Serikali yakanusha kufukuza wageni na wafanyabiashara kuwekeza nchini

Jay Milionea

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
1,185
154
Hivi karibuni kumejitokeza uzushi unaosambazwa katika mitandao ya kijamii ya ndani ya nchi na nje ya nchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amefukuza wageni kutoka nje waliokuwa wanafanyabiashara zao nchini kwa kuwa serikali yake haitaki wageni kufanya biashara nchini.

Serikali haijafukuza wageni kutoka nje ya nchi kufanya biashara nchini na haina mpango wa kuwafukuza wageni wanaoishi nchini kwa vibali vilivyotolewa kisheria na Idara ya Uhamiaji.

Uzushi huo usiokuwa na ukweli umeenezwa kufuatia Idara ya Uhamiaji kutekeleza jukumu lake la kufuatilia wageni wote wanaoishi nchini bila vibali halali vya ukaazi ambapo kwa mwezi Novemba na Desemba mwaka 2015 wageni 372 walioondoshwa nchini.

Kazi ya kufuatilia wageni wanaoishi nchini bila vibali halali vya kisheria haijaanza katika Serikali ya Awamu ya Tano. Idara ya Uhamiaji nchini tangu Januari hadi Desemba mwaka jana iliondosha nchini jumla ya wageni 1,642 waliokuwa wanaishi na kufanya shughuli zao nchini kinyume na Sheria.

Uzushi unaoenezwa hauna ukweli wowote na hauna nia njema na nchi yetu kwani kati ya mwaka 2014 na 2016 Idara ya Uhamiaji imetoa vibali vya ukaazi (Residence Permits) 40,765 kwa wageni wawekezaji na wafanyabiashara, wageni wanaofanyakazi za kuajiriwa, wageni wanaokuja kwa ajili ya Masomo, matibabu, dini, utafiti na wastaafu kuishi na kufanya shughuli zao nchini.

Serikali inawakaribisha wageni kuja nchini kuwekeza na kufanya shughuli zao kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi.

Aidha, kuna uzushi unaenezwa kuwa Rais Dkt John Pombe Magufuli amepiga marufuku wanawake kuvaa nguo fupi kama njia ya kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI.

Mheshimiwa Rais tangu aingie madarakani hajawahi kuagiza wala kutoa tamko kuhusiana na uzushi wa kukataza uvaaji wa nguo fupi ili kupunguza maambukizi ya Ukimwi kama inavyoenezwa katika mitandao ya ndani na Nje ya Nchi ambayo inanukuu habari hiyo kuwa imeandikwa na Gazeti la Kenya “The Standard”

Serikali inapenda kuutangazia umma kuwa uzushi huo unaomhusu Mheshimiwa Rais Magufuli umetungwa na watu wasioitakia mema nchi yetu kwa lengo la kumdhalilisha Rais na hauna ukweli hivyo watu wasishiriki kuueneza kwa njia yeyote ile.

Serikali kupitia balozi zake za Kenya na Afrika Kusini zinafuatilia chanzo cha uzushi huu kuhusu Rais Magufuli kwa kushirikiana na nchi husika na watakaobainika kutunga na kueneza uzushi huu watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho.
 

Attachments

  • SERIKALI KANUSHA UZUSHI.pdf
    103.3 KB · Views: 96
Mheshimiwa Rais tangu aingie madarakani hajawahi kuagiza wala kutoa tamko kuhusiana na uzushi wa kukataza uvaaji wa nguo fupi ili kupunguza maambukizi ya Ukimwi kama inavyoenezwa katika mitandao ya ndani na Nje ya Nchi ambayo inanukuu habari hiyo kuwa imeandikwa na Gazeti la Kenya “The Standard”

Gazeti la The standard lifungiwe Tanzania
 
Ameshasema ule ni uzushi sasa anataka kumtafuta nani? Hii ni Tanzania,siyo Uzbekistan,siyo Burundi.
 
Sasa hutaki wazushi washighulikiwe?? Au unawajua wahusika uisaidie polisi. Ukizingatia wewe ni mtoto wa baba wa Taifa tunategemea kukuona mstari wa mbele ktk kutetea MASLAHI MAPANA YA NCHI HII.

Hivi siku hizi kaka Andrew unajishughulisha na nini hasa ktk kutafuta kipato??

Queen Esther

Ameshasema ule ni uzushi sasa anataka kumtafuta nani? Hii ni Tanzania,siyo Uzbekistan,siyo Burundi.
 
Ni vyema serikali badala ya kutoa nyaraka za kukanusha habari za media, iwape agizo wahusika kutoa ushahidi/uthibitisho/chanzo cha huo uzushi. Wakishindwa, basi waagizwe kukanusha na kuomba radhi kupitia chombo chao wenyewe. Kama ni gazeti waweke habari kamili ya kanusho ukurasa wa mbele. Kama ni redio na tv, iwe habari ya kwanza. Wapewe na deadline ya agizo. Vinginevyo wanachukuliwa hatua za kisheria.

Athari za serikali kutoa waraka wake kukanusha bila kuwashughulikia wahusika, ni kuruhusu uvumi uendelee kichinichini. Ifahamike kuwa hulka ya watu kutoiamini serikali ni kubwa sana hivyo watakuwepo wengi watakaochukulia waraka wa kanusho kama "geresha".
 
Back
Top Bottom