Serikali yajiandaa kueleza marejesho fedha za EPA

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Serikali yajiandaa kueleza marejesho fedha za EPA

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

SERIKALI itaweka hadharani kiwango cha fedha kilichorudishwa na kampuni zilizochota fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kupitia Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA), baada ya wiki mbili kuanzia sasa.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Mustafa Mkulo, alipozungumza na wakurugenzi watendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) waliopo nchini.

Wadau hao walikuwa wakizungumzia changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kwenye juhudi za kuleta maendeleo pamoja na matumizi ya fedha za misaada za IMF.

Mkulo alisema serikali itataja kiasi hicho na fedha pamoja na akaunti zao, lakini haitakuwa tayari kutaja majina ya watu hao kwa sababu ambazo hakuziweka bayana.

"Najua watu wana hamu ya kutaka kujua kiasi cha fedha kilichorejeshwa na kinachoendelea kurejeshwa, lakini kwa sasa ni mapema mno kufanya hivyo ila nina ahidi tutatangaza kiwango na akaunti namba baada ya wiki mbili zijazo kuanzia leo (jana)," alisema Mkulo.

Alisema serikali haina cha kuficha inapofika katika suala la ubadhirifu wa mali za umma na ndiyo maana wahisani na IMF wameridhika na hatua zilizochukuliwa dhidi ya watu waliohusika na upotevu wa fedha za wavuja jasho.

"Serikali tumekuwa wazi katika kushughulikia tuhuma mbalimbali na pia tumekuwa tukiwawajibisha watu wanaohusika na tuhuma hizo, ndiyo maana wenzetu hawa wa IMF wametuelewa na kutuunga mkono katika juhudi zetu za kupambana na watu wanaotumia vibaya rasilimali za nchi," alisema waziri huyo.

Naye Mkurugenzi wa IMF kutoka nchini Ufaransa, Jonathan Fried, alisema IMF imeridhishwa na hatua za serikali zilizochukuliwa dhidi ya watu wanaotumia vibaya rasilimali za nchi, hivyo kuchelewesha maendeleo ya taifa.

"Tumeridhishwa na Serikali ya Tanzania ilivyolishughulikia suala la EPA, na sisi tutaendelea kuisaidia, ili iweze kufikia malengo iliyojiwekea katika kujikwamua kiuchumi," alisema Fried.

Katika hatua nyingine, wadau mbalimbali nchini wameitaka IMF kufanya mapinduzi ya sera zake, ili kuweka masharti ya misaada kwa nchi maskini kulingana na uwezo wa nchi hizo badala ya kuweka masharti ya jumla kwa nchi zote.

Profesa Hamphery Moshi, wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema masharti yasiyozingatia uwezo wa nchi kwa kiasi kikubwa yamechangia nchi zenye uchumi mdogo kutoendelea kiuchumi.

"Kuna haja kwa nyinyi wataalamu wa IMF kufanya mapinduzi katika sera zenu, ili masharti ya misaada yaendane na uwezo wa nchi, tofauti na ilivyo sasa ambapo masharti yote ni sawa," alisema Profesa Moshi.

Hussein Kamoto, kutoka Shirikisho la Wafanyabiashara wenye Viwanda Tanzania (CTI), alisema kutokuwapo kwa miundombinu imara na kupanda kwa bei ya umeme kila mara ni miongoni mwa sababu zinazochangia Tanzania kutopiga kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa muda uliokusudiwa.

Alisema gharama za uzalishaji wa hapa nchini zimekuwa juu kutokana na matatizo hayo, hivyo ni vema wataalamu hao wa IMF wakaangalia zaidi maeneo hayo, ili kuweza kuisaidia Tanzania.

"Uchumi wetu hauwezi kuendelea katika mazingira haya tuliyonayo ya gharama kubwa za umeme pamoja na miundombinu mibovu, hivyo ni jukumu lenu nyinyi wataalamu kumshauri mkuu wenu atusaidie kulingana na hali ya mambo mlivyoiona," alisema Kamoto.

Naye Ali Mufuruki, alisema Tanzania ielekee katika kujitegemea zaidi badala ya kutegemea misaada ya IMF na wahisani wengine, ambayo wakati mwingine ina masharti magumu na yasiyoendana na matakwa ya nchi.

Profesa Idris Kikula, Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma, alisema ili Tanzania iweze kuwa na dira nzuri ya kuelekea katika maendeleo ni lazima iongeze idadi ya kudahili wanafunzi wa elimu ya juu.

Alisema Tanzania inadahili wanafunzi wachache zaidi katika ukanda wa Afrika, hivyo ni vema juhudi za makusudi zikatumika kuboresha sekta ya elimu ili nchi iweze kuwa na wataalamu wa kutosha watakaokuwa na uwezo wa kupanga mipango itakayoliwezesha taifa kujitegemea.

Wataalamu wa IMF wapo nchini kujadiliana na wadau mbalimbali kuangalia ni maeneo gani yapewe kipaumbele katika misaada inayotolewa na shirika hilo nchini.

Mbali na waatalamu hao kuwapo hapa nchini, pia mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo anatarajia kuwasili nchini leo, kwa lengo la kuangalia namna ya kuongeza misaada kwa Tanzania na maeneo ya kuyapa kipaumbele.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Miundombinu, Adrew Chenge, Gavana wa BoT, Professa Beno Ndullu na maofisa mbalimbali wa serikali.
 
Halafu nikitowa pongezi kwa JK kwa uongozi wake mzuri, kuna baadhi ya watu humu hawalipendi hilo.

JK kazi yako njema tunaiona na hata IMF wanakiri kuwa ni kazi nzuri, wale wasiyoona na wabaki hivyo hivyo hawaoni.
 
Did you just say IMF?! approval ya IMF ndiyo kitu cha kupongeza hapa? ama kweli siku imeanza mapema hapa!
 
Serikali yajiandaa kueleza marejesho fedha za EPA

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

SERIKALI itaweka hadharani kiwango cha fedha kilichorudishwa na kampuni zilizochota fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kupitia Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA), baada ya wiki mbili kuanzia sasa.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Mustafa Mkulo, alipozungumza na wakurugenzi watendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) waliopo nchini.

Wadau hao walikuwa wakizungumzia changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kwenye juhudi za kuleta maendeleo pamoja na matumizi ya fedha za misaada za IMF.

Mkulo alisema serikali itataja kiasi hicho na fedha pamoja na akaunti zao, lakini haitakuwa tayari kutaja majina ya watu hao kwa sababu ambazo hakuziweka bayana.

“Najua watu wana hamu ya kutaka kujua kiasi cha fedha kilichorejeshwa na kinachoendelea kurejeshwa, lakini kwa sasa ni mapema mno kufanya hivyo ila nina ahidi tutatangaza kiwango na akaunti namba baada ya wiki mbili zijazo kuanzia leo (jana),” alisema Mkulo.

Alisema serikali haina cha kuficha inapofika katika suala la ubadhirifu wa mali za umma na ndiyo maana wahisani na IMF wameridhika na hatua zilizochukuliwa dhidi ya watu waliohusika na upotevu wa fedha za wavuja jasho.

“Serikali tumekuwa wazi katika kushughulikia tuhuma mbalimbali na pia tumekuwa tukiwawajibisha watu wanaohusika na tuhuma hizo, ndiyo maana wenzetu hawa wa IMF wametuelewa na kutuunga mkono katika juhudi zetu za kupambana na watu wanaotumia vibaya rasilimali za nchi,” alisema waziri huyo.

Naye Mkurugenzi wa IMF kutoka nchini Ufaransa, Jonathan Fried, alisema IMF imeridhishwa na hatua za serikali zilizochukuliwa dhidi ya watu wanaotumia vibaya rasilimali za nchi, hivyo kuchelewesha maendeleo ya taifa.

“Tumeridhishwa na Serikali ya Tanzania ilivyolishughulikia suala la EPA, na sisi tutaendelea kuisaidia, ili iweze kufikia malengo iliyojiwekea katika kujikwamua kiuchumi,” alisema Fried.

Katika hatua nyingine, wadau mbalimbali nchini wameitaka IMF kufanya mapinduzi ya sera zake, ili kuweka masharti ya misaada kwa nchi maskini kulingana na uwezo wa nchi hizo badala ya kuweka masharti ya jumla kwa nchi zote.

Profesa Hamphery Moshi, wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema masharti yasiyozingatia uwezo wa nchi kwa kiasi kikubwa yamechangia nchi zenye uchumi mdogo kutoendelea kiuchumi.

“Kuna haja kwa nyinyi wataalamu wa IMF kufanya mapinduzi katika sera zenu, ili masharti ya misaada yaendane na uwezo wa nchi, tofauti na ilivyo sasa ambapo masharti yote ni sawa,” alisema Profesa Moshi.

Hussein Kamoto, kutoka Shirikisho la Wafanyabiashara wenye Viwanda Tanzania (CTI), alisema kutokuwapo kwa miundombinu imara na kupanda kwa bei ya umeme kila mara ni miongoni mwa sababu zinazochangia Tanzania kutopiga kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa muda uliokusudiwa.

Alisema gharama za uzalishaji wa hapa nchini zimekuwa juu kutokana na matatizo hayo, hivyo ni vema wataalamu hao wa IMF wakaangalia zaidi maeneo hayo, ili kuweza kuisaidia Tanzania.

“Uchumi wetu hauwezi kuendelea katika mazingira haya tuliyonayo ya gharama kubwa za umeme pamoja na miundombinu mibovu, hivyo ni jukumu lenu nyinyi wataalamu kumshauri mkuu wenu atusaidie kulingana na hali ya mambo mlivyoiona,” alisema Kamoto.

Naye Ali Mufuruki, alisema Tanzania ielekee katika kujitegemea zaidi badala ya kutegemea misaada ya IMF na wahisani wengine, ambayo wakati mwingine ina masharti magumu na yasiyoendana na matakwa ya nchi.

Profesa Idris Kikula, Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma, alisema ili Tanzania iweze kuwa na dira nzuri ya kuelekea katika maendeleo ni lazima iongeze idadi ya kudahili wanafunzi wa elimu ya juu.

Alisema Tanzania inadahili wanafunzi wachache zaidi katika ukanda wa Afrika, hivyo ni vema juhudi za makusudi zikatumika kuboresha sekta ya elimu ili nchi iweze kuwa na wataalamu wa kutosha watakaokuwa na uwezo wa kupanga mipango itakayoliwezesha taifa kujitegemea.

Wataalamu wa IMF wapo nchini kujadiliana na wadau mbalimbali kuangalia ni maeneo gani yapewe kipaumbele katika misaada inayotolewa na shirika hilo nchini.

Mbali na waatalamu hao kuwapo hapa nchini, pia mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo anatarajia kuwasili nchini leo, kwa lengo la kuangalia namna ya kuongeza misaada kwa Tanzania na maeneo ya kuyapa kipaumbele.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Miundombinu, Adrew Chenge, Gavana wa BoT, Professa Beno Ndullu na maofisa mbalimbali wa serikali.

Mmekuwa wazi mbona mnashindwa kutaja majina ya wakopaji .Maana kutoa account numbers zao may lead to find their names.What is the use kama hamna msamaha ?Longo longo tu hapa sijaona ukweli na siamini kama wanarudisha pesa hizo kweli .
 
Halafu nikitowa pongezi kwa JK kwa uongozi wake mzuri, kuna baadhi ya watu humu hawalipendi hilo.

JK kazi yako njema tunaiona na hata IMF wanakiri kuwa ni kazi nzuri, wale wasiyoona na wabaki hivyo hivyo hawaoni.

Tunaompa pongezi JK hapa JF pale anapofanya mazuri tuko wengi, hebu pitia threads za nyuma kuna ushahidi belele, siyo wewe pekee yako unayeifanya hivyo.
 
Halafu nikitowa pongezi kwa JK kwa uongozi wake mzuri, kuna baadhi ya watu humu hawalipendi hilo.

JK kazi yako njema tunaiona na hata IMF wanakiri kuwa ni kazi nzuri, wale wasiyoona na wabaki hivyo hivyo hawaoni.

Kutoka hapo ulipo kaa na juu ya hicho ulichosimamia umeridhika.
Kuridhika kwako pengine ni kwa sababu ambazo ziko nje ya yote yanayoendelea. Inawezekana pia uliridhika pale uliposikia BOT kumetokea wizi. Zaidi inawezekana hukusikia kabisa kwamba BOT kumetokea wizi kwa sababu ulikuwa katika ya duara la ndani kule mambo ya wanyonge yasiko sikika.

Sisi haturidhiki kwa sababu tunajua mambo yote yanayoendelea juu ya uridishaji wa Fedha zilizo ibiwa BOT ni kinyume cha sheria za jamhuri ya Muungano wa Tanzaia.

Ona hata lugha wanayotumia kuuelezea wizi, eti Waliochota fedha BOT waanza kuzirudisha.

Kuiba siku hizi ni kuchota??

Hivi nikisema Kibaka wa Manzese kachota pochi yenye fedha kutoka kwenye mfuko wa abiria wa Dala dala, kiswahili hicho kinakubalika kisheria?

Kibaka wa Manzese arudisha Pochi yenye fedha aliyoichota kutoka kwenye mfuko wa suruali ya abiria wa dala dala, hatua hiyo imepongezwa na Mkuu wa wilaya ya kinondoni kwamba ni hatua moja kubwa ya maendeleo juu ya tabia ya uchotaji wa fedha wa vibaka hao.

Nisaidieni jamani labda ni mimi tu nisiye elewa kwa sababu ya kukokotoa sana hesabu za integration.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom