Serikali yakacha kutokea Mahakamani kwenye kesi dhidi ya Kampuni ya ujenzi Konoike. Yadaiwa Dola Milioni 60

Kampuni ya ujenzi ya Konoike ya Japan imeiomba mahakama ya Washington DC, Marekani kuziwekea ‘defaults’ taasisi kadhaa za serikali ya Tanzania kutokana na kupuuzwa kwa hukumu ya malipo ya dola milioni 60 kwa kampuni hiyo, lakini serikali ya Tanzania imekuwa haitokei mahakamani.

Kampuni hiyo imeeleza kuwa iliwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania Oktoba mwaka jana, na wanasheria wa Wizara hiyo walikiri kufahamu kuhusu kutakiwa kulipwa fedha hizo lakini wakaamua kupuuza.

Konoike imeeleza kuwa serikali ya Tanzania ililipa dola 11.3 mwezi uliopita kufuatia ushauri wa kisheria uliotolewa jijini London, Uingereza, lakini kiasi hicho kilikuwa kidogo mno kulinganisha na kiwango halisi kinachopaswa kulipwa pamoja na riba, yaani dola milioni 65 tangu hukumu ilipotolewa Februari mwaka jana.

Katika hukumu hiyo, Wakala wa Barabara (TANROADS), Wizara ya Ujenzi, na taasisi nyingine za serikali ziliingia mkataba na kampuni nyingine kumalizia ujenzi wa barabara ya maili 79 baada ya Konoike kutoa notisi ya kuvunja mkataba.

Serikali ya Tanzania inadai kuwa malipo hayo ya dola milioni 11.3 ndio ya mwisho baada ya kukata kodi iliyokuwa ikidaiwa tangu mwaka 2016. Konoike inasema dai hilo si halali wala la kweli.

Chanzo: Evirist Chahali

Safi sana. Walifikiri kesi ipo mahakama ya kisutu.!
 
Leo mtaleta sana vihabari uchwara lakini ndege iko njiani inakuja TZ poleni sana najua inawauma sana!!
Ungejiuliza gharama zilizotumika kuinunua hiyo Bombadia ungetoa machozi kama una akili.
Bei ya kununulia + gharama za kulipa deni + riba ya deni = Boeing 787 not Bombadier. Sasa jee huo sio ufala kujisifu kama mazuzu?
 
Kampuni ya ujenzi ya Konoike ya Japan imeiomba mahakama ya Washington DC, Marekani kuziwekea ‘defaults’ taasisi kadhaa za serikali ya Tanzania kutokana na kupuuzwa kwa hukumu ya malipo ya dola milioni 60 kwa kampuni hiyo, lakini serikali ya Tanzania imekuwa haitokei mahakamani.

Kampuni hiyo imeeleza kuwa iliwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania Oktoba mwaka jana, na wanasheria wa Wizara hiyo walikiri kufahamu kuhusu kutakiwa kulipwa fedha hizo lakini wakaamua kupuuza.

Konoike imeeleza kuwa serikali ya Tanzania ililipa dola 11.3 mwezi uliopita kufuatia ushauri wa kisheria uliotolewa jijini London, Uingereza, lakini kiasi hicho kilikuwa kidogo mno kulinganisha na kiwango halisi kinachopaswa kulipwa pamoja na riba, yaani dola milioni 65 tangu hukumu ilipotolewa Februari mwaka jana.

Katika hukumu hiyo, Wakala wa Barabara (TANROADS), Wizara ya Ujenzi, na taasisi nyingine za serikali ziliingia mkataba na kampuni nyingine kumalizia ujenzi wa barabara ya maili 79 baada ya Konoike kutoa notisi ya kuvunja mkataba.

Serikali ya Tanzania inadai kuwa malipo hayo ya dola milioni 11.3 ndio ya mwisho baada ya kukata kodi iliyokuwa ikidaiwa tangu mwaka 2016. Konoike inasema dai hilo si halali wala la kweli.
Mkuu, asante kwa ku-share but next time fanya kutoa credit to source “Tanzania Ya Magufuli: Serikali Yakacha Kutokea Mahakamani, Yadaiwa Dola Mil 60” @Chahali
 
Watakuwa wasariti wamepenyeza hyo habari kwa aduizetu, ciz tuko kwenye vita ya uchumi, na vita ya uchumi n mbaya.
 
Konoike si ni kampuni ya Japan ambao ni wadau wetu wa maendeleo katika ujenzi wa miundombinu?
 
SASA HAPA MNCHOSHABIKIA NI NINI?......Haya ndio kikundi cha kigaidi CHADEMA mnayoyafanya sasa kushikiza baadhi ya wadai wetu wafukue makabuli
HATUONGELEI SIASA ZA VYAMA HAPA, tunaangalia wasaliti wa kodi zetu tunazotoa kwa JASHO letu
 
haya madeni hatukuyasikia hapo awali au kuna watanzania wanamaslahi?
 
Back
Top Bottom