Serikali yaja na mbinu mbadala ya kuwatambua Madaktari Bingwa, wote wenye uzoefu wa muda mrefu kuwa Madaktari Bingwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
46,921
122,188
KUWATAMBUA MADAKTARI BINGWA

Mhariri 12/07/2019: Maoni

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile ametangaza mpango wa kuwatambua madaktari wenye uzoefu wa muda mrefu kama mabingwa.

Amesema wamebuni mpango huo kuongeza idadi ya madaktari bingwa walio katika hospitali mbalimbali nchini, hususani za mikoa na wilaya.
Katika mpango huo, wizara imeamua kuandaa utaratibu wa madaktari wenye uwezo mkubwa na uzoefu wa muda mrefu, kufanya mitihani maalumu ya kuthibitisha viwango vyao vya ujuzi.

Alisema, mpango huo utafanana na upimaji ujuzi wa wataalamu wa fani ya uhasibu ambao hufanya mitihani ya shahada za umahiri (CPA).

Tumeguswa na hatua hii ya wizara kuongeza wigo wa madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali nchini kupitia mfumo mbadala.

Kwa muda mrefu, madaktari bingwa wamekuwa wakitokana na wanaoenda kusomea shahada za juu za uzamili (Msc) na uzamivu (PhD) katika umahiri wa fani ambayo wamekuwa wakitibia.

Kutokana na mfumