Serikali yajipanga kufufua michezo ya jadi ili kuvutia watalii na vizazi vijavyo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Naibu waziri wa habari michezo utamaduni na sanaa Abdala Ulega amesema kuwa wizara yake ina mpango wa kufufua michezo ya jadi ili kuendeleza urithi wa utamaduni wa watanzania lakini pia kuwa kivutio kwa watalii wanaoitembelea nchi.

Ulega aliyasema hayo wakati akifunga bonanza la Arusha super cup ambapo alisema kuwa nia ya kufufua na kuipanguvu michezo ya jadi ni kuhakikisaha kwamba urithi wa utamaduni unaendelea kurithiwa na vizazi vijavyo.

Alisema michezo ya jadi itayofufuliwa ni pamoja na mchezo wa bao ambao bingwa wake alikuwa ni hayati mwalimu Julias Nyerere pamoja na michezo mingine mingi ambapo pia itakuwa ni kivutio cha utalii kwa watalii watakao ngia hapa nchini.

“Itakuwa ni kivutio kwani wageni wataweza kuangalia utamaduni wa makabila mbalimbali yaliyopo hapa nchini lakini pia namna ambavyo watanzania wanavyoishi kwa kwa ummoja, mshikamano na upendo na michezo yetu ambayo watakuja kuiona wakati wa matamasha na mabonanza kama haya,”Alisema Ulega.

Alifanua kuwa wana mipango ambayo itahakikisha wanafufua jadi za watanzania katika mambo ya michezo ambayo itawavutia watalii kuja kuona namna ambavyo utamaduni wa Tanazania ulivyo.

Aidha kwa upande wa bonanza la Arusha super cup waziri Ulega aliupongeza uongozi wa wilaya ya Arusha na kusema kuwa bonanza hilo linafaa kuwa mfano wa kuigwa na maeneo mengine kwa umekutanisha watu wengi na kuchezwa michezo zaidi ya 24 ikiwemo ya jadi pamoja na mechi ya mpira wa miguu kati ya mashabiki wa Simba na Yanga.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi ambaye ndio muuandaji wa bonanza hilo alisema kuwa lengo la bonanza hilo ni kuwaleta wananchi wa Arusha pamoja lakini pia kutambua na kuibua vipaji katika michezo mbalimbali .

“Kama mlivyoona katika michezo yote 24 kuna talanta ambayo imejificha kwa vijana na sisi kama viongozi wenye dhamana tuna wajibu wa kufanya mabonanza kama haya ili kuendeleza vipaji vinavyopatikana,” Alisema Kenan.

Naye mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt John Pima alisema kuwa bonanza hilo limewafanya wananchi wa Arusha kuwa pamoja na kwa asilimia kubwa linawanufaisha wao kiuchumi na kiafya na kutokana na hilo wanataka jiji hilo liwe la mfano kwa nchi nzima.

Hata hivyo washindi waliopatikana katika bonanza hilo walipewa zawadi mbalimbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi pamoja na medani huku wasanii wa bongo fleiva Billnas na Dogo Janja pamoja na wasanii wengine mbalimbali wa mkoa wa Arusha wakitoa burudani.
 
Back
Top Bottom