Serikali yakacha kutokea Mahakamani kwenye kesi dhidi ya Kampuni ya ujenzi Konoike. Yadaiwa Dola Milioni 60

Sasa hii ni tu machi. Asante kwa taarifa ila yauma. Ukisearch google case zilizopo inc tribunal za tz ni nyingi.
 
Hapa mpaka jpm atajuta. Wazungu ndo zao na kama haya madeni hayalipwi na akaelekea china tu inakula kwetu
 
Kwa kweli ni aibu!
Wafukue tu kwani mlipoyasababisha na serikali ya ccm mlitushirikisha cdm? Mlikuwa mnashauriwa mnapuuza. Tukieni sindano ziingie iwe aibu kwenu na mtazomewa kama mazimwi duniani kote isipokuwa rwanda uganda na burundi
 
Mnafikiri kukaa kila kukicha kutafuta habari hasi ndio mtashinda uchaguzi na kwenda Ikulu?
Uko mjinga eeh? Habari hasi ndo nini? Nakuukiza ww una akili? Yaani huu ujinga unataka tunyamaze? Hii aibu tunyamaze? Tutaongea na acha wakamate tujifunze kuchagua rais makini.
 
haya madeni hatukuyasikia hapo awali au kuna watanzania wanamaslahi?
Hata kama wana maslahi ni ccm. Halafu deni linakuwa baya kama huendi kujadiliana na badala yake unakacha. Na unajua watakamata hadi meza za balozi zetu majuu, magari, mpaka peaa zao zitimie
 
Kampuni ya ujenzi ya Konoike ya Japan imeiomba mahakama ya Washington DC, Marekani kuziwekea ‘defaults’ taasisi kadhaa za serikali ya Tanzania kutokana na kupuuzwa kwa hukumu ya malipo ya dola milioni 60 kwa kampuni hiyo, lakini serikali ya Tanzania imekuwa haitokei mahakamani.

Kampuni hiyo imeeleza kuwa iliwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania Oktoba mwaka jana, na wanasheria wa Wizara hiyo walikiri kufahamu kuhusu kutakiwa kulipwa fedha hizo lakini wakaamua kupuuza.

Konoike imeeleza kuwa serikali ya Tanzania ililipa dola 11.3 mwezi uliopita kufuatia ushauri wa kisheria uliotolewa jijini London, Uingereza, lakini kiasi hicho kilikuwa kidogo mno kulinganisha na kiwango halisi kinachopaswa kulipwa pamoja na riba, yaani dola milioni 65 tangu hukumu ilipotolewa Februari mwaka jana.

Katika hukumu hiyo, Wakala wa Barabara (TANROADS), Wizara ya Ujenzi, na taasisi nyingine za serikali ziliingia mkataba na kampuni nyingine kumalizia ujenzi wa barabara ya maili 79 baada ya Konoike kutoa notisi ya kuvunja mkataba.

Serikali ya Tanzania inadai kuwa malipo hayo ya dola milioni 11.3 ndio ya mwisho baada ya kukata kodi iliyokuwa ikidaiwa tangu mwaka 2016. Konoike inasema dai hilo si halali wala la kweli.
Wakamate kila kitu maana ccm tu ndo wanufaika, wengine yetu gereza
 
Hivi wakandarasi wa Tz wanafanyaga nini? Kazi hizi za ujenzi zingekuwa zinafanywa na wakandarasi wa ndani.
Wahandisi tunao na wengine wamesoma huko huko majuu, lakini kwa nini hatuoni matunda yao? Wanajisifu kuwa na vyeti vizuri visivyo na msaada kwa jamii!
Tukakaa tunahangaishana na hawa watu weupe wanachukua pesa zetu bure tu.

Wahandisi amkeni muingie kazini. Tutawategemea watu weupe hadi lini wakati na ninyi mpo?
 
sasa tumemalizana na Canada ili parade la chuma lije na lisu tushaanza kumshambulia na nyie konoike mmeanza kuinyemelea sasa tutaficha wap sura zetu
 
Back
Top Bottom