Serikali yajenga masoko ya kisasa Jiji Mwanza, Ilemela, sasa ile kero ya machinga kuzagaa mtaani imekwisha

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Serikali yajenga masoko ya kisasa Jiji Mwanza, Ilemela, sasa ile kero ya machinga kuzagaa mtaani imekwisha

Serikali ya Tanzania kwa Shirikiana na Shirika la Misaada la nchini Uingereza (DFID) wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha uboreshaji wa miundombinu ya kisasa katika masoko ya wafanyabiashara wadogo mkoani Mwanza ili kuwezesha mazingira ya masoko hayo yanakuwa rafiki.

Masoko hayo ni Mirongo katika wilaya ya yamagana na Kiloleli wilaya ya Ilemela ambayo yanafanyiwa maboresho ili kusaidia wafanyabiashara kuwa na mazingira rafiki ya kufanyia shughuli zao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika soko la Kiloleli, Mkurugenzi wa Shirika la kutetea Haki za Wanawake na Watoto la Kivulini,Yassin Ally amesema ukarabati wa masoko hayo pamoja na ujenzi wa vyoo, vyumba vya kunyonyeshea utagharimu kiasi cha Tsh. milioni 256.

Ally alisema kuwa, kati ya asilimia 70 - 80 ya wajasiliamali wengi katika masoko hayo mawili ni wanawake ambapo wengi wamekuwa wakipata hasara ya bidhaa zao hususani ni wauzaji wa ndizi kutokana na mazingira mabovu ya masoko hayo.

Amesema wafanyabiashara hao wamekuwa wakipata hasara kwa siku ya Tsh. 10000 katika kipindi mvua kwa kuwa ndizi hao huingiliwa na ugonjwa wa kimeta na kwamba hasara hiyo huwafanya wasipige hatua ya kujikwamua kiuchumi.

"Changamoto nyingine tuliobaini ni miundombinu mibovu ya vyoo hasa kwa walemavu na wanawake wanaonyonyesha kwa kuwa katika masoko hayo hakuna miundombinu rafiki inayoangalia wanawake walemavu na wanaonyonyesha.

"Pia tumebaini kwenye masoko mengi kuna unyanyasaji wa kijinsia iwe anapotoa mzigo iwe anapokuwa sokoni na kingine uendeshaji wa masoko kiholela hayavutii wateja na kuwafanya hawawezi kuwaongezea kipato," amesema Ally.


"Kutokana na changamoto hizo sasa wenzetu wa IFID, DFID , Kivulini na ubalozi wa Irelanda, wametoa pesa hizi ambazo ni za kwanza zinaenda kujenga masoko ya kisasa na rafiki kwa wafanyabiashara wadogo," amesema Ally.


Ally amesema katika masoko hayo wanaenda kuboresha masoko hayo ambayo yatakuwa na sehemu ya kunyonyeshea, kucheza watoto, kujenga vyoo vya walemavu na watoto.

Hata hivyo, amesema pamoja na hivyo, wanaenda kujenga stendi kubwa na ya kisasa katika eneo hilo la kiloleli ili kuwasaidia wajasiliamali na watu waliokuwa wakitumia gharama kubwa kufika sokoni hapo (Kiloleli).

Katika masoko hayo mawili, yatakuwa na uwezo wa kubeba wajasiliamali 1200 (Kiloleli 620) (Mirongo 620) kwa kuwa ukubwa wa masoko yote mawili yana ukubwa unaofafanana.

Mwenyekiti wa soko la Kiloleli wilaya ya Ilemela mkoani humo, John Simfukwe amesema uboreshaji wa soko hilo umeleta tija kwao kwa kuondoa adha ya kunyeshewa na mvua.

Simfukwe pia akamuomba Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleman Jaffo, kuisaidia halmashauri ya Ilemela kuhakikisha wanatenga bajeti itakayosaidia kukamilisha na kuboresha zaidi soko hilo ambalo ni miongoni mwa masoko yenye wajasiliamali wengi mkoa wa Mwanza.

Baadhi ya wajasiliamali hao, Flaviana Jastin, Rukia Mohamed, Herieth Hezron na Gilbat Nganzi katika masoko hayo, wamesema awali walikuwa wakifanya biashara katika mazingira magumu huku wakieleza kukamilika kwa ujenzi wa masoko hayo utasaidia kuondokana na changamoto zilizokuwa zikiwakabili.


Mwisho
 

Attachments

  • IMG20200409091147.jpg
    IMG20200409091147.jpg
    130.1 KB · Views: 1
  • IMG20200409091149.jpg
    IMG20200409091149.jpg
    191 KB · Views: 1
  • IMG20200409091354.jpg
    IMG20200409091354.jpg
    130.1 KB · Views: 1
  • IMG20200409094111.jpg
    IMG20200409094111.jpg
    129.8 KB · Views: 1
  • IMG20200409092019.jpg
    IMG20200409092019.jpg
    152.2 KB · Views: 1
  • IMG20200409091158.jpg
    IMG20200409091158.jpg
    207.2 KB · Views: 1
Kwa hiyo tunaona fahari kufadhiliwa msaada wa ml.256,000,000/ V8 moja inathamani ya sh.ngapi?vitu vingine tusiwe tunashabikia kuviandika, kwani tunajidhalilisha wenyewe,hawakawii kusema unahujumu uchumi au kwa vile umewapongeza na kuwasifia?
 
Kwa hiyo tunaona fahari kufadhiliwa msaada wa ml.256,000,000/ V8 moja inathamani ya sh.ngapi?vitu vingine tusiwe tunashabikia kuviandika, kwani tunajidhalilisha wenyewe,hawakawii kusema unahujumu uchumi au kwa vile umewapongeza na kuwasifia?
Sasa V8 na soko wapi na wapi sheikh?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom