Serikali yajivunia kuwa na Asilimia 57 ya wanafunzi waliopata zero Kidato cha Nne 2012

Shafiri

Member
May 5, 2013
98
14
Katika hali isiyo ya kawaida, wabunge wengi wa CCM waliochangia hotuba ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wameoneshwa kufurahishwa na matokeo mapya yaliyotangazwa na Kawambwa baada ya yale ya awali kufutwa. Wanadai kuwa matokeo ya awali hayakuwa sahihi na ndiyo maana asilimia 65 ilionekana kuwa wamefeli. Sasa mambo yamekuwa mazuri maana waliofeli ni asilimia 57 ikilinganishwa na asilimia 43 waliofeli mwaka 2011. Kuongezeka kufeli kwa asilimia 10 ndani ya mwaka mmoja ni mafanikio au ni udhaifu?

Ama kweli siasa inaleta upofu, hivi kweli mtu anayejali nchi hii anaweza kufurahia hata haya matokeo yaliyotangazwa mara ya pili ambayo ni ya chini kuliko matokeo yoyote katika historia ya nchi hii

Div I 3,242 (0.87%)
Div II 10,112 (2.79%)
Div III 21,758 (5.8%)
Div IV 124,390 (33.54)
Div 0 211,090 (56.92)

Hongera sana serikali ya CCM kwa mafanikio makubwa katika elimu yanayoletwa na waziri wenu makini wa Elimu Shukuru Kawambwa
 
Ni aibu kama watu waliopewa dhamana wanafurahia huo upuuzi. Hivi wanaopata I-III hawatakiwi kuzidi asilimia 10? Wanyonge tutaendelea kunyongwa kwenye nchi yetu kama viongozi wanafurahia matokeo hayo mabovu
 
Wanaumwa hao, watoto wao wapo private

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom