Serikali yakanusha kuhusu namba +255 901 009 999

Adrian Stepp

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
2,764
2,581
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Imesema Watanzania wanatakiwa kupuuza taarifa zinazosambazwa kuhusu kutopokea simu endapo utapigiwa kwa namba +255 901 009 999 kwamba utadhurika.

Akizungumza katika mahojiano maalum nasi, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Innocent Mungy amesema jambo kama hilo kiteknolojia halijawahi na haliwezi kutokea kwamba mtu akipokea simu aweze kuzimia/ kudhurika labda muhusika apewe taarifa za jambo la kijamii kama taarifa za msiba nk.

Aidha ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kupokea simu na kujibu jumbe fupi kama kawaida kwakua jambo hilo halipo katika ulimwengu wa kiteknolojia labda kwa wale wanao amini katika sayansi ya Uchawi ambapo kwenye teknolojia suala hilo halipo!.

Awali kulikua na taarifa zilizokua zinasambazwa mtandaoni kwamba Mkazi mmoja Wilayani Bunda, Mkoani Mara alipokea simu kwa namba tajwa na hadi sasa hali yake ni mbaya.

Akikanusha taarifa hizo, Mkuu wa Wilaya hiyo na Kamanda wa polisi wilayani hapo wote kwa pamoja wamekanusha kuwapo kwa taarifa hizo wilayani humo.

"Sosi"- Mimi Mwenyewe.
 
Ukiamini hii daima uko shidani
�� ImageUploadedByJamiiForums1400759374.544184.jpg
 
Hivi kuna watu walikuwa wanaamini hizo porojo za kupokea hiyo number?
 
Mimi nadhan ni watu mitandao mingine wanataka kuwaharibia watu wa mtandao wa Smart kwa sabab jana asbh niliipokea sim ya namba hiyo na walichokuwa wanasema ni kuhusu kujiunga na caller tune zao sikuona zaid ya hapo.
Zaid zaid ni kuwaharibia tu watu wa huo mtandao na navyosikia kuwa wako vizuri sana kwenye internet lazima wengine waogope!
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Imesema Watanzania wanatakiwa kupuuza taarifa zinazosambazwa kuhusu kutopokea simu endapo utapigiwa kwa namba +255 901 009 999 kwamba utadhurika.

Akizungumza katika mahojiano maalum nasi, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Innocent Mungy amesema jambo kama hilo kiteknolojia halijawahi na haliwezi kutokea kwamba mtu akipokea simu aweze kuzimia/ kudhurika labda muhusika apewe taarifa za jambo la kijamii kama taarifa za msiba nk.

Aidha ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kupokea simu na kujibu jumbe fupi kama kawaida kwakua jambo hilo halipo katika ulimwengu wa kiteknolojia labda kwa wale wanao amini katika sayansi ya Uchawi ambapo kwenye teknolojia suala hilo halipo!.

Awali kulikua na taarifa zilizokua zinasambazwa mtandaoni kwamba Mkazi mmoja Wilayani Bunda, Mkoani Mara alipokea simu kwa namba tajwa na hadi sasa hali yake ni mbaya.

Akikanusha taarifa hizo, Mkuu wa Wilaya hiyo na Kamanda wa polisi wilayani hapo wote kwa pamoja wamekanusha kuwapo kwa taarifa hizo wilayani humo.

"Sosi"- Mimi Mwenyewe.
Ningependa kujadili hapo kwenye red.
Inategemea unapokea simu ukiwa katika mazingira gani! Naomba kutoa rai kuwa ni hatari kupokea simu ukiwa karibu na vitu vinavyoweza kusababisha moto kwa urahisi kama Petrol, Gesi n.k. Vifaa hivi vya mawasiliano (electronics) vina umeme ndani yake na inawezekana kabisa kuwa kupokea simu karibu na vitu vinavyoweza kusababisha moto unaweza kupoteza maisha!
Kwa jinsi watu wengine tulivyo wabishi au wepesi wa kupuuzia mambo. Watu wanazungumza na simu wakiwa karibu kabisa na vitu hivyo vishikavyo moto au mahali kwenye vitu hivyo! Mfano watu wanazungumza na simu wakiwa kwenye vituo vya mafuta (Petrol Stations) au Mafundi wa welding, au wapishi wanaotumia gesi kupikia! Tena kwenye vituo vingi vya mafuta kuna alama za tahadhari zikionyesha usitumie simu kwenye mazingira hayo lakini watu wanafanya vinginevyo! Inawezakana kukatokea uvujaji wa gasi au mafuta na ikasababisha madhara makubwa kwa watu mali zao.
Hata kutumia simu wakati ukiwa kwenye mvua ni hatari, kwa uelewa wangu kidogo wa sayansi "maji ya mvua yanapitisha umeme" hivyo yapoingia kwenye simu wakati unaongea yanaweza kuleta itilafu kwenye mfumo wa umeme wa simu yako hivyo betri ikazidiwa nguvu "Boooom" kwenye sikio lako.
 
