vipofu wanapoongozana, 'kujiuzulu' siyo 'kujiudhuru'
Mkuu kipilipili, waache tu hao vipofu wakatumbukizane huko kunako handaki. Nchi ikishapoteza dira na mwelekeo tabu sana..hapa tatizo si la hao vipofu wawili hapo juu, ila ni mfumo mbovu wa elimu, na kwenye lugha tatizo halijatuhurumia hata chembe..angalia unaanza 'kendagateni" unafundishwa kwa kiswahili, unaingia la kwanza mpaka la saba ni kiswahili...akili inaanza kujengeka vizuri na kujipanga....mara vuuuuuu bin vuuuuuu unaanza kushindiliwa "kingeledha" unapoanza "fomu wani"...huna msingi wa hicho kiingeledha.. so ka-msingi ni ka kujenga nyumba ndongo ya vyumba viwili, lakini hatimaye linakuja kulazimishwa ghorofa la "floo" kumi juu ya hako ka-mzingi--teh teh tehi!!!!!!!!!!! matokeo kwenye kingeledha hatumo kwenye kiswahili hatumo. tumejaribu kuunda lugha-pori yakusaidia kupunguza tatizo - "kiswa-inglidhi" lakini nacho tabu tu zaidi. solusheni ya haraka ya watawala vichwa maji ni kugawa wanafunzi..wa watawala "wa-enroool" kwenye "akademiiiz" na "seints" na wale wa wakulima "wa-enirool" kwenye zile za kata, lakini kodi wote wanachanga.....matokeo yake ndo hawa vipofu, "akchuale" si hawa vipovu ndo vipovu ila ka-nchi kalikokuwa kametukuka sasa kamekuwa kipofu, hakaoni tena na kanaelekea handakini. mafisadi yanakata tawi walilokalia, nayo yatatumbukia huko huko kunako handakini...Nyie ngojeni tu "T" will "T"(Time will Tell)
mafisadi yanatutesa na kutulostisha sana watoto wa pizants...lakini ipo siku Insha-Allah...