kiluwiluwi
Member
- Mar 14, 2011
- 15
- 1
taarifa za kujiuzulu zatolewa na magazeti ya udaku au credible sources?
Akiandika barua hawezi kumpa nakala katibu mkuu wake atapewa rais mwenyewe labda kuptia kwa katibu muu kiongozi, hivyo taarifa imetoka kwa asiye sahihi. Watu sahihi wa kuliongelea ni Pombe mwenyewe, JK na Luhanjo vinginevyo serikali haijatoa taarifa
Hiyo ofisi unayofanya kazi haifuati taratibu za Serikali; Barua lazima iwe na Kumbukumbu Na., pia iwekwe kwenye faili (Jalada) husika, Mmiliki wa Majalada yote ya Serikali Wizani ni Katibu Mkuu (Custodian), full stop.
Katibu Mkuu ndie Msemaji Mkuu wa Serikali katika ngazi ya Wizara, pia anaweza kuagizwa na Rais au Katibu Mkuu Kiongozi kutoa ufafanuzi wa jambo lolote kwaniaba ya Serikali, husidhani alijiamulia yeye kutoa ufafanuzi wa Bwana Misifa.
Kama Rais na Katibu Mkuu Kiongozi hawana barua ya kujiuzulu kwa Bwana Misifa, mtu sahihi wanayew kumuuliza ni Katibu Mkuu kama barua ipo kwenye Jalada labda haijafika tu! Kama nae hana katika Jadala ni trick nzuri sana kumwambia Katibu Mkuu ebu kanusha alafu tuone yeye atafanya nini au atasemanini ili 'Tumshughulikie huyo Mpotofu, yaani anataka kusema kwenye list ya ahadi kuna ahadi ya Bomobomo bila kufuata sheria na Taratibu za nchni huku ukiacha watanzania bila makazi?!' Kama akikaa kimia basi tujue anatikisa kiberiti.
Akiendelea kukaa kimia basi ndio ponapona yake ila hafai hata kuwa Barozi wa Nyumba kumi

Nyerere alikuwa makini, hakuwa mtu wa kuendeshwa na wapenda sifa, watanzania walimshangaa katika kuibua viongozi mara zote walipo fikiri kusiki jina la mpenda sifa fulani Mwl aliibuka na jina ambalo hata halijunikani vichwani mwa wengi. Hii ilikuwa hata kwa kada ya Watendaji wakuu kama Mkatibu wakuu, Wakurugenzi, Wakuu wa vyombo vya Dola nk.
Siku hizi watu wanamjua IGP ajae kabla hata Mamlaka ya uteuzi haijaingia madarakani, hivyo hivyo kwa CDF, Mkuu wa UWT, Wakurugenzi nk. unaweza kukutana na mtu akakwambia nasubiria kuwa Mkurugenzi au Katibu mkuu kiongozi soon.
Watu wanasubiri nafasi zao za RC ndio maana utasikia kila siku wanauliza mbona Rais anachelewa kutangaza majina ya RC's wanajulikana, Wanasiasa wametusoma sawasawa wanatujua Watanzania uwezo wetu wa kuchambua na tamaa zetu za kupewa hongo wakati wa Uchaguzi. Kuna mtu anaweza kujua kwanini Mkono kila mara hana mgombea hata wa upinzani? Kwanini wakina MO wanashinda bila shaka huko Singida?, Kama RA hafai na mchafu kwa Umma wa Tanzania kwanini anashinda kwa kishindo huko Igunga pamoja na kelele zote zinazopigwa? Zaidi ya wa 90% ya wapiga debe wa Pombe hawawezi kujibu hayo maswali bila kupindisha.
Katika wimbo wa Taifa tunatakiwa kubadilisha kile kipengere cha "Mungu Ibariki Tanzania" iwe "Mungu Isaidie Tanzania" wananchni wengi wanahitaji kusaidiwa hawajijui hata kidogo.
Nina wasiawasi kama vile unataka kupotosha mambo. Rejea uteuzi wa waziri husika. Hakuna suala la kumbukumbu katika wizara husika katika hatua za mwanzo za uteuzi vinginevyo siri itakuwa inafichuka. Vile vile waziri huteuliwa na rais kwa jina. Naomba utuambie, kama barua anayoandika waziri kuhusu kujiuzulu kwake na kuwekewa kumbukumbu za wizara usiri katika suala hilo uko wapi?
Sidhani kama suala la waziri kujiuzulu ni la kiwizaara zaidi ya suala linalohusu mamlaka ya uteuzi wake ambayo ni ikulu. Ninadhani kama Magufuli kama angeweka kumbukumbu katika barua yake angetumia kumbukumbu za barua yake binafsi.
Hapo penye red- wanaokiuka sheria ni kina nani, Magufuli au walojenga katika hifadhi ya barabara? ma-bush lawyers mnatusumbua hapa Jf huku mki-mislead umma kwa hoja chakavu. Watu tunalia na foleni kwa vile wajinga fulani wamevunja sheria na kujenga kwenye barabara, halafu tukitaka kubomoa makazi mnaanza ooh! haki za binadam. Uchumi unaopotea kwa foleni za barabarani unazidi hivyo vibanda holera vilivyojengwa katika hifadhi ya barabara. Tuseme ukweli tuache kuropka. Kama huna hoja kalale, Magufuli songa mbele na bomoa bomoa, usimsikilize mtu.
hapo kwenye red nakukubali, ila ningependa kama ungeendelea kidogo kuchambua makundi ya wananchi wajinga na seheme/eneo walipo (kwa wingi zaidi) ili elimu ielekezwe huko. nina amini kundi la wajinga wengi hawasomi JF NA HATA MAGAZETI NA VYOMBO VINGINE VYAWAFIKIA KWA NADRA. Kumbuka asilimia 80 ya sisi Wa-TZ ni mambumbu na maskini tunaoishi chini ya dola moja kwa siku na hiyo asilimia 80 ipo huku vijijini kwetu, siyo huko mjini kwenu kwenye JF, NA HAO 80% ndiko mafisadi wanakogawa kanga na kofia kupora uongozi. Njia mbadala kama zinazotumiwa na CHADEMA ni muhimu ziendelee kubuniwa na kutumika kufikisha elimu na maarifa hasa kwa sisi wadanganyika wa vijijini.(samahani kwa kutoka nje ya mada kidogo, nia ni kufikisha tu elimu kila unapojitokeza upenyo)
Sio Kujiuzulu ni kujidhuru Teh teh haha haaaa
Mhhh jamani tujitahidi kuandika kiswahili fasaha, hatusemi "Unamulaumu" bali unamlaumu. Pia hatusemi "Kujihuzuru" bali Kujiudhuru.
Heshima kwako Mathias Byabato.
Ingawa jina lako la mwisho linatumiwa na watu wa Kagera lakini nina wasiwasi wewe utakuwa mpare.Unashindwa kuandika kujiuzulu je kuongea itakuwaje ?.
Shikamoo mkuuhawa jamaa nafikiri ni njama au mipango ya kumtangaza kisiasa kwenda uchaguzi wa 2015.
Oh.Nami nilshtuka.nikafikiri account yangu imeingiliwa.Shiiiit, kumbe uzi wa 2011 bhana! Mimi nilidhani ni wa leo,
Profet figganigahawa jamaa nafikiri ni njama au mipango ya kumtangaza kisiasa kwenda uchaguzi wa 2015.