Adrian Stepp
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 2,764
- 2,581
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Imesema Watanzania wanatakiwa kupuuza taarifa zinazosambazwa kuhusu kutopokea simu endapo utapigiwa kwa namba +255 901 009 999 kwamba utadhurika.
Akizungumza katika mahojiano maalum nasi, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Innocent Mungy amesema jambo kama hilo kiteknolojia halijawahi na haliwezi kutokea kwamba mtu akipokea simu aweze kuzimia/ kudhurika labda muhusika apewe taarifa za jambo la kijamii kama taarifa za msiba nk.
Aidha ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kupokea simu na kujibu jumbe fupi kama kawaida kwakua jambo hilo halipo katika ulimwengu wa kiteknolojia labda kwa wale wanao amini katika sayansi ya Uchawi ambapo kwenye teknolojia suala hilo halipo!.
Awali kulikua na taarifa zilizokua zinasambazwa mtandaoni kwamba Mkazi mmoja Wilayani Bunda, Mkoani Mara alipokea simu kwa namba tajwa na hadi sasa hali yake ni mbaya.
Akikanusha taarifa hizo, Mkuu wa Wilaya hiyo na Kamanda wa polisi wilayani hapo wote kwa pamoja wamekanusha kuwapo kwa taarifa hizo wilayani humo.
"Sosi"- Mimi Mwenyewe.