tanzania ilivyotajwa kwenye tatu bora za uchawi duniani watu walishangaa sana....kwa hali hii ya kuamini ukipokea hii namba unadhurika wala sishangai na waliotoa ile habari....mimi leo nimepokea hii namba 0901006666 nikasikiliza sekunde chace nikasikia mambo kama promotion hivi nikaikatilia mbali kwa sababu huwa sipendi kupoteza muda na promotion
 
Ningependa kujadili hapo kwenye red.
Inategemea unapokea simu ukiwa katika mazingira gani! Naomba kutoa rai kuwa ni hatari kupokea simu ukiwa karibu na vitu vinavyoweza kusababisha moto kwa urahisi kama Petrol, Gesi n.k. Vifaa hivi vya mawasiliano (electronics) vina umeme ndani yake na inawezekana kabisa kuwa kupokea simu karibu na vitu vinavyoweza kusababisha moto unaweza kupoteza maisha!
Kwa jinsi watu wengine tulivyo wabishi au wepesi wa kupuuzia mambo. Watu wanazungumza na simu wakiwa karibu kabisa na vitu hivyo vishikavyo moto au mahali kwenye vitu hivyo! Mfano watu wanazungumza na simu wakiwa kwenye vituo vya mafuta (Petrol Stations) au Mafundi wa welding, au wapishi wanaotumia gesi kupikia! Tena kwenye vituo vingi vya mafuta kuna alama za tahadhari zikionyesha usitumie simu kwenye mazingira hayo lakini watu wanafanya vinginevyo! Inawezakana kukatokea uvujaji wa gasi au mafuta na ikasababisha madhara makubwa kwa watu mali zao.
Hata kutumia simu wakati ukiwa kwenye mvua ni hatari, kwa uelewa wangu kidogo wa sayansi "maji ya mvua yanapitisha umeme" hivyo yapoingia kwenye simu wakati unaongea yanaweza kuleta itilafu kwenye mfumo wa umeme wa simu yako hivyo betri ikazidiwa nguvu "Boooom" kwenye sikio lako.

mkuu naomba nikuulize kwa nia njema tu....tangu umeijua mobile phone ushasikia/kushuhudia matukio mangapi ya watu kulipua petrol station au mitungi ya gas kwasababu ya mobile phone??? mimi kwa kweli sijawahi kusikia hata tukio moja.

nilichokisikia na kukisoma sana ni tukio la mtu kulipukiwa na simu aliyokuwa anitumia ikiwa kwenye charger.
 
Labda nikuulize kwanini imelipuka akiwa anaongea kwenye charger? Je sayansi behind nini? Mara ngapi watu wanaongea na simu zikiwa kwenye charger?
Zote ni ajali kamanda, na kinga ni bora kuliko tiba! Kama ikitokea kuvuja au itilafu kwenye vifaa vya kutunzia hivyo vitu basi inawezekana ikatokea ajali ya namna hiyo!
Labda unaweza kufanya very simple experiment ili kuthibitisha kama itawaka au laah!
***But don't try it at home! & Be alone when you do it!***
 
mkuu hujajibu swali unauliza swali ambalo kiini chake ni experience yangu. wewe uliesema kuwa ni hatari kwasababu inaweza kuleta milipuko naomba uniambie umewahi kusikia mlipuko wa kituo cha mafuta kwa sababu mtu/mteaja alipokea simu?? au mitungi ya gas sehemu imelipuka kwa sababu mtu kapokea na kuongea na simu?? naomba tu unieleze kama ushawahi kusikia hilo tukio.

kuhusu kulipuka kwenye charger huwa ni faulty battery. ambayo hata usipopokea au kuongea inaweza kulipuka.

naomba nijibu swali langu.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom