoa komenti badala ya kusoma maudhui ya habari/taarifa.

Hakuna kwenye maudhui ambapo iliandikwa kuwa watumishi wa umma wamezuiwa kukopa kama bado wanadaiwa na Bodi ya Mikopo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom