Serikali yajikomba na GEPF, yasaliti PPF, NSSF, kulikoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yajikomba na GEPF, yasaliti PPF, NSSF, kulikoni?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kagosaki, Oct 24, 2012.

 1. Kagosaki

  Kagosaki JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2010
  Messages: 208
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa nasikiliza matangazo ya GEPF kwamba unapomaliza tu mkataba wako unapewa kitita chako. Pia, wanauwezo wa kukukopesha asilimia 40 za pesa yako pindi unafanya kazi na kuendelea na Mkataba. Tukumbuke kwamba GEPF iko chini ya serikali (Govt Employees Pension Fund). Sasa sisi huku PPF na NSSF wanatubania kwamba tufike miaka 55 ndo tupate mafao yetu kama sheria ilivyo badilishwa kutokana na mapendekezo ya Mamlaka ya Mifko ya Jamii (SSRA). Swali langu ni kwamba, iweje sheria kandamizi itubaguwe sisi watu wa PPF na NSSF? Kwanini mfanyakazi wa serikali ambaye anaajiriwa kama "permanent and pensionable" awekewe mazingira rahisi namna hiyo wakati sisi tunaojulikana watu wa mikataba tuwekewe mizenge? Naomba ufafanuzi kwa anaejua hili tafadhari.
   
Loading...