Serikali yajiandaa kuilipa Dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yajiandaa kuilipa Dowans

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 4, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  Serikali yajiandaa kuilipa Dowans Monday, 03 January 2011 20:05

  Elizabeth Ernest na Hassan Mohamed
  SERIKALI imeanza mchakato wa kuilipa Kampuni ya Dowans, siku chache baada ya Mwanasheria wake Mkuu (AG), Jaji Frederick Werema, kusema ameridhika na hukumu dhidi ya kampuni hiyo na kuishauri Serikali kuubeba mzigo huo.

  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliliambia gazeti hili jana kuwa Serikali ipo katika mchakato wa kuufanyia kazi ushauri huo wa Jaji Werema na kwamba itatoa taarifa yake wakati wowote kuhusu suala hilo. Desemba 27 mwaka huu, Jaji Werema alisema Serikali imekubali kulipa fidia ya Sh 185 bilioni kwa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Ltd na hivyo kuufunga mjadala kuhusu suala hilo.

  “Mimi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali nimeisoma hukumu hiyo kwa makini na nimeridhika nayo kuwa iko sawa,” alisema Jaji Werema alipokuwa akizungumza na gazeti hili baada ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu mpya, Mohamed Othman Chande.

  Alisema “Kwa hukumu hii siwezi kusema tutalivalia njuga suala la Dowans maana kwa hukumu hii hata ukiivalia hiyo njuga itafikia mahala njuga hizo zitakatika tu,” alisisitiza Jaji Werema. “Watu wamezungumza sana, nendeni mkaisome muone ile Dowans ni ya nani na imesajiliwa wapi, maana watu walitaka kupotosha kidogo,” alisema Jaji Werema.

  Jana, Waziri Ngeleja alilieleza gazeti hili kuwa “Tayari tumemsikiliza Mwanasheria Mkuu na hatuna budi kuyafanyia kazi maagizo yake kuhusu suala hilo”.

  Lakini, alipotakiwa kuzungumzia taarifa za Serikali kuanza kuwekeza Sh50 bilioni katika benki moja nchini kwa ajili ya malipo hayo, Waziri Ngeleja alisema "Sina taarifa". “Sijawahi kusikia kabisa suala linalohusiana na mambo ya kufungua hiyo akaunti ndio kwanza nakusikia wewe, silijui hilo,”alisema.

  Ulipaji wa fidia hiyo unafuatia uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court), Novemba 15, mwaka huu chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen na wasuluhishi Swithin Munyantwali, Jonathan Parker uliamuru Tanesco iilipe Dowans kiasi hicho cha fedha.

  "Jopo la wasuluhishi limeamuru zaidi ya Sh36bilioni (dola za Marekani 24,168,343) na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka inayofikia kiasi cha zaidi ya Sh 26bilioni (dola za Marekani 19,995,626) tangu Juni 15, 2010 hadi fidia hiyo itakapolipwa,’ ilieleza sehemu ya uamuzi huo.

  Pia jopo hilo la wasuluhishi wa migogoro ya kibiashara liliamuru Sh60bilioni (sawa na dola za Kimarekani 39,935,765) na riba ya kiasi cha asilimia 7.5 ambayo ni sawa na Sh 55bilioni (dola za Marekani 36,705,013.94) zilipwe kuanzia Juni 15, 2010 hadi wakati wa malipo.

  Jopo hilo lilisisitiza kuwa ada na gharama za wasuluhishi na za utawala Sh1bilioni (dola za Marekani 750,000) kwa wasuluhishi wa ICC zinatakiwa zilipwe na pande zote husika yaani Tanesco na Dowans. "Tanesco wanatakiwa kumlipa mdai (mlalamikaji) Sh3bilioni (dola 1,708, 521) ikiwa ni gharama za uendeshaji wa kesi na gharama zingine na kwamba madai mengine yaliyotolewa na pande zote katika kesi hiyo yanatupwa.

  Awali baada ya uamuzi huo kufikiwa, Tanesco ilionyesha nia kwamba ingechukua hatua za kukata rufaa, lakini tangu Jaji Werema alipoweka wazi ushauri wake uongozi wa shirika haujawahi kutoa taarifa yoyote kuhusu msimamo wake.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  JK ni kiboko hizi safu za mafisadi alizozipa uongozi sasa zimeanza kazi ya kulipeleka taifa hili gizani kabisa.......................lakini watakapomaliza kulipora taifa hili mwishowe wataanza mikakati hata ya kutuuza sisi raia wanyonge utumwani..............

  Hili halina ubishi kwani Nyerere alituasa ya kuwa.........................Mtu akianza kula nyama ya mtu haatacha ataendela hivyo hivyo kula nyama ya mtu................................

  Na kwa mafisadi kila kukicha watabuni mbinu za kulipora taifa hili na maisha bora kwa kila Mtanzania ni njozi kwetu lakini kwao ni kipvuno cha leo.........................uzuri wa yote ni kuwa mwanadamu ni mavumbi atarudi mavumbini na yote haya ataayaacha ila shubiri ataikuta kwa Mwuumba wa vyote..........................hongera JK kwa kulipora taifa hili changa ili liendelee kubaki kwenye lindi la umasikini.............
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  bado hawajalipana tu?

  mbona wanachelewa?

  au kuna utata kwenye 'mgao'?
   
 4. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Huyo anaonekana akibanwa ni kigeugeu,

  Muulizeni werema kama alisema kama jaji Mkuu au yalikuwa maoni yake binafsi!

  Inanikumbusha wimbo wa Tax Bubu-Mchana plate number rangi ya njano na usiku nyeupe.:A S-coffee:
   
 5. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,991
  Likes Received: 3,740
  Trophy Points: 280
  Ruta ndugu yangu, haya yote yatakwisha nchi hii ikirudi kwa wenye nayo (wananchi).

  JK & co can do whatever they wish for now lakini pia wasisahau kuwa kuna siku itafika hata kwa kukimbilia hakutawepo....labda nao waje "kufa" kama Balali!!
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Sijawahi kuona nchi inang'ang'ania kulipa deni hata nchi tajiri kama Marekani ambayo ni mdaiwa namba moja duniani sijawahi kuona waking'ang'ania kulipa madeni kama Serikali inataka kuilipa Dowans sikatai kuna madeni yaliyopo nyuma kabla ya hilo la Dowans waanze kuwalipa hao wazee wastaafu wa jumuiya ya afrika mashariki walipe bili za maji na simu wanazodaiwa na Dawasco na TTCL walipe fidia wanazodaiwa na wananchi baada ya kuwahamisha kwenye viwanja vyao halafu baadae ndio waje wailipe Dowans hata ikipita miaka 50 mbona mkopo waliochukua kutoka Serikali ya Brazil enzi za Nyerere kujenga barabara ya Dar-Dodoma walikuwa hawajalipa mpaka Rais wa Brazil alipokuja kutembelea Tanzania ndio akasamehe deni leo hii ndio wanataka kujifanya wana haraka sana ya kuilipa Dowans obviously ndio maana Slaa aliposema Kikwete is part and parcel of Dowans siwezi kushangaa kabisa

  Ni upumbavu tu....
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  JK hawezi kuukwepa ukweli kuwa ana masilahi mazito ndani ya DOWANS.......na huu hapa ni ushahidi:-

  a) Uteuzi wa Dr. Idrissa Rashid kuiongoza Tanesco ulijaa mizengwe kibao..............Dr. Rashid mwenyewe alikiri kuwa pamoja na kuwa nafasi hiyo ilitangazwa magazeti yeye hakuiomba ila JK alimwomba amsaidie kwenye nafasi hiyo...........Hivyo pamoja na sheria ya Tanesco kuweka wazi kuwa Mtendaji Mkuu wa Tanesco atateuliwa na Bodi, JK aliingilia Bodi kinyume na sheria pale alipombandika swahiba wake pale Tanesco..........................Swali la kujiuliza JK alikuwa anatetea masilahi ya nani kwa kuiingilia Bodi ya Tanesco?

  b) Kwa vile Dr. Rashid hakuwa ameteuliwa na Bodi ya Tanesco hivyo na yeye hakuona sababu ya kuishirikisha Bodi tajwa katika utoaji wa zabuni ya uzalishaji wa umeme kwa Richmond na hata zabuni hiyo haikupitishwa kwa Bodi ya zabuni na matokeo yake kampuni kivuli ikapewa kazi hiyo..........Kulingana na rekodi zilizopo Brella, Richmond haijawahi kusajiliwa hapa nchini na hivyoufanyaji wake wa kazi ulikuwa ni batili na haikupaswa kupewa zabuni tajwa............Haya ni makosa ya kijinai yaani "criminal negligence" na JK anashindwa nini kumkabidhi swahiba wake Takukuru? Hapa inaonyesha kabisa hoja za Dr. Hosea kwa Wikileaks ni za kweli ya kuwa JK ndicho kikwazo kikuu cha utawala bora hapa nchini...............

  c) Baada ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme ikaikabidhi kazi hiyo kwa DOWANS ambao walitumia dola za kimarekani 7.5 milioni kununua mitambo hiyo ya kuzalisha umeme kazi ambayo ilikuwa ndani ya uwezo wa Tanesco.........................na hivyo hawakuhitaji mzabuni yeyote..........................

  d) Tanesco kwa matendo yao walimhalalisha Dowans kuwa mzabuni wa kumrithi Richmond bila ya kupata kibali cha Bodi ya zabuni....

  e) Baada ya mkataba kuisha Tanesco wakaishinikiza serikali kununua mitambo ya DOWANS kwa bei ambayo ilikuwa ni zaidi ya mara 20 ya bei ambayo Dowans walinunulia mitambo tajwa.......na ili kuishinikiza serikali kuinunua mitambo ya DOWANS, Tanesco wakaamua kuitumia Mahakama Kuu kwa kuwazuia Dowans wasiondoke na mitambo yao kwa amri ya Mahakama.....................bila sababu za kimsingi.........

  f) Kutokana na uvunjaji huo wa mkataba kwa kutumia visingizio vya kuwa Dowans hawajalipa kodi, Msuluhishi akaibandika Tanesco jumla ya Tshs 185 Bilioni ikiwa ni zaidi ya mara 18 ya gharama ambazo Dowans walinunulia ile mitambo...............

  g) Mwanasheria Mkuu ametoa ushauri Dowans walipwe huku uamuzi huo haujatoa sababu ni maeneo yapi Tanesco ilikuwa imekiuka huo mkataba kitendo ambacho kwa AG makini angeligangamala kuhakikisha analifungua shauri upya hapa Dar kupinga tuzo ambayo hata sababu za Tuzo hiyo hazifahamiki.........................Katika hukumu hiyo Msuluhishi aliahidi kutoa sababu lakini sababu hizo hakuzitoa sasa mdaiwa ataonaje kuwa katendewa haki? Hivi tuna AG au tunambabaishaji ambaye anadai ameipitia hiyo hukumu na ameona ipo beneti na tuilipe tu...............Hawa ndiyo wateule wa JK ambao kazi yao kuu ni kujenga mazingira ya kulipora taifa hili changa..........

  h) JK hayuko tayari kumfikisha mahakamani Dr. Idrissa Rashid kwa sababu alimpeleka pale Tanesco kwenda kulipora hilo shirika la umma na hasa ukizingatia ya kuwa JK alivunja sheria za tanesco kuhakikisha Dr. Rashid anakwenda pale tanesco kulifilisi shirika hilo na mzigo wa hasara hizo kutupiwa raia wanyonge ambao kosa letu ni kumvumilia JK ambaye hana sifa ya kuliongoza taifa hili masikini duniani........

  i) Haya ni mazingira yanaonyesha ya kuwa JK ni mshiriki kwenye mradi wa Dowans na hata kama jina lake halipo ila linawakilishwa na swahiba wake wa karibu Rostam Aziz kama ushahidi huu kwenye hukumu ya Dowans unavyothibitisha ambao tanesco wenyewe waliutumia ................................

  [​IMG]
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  Tusikate tamaa....................JK and his 40 thieves are not the Almighty God.....................
   
 9. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Yeah, kuna kitu hapa! Mbona hata madeni inayodaiwa na Tanesco ni shida kulipa, na as always wanasema serikali haina fedha, ila kwa hili, mmh, wansema lazima walipe. Hapana, kuna kitu ndani hatukijui express, but implied, watu wanadhani kuna kitu.
   
 10. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,230
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  ama kweli tunakaribia kuangamia...sijui kama 2015 tutafika tukiwa hai maana haya madudu yanayofanyika tunaweza kufa kwa presha...
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CCM ikijilipatu fedha za walipakodi kiujanja kwa kujificha nyuma ya Dowas basi wajue moja kwa moja ndio itakuwa ni tamko la kupewa TALAKA TOMEA na wapiga kura wa nchi hii.

  Waacheni CCM, sikio la kufa halisikii dawa.
   
 12. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Not at all kabisa Ruta
   
 13. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ruta .. Hata hawa Dowans sijui ilikuwaje wakanunua mitambo yao maana kuna kesi huko Texas kama ilivyolipotiwa hapa na Mwanakijiji na documents kumwagwa humu jamii forum jana kwamba Dowans anamshitaki Richmond kwa Richmond Kudai eti hizo gas turbines ni zake wakati sio...

  Naumwa kichwa kwa kufikiri iweje AG wetu na Tanesco Pia wasiombe kuwa interested parties kwenye kesi huko Texas ili mbivu na mbichi zijulikane maana kwenye moja ya mafaili kuna hii inayosema list any interested party, Dowans ha-list lakini Richmond kawataja Tanesco...

  Hebu soma hapa chini ujionee

  List the cases related to this one that are pending in any state or federal court with
  the case number and court, and state how they are related.​
  Dowans: None.
  RDEVCO: There are two, related matters pending in the International Court of
  Arbitration. One matter is between Dowans and the Tanzania Electric Supply Company Ltd.
  (“Tanesco”). The other matter is between RDEVCO and Tanesco. Both matters are related to
  the Agreement for the Emergency Supply of Power, Sale (the “PPA”), the Assignment and
  Assumption Agreement and Consent of Tanesco (the “Tanesco Agreement”), the Assignment
  and Assumption Agreement and Consent of Vulcan (the “Vulcan Agreement”; both shall be
  collectively referred to as the “Assignment Agreements”), and the Turbine at issue in this
  lawsuit. It is RDEVCO’s contention that the results of these arbitrations will substantially
  impact the matters to be considered by this Court and the jury. Accordingly, RDEVCO’s
  Proposed Docket Control Order reflects additional time necessary to complete discovery (and
  trial) in light of both highly anticipated decisions from the International Court of Arbitration.​
  3. Briefly describe what this case is about.​
  Dowans: This case involves a dispute as to the ownership of a mobile gas turbine.
  Dowans paid for and received the turbine. RDEVCO, however, has falsely claimed that it owns
  the turbine. RDEVCO’s false claims of ownership have interfered with Dowans’ ability to sell
  the turbine. Dowans asserts claims for declaratory judgment, breach of contract, slander of title,
  and conversion.
  RDEVCO: In June 2006, RDEVCO and Tanesco entered into the PPA whereby
  RDEVCO agreed to construct, install, commission, operate and maintain a gas-based electrical
  generating plant in the country of Tanzania. On October 14, 2006, RDEVCO and Dowans
  Holdings executed the Assignment Agreements whereby RDEVCO agreed to sell, assign and
  delegate to Dowans Holdings certain rights and obligations under the PPA, subject to the terms​
  Case 4:10-cv-01086 Document 11 Filed in TXSD on 07/26/10 Page 2 of 10​
  DM1\2270852.1 ​
  - 3 -
  and conditions of the Assignment Agreements. Pursuant to the Tanesco Agreement, Dowans
  engaged RDEVCO as a consultant “to assist in the transition of the work contemplated under the
  Power Purchase Agreement” and agreed to compensate RDEVCO $65,000.00 per month and
  reimburse its “reasonable expenses for such things as travel, lodging, meals or payments to thirdparty
  providers.” However, Dowans Holdings breached the Tanesco Agreement because it did
  not pay all reimbursable expenses as agreed. Further, Dowans Holdings breached the Tanesco
  Agreement because it (1) has not paid all of the agreed compensation on the agreed payment
  schedule; (2) improperly used the operating name “Richmond Development Company LLC 100
  mw Emergency Power Supply”; (3) unilaterally approached Tanesco without RDEVCO’s
  consent or approval in attempting to obtain Tanesco’s consent; and (4) failed to maintain
  information with respect to the Tanesco Agreement confidential by unauthorized disclosures to
  third parties, including but not limited to the Indian Ocean Newsletter and/or The Citizen.
  Additionally, Dowans is liable to RDEVCO for business disparagement because it used
  RDEVCO’s operating name to publish disparaging and false words about RDEVCO’s economic
  interests.

  4. Specify the allegation of federal jurisdiction.​
  This Court has diversity jurisdiction under 28 U.S.C. § 1332(a)(2) because this suit is
  between Dowans Holdings and DTL, both citizens of a foreign state, and RDEVCO, a citizen of
  Texas, and the amount in controversy exceeds $75,000, exclusive of interests and costs.​
  5. Name the parties who disagree with the plaintiff’s jurisdictional allegations and
  state their reasons.​
  None.​
  6. List anticipated additional parties that should be included, when they can be added,
  and by whom they are wanted.​
  Dowans: Dowans does not anticipate joining any additional parties at this time.
  RDEVCO: Tanesco is an potential party that may be added by RDEVCO.​
  7. List anticipated interventions.​
  The parties do not anticipate any interventions.​
  8. Describe class-action issues.​
  None.​
  9. State whether each party represents that it has made the initial disclosures required
  by Rule 26(a). If not, describe the arrangements that have been made to complete
  the disclosures.​
  The parties will make their initial disclosures on or before August 2, 2010.
   
 14. N

  Ndeusoho Member

  #14
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nchi inapongangania kulipa ina maana wapo watakaofaidika na hawataki kuchelewa kupata faida hiyo.
   
 15. N

  Ndeusoho Member

  #15
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  The problem with most of us Tanzanians is our generosity. We are generous even to those who are planning to kill us. We should not continue with this sheepish behavior. Let us realize that the 'elites' have their way of robing our wealth and they are not for us neither are they for the nations' interest. The problems we currently face have been caused by our present way of thinking. We can not solve our problems using the same way of thinking. In other words we can not move forward using the same people who have proved to be short-sighted and infected with ill motives. One thing we should not forget is that there is an end to everything under the sun. Do what is right and avoid what is wrong.
   
 16. N

  Ndeusoho Member

  #16
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wakati mwingine misimamo ya mashirika na makampuni hubadilishwa bila watu kujulishwa. Ukifanya surprise check utakuta kuna vimemo vyenye kubatilisha maamuzi au msimamo wa TANESCO. Usishangae nchi hii hata polisi anapofanya kazi nzuri ya kumfuatilia mhalifu akikaribia kumtia mbaroni anabadilishiwa kazi au anahamishwa. Nenda kituo cha Oysterbay uone jinsi kuna kesi nyingi ambazo wahalifu wake wanajulikana lakini hawakamatwi. Jiulize wale jamaa waliomnyang'anya mtu laptop wakakimbia na baadaye wakapata ajali na kukamatwa. Je unajua wako wapi? Wanaiba kama kawaida mitaani. Tatizo kubwa ni utashi wa wenye dhamana kuitumikia nchi kwa uaminifu kukosekana. Wakati tukilalamikia hili la watu kujipanga kujilipa kwa kusingizia wanailipa Dowans kuna mtoto wa kigogo mmojawapo kanunua Hotel ya Embassy. Je fedha kapata wapi?? Kama wizi ni haramu basi kwa Tanzania ni halali kwa sababu viongozi tulio nao hawana hofu ya Mungu.
   
 17. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Jamani hebu tujiulize, serikali inaingiaje kwenye mkataba baina ya Tanesco na Dowans.

  Ni suala lililo wazi kuwa mkataba batili ulikuwa kati ya Tanesco na Dowans, waliopelekena kwenye usuluhishi ni Tanesco na Dowans, iweje leo serikali iwe kimbelembele katika kulipa madai ambayo yenyewe haihusiki kabisa. Kwa nini serikali iwe na kiherehere cha kumfanya AG amshauri waziri wa Nishati kuwa kulipa ni lazima halafu inayolipa ni serikali?

  Waziri na AG wanaingiaje kwenye sakata hili?

  Serikali ieleze bayana uhusika wake katika hili.
   
Loading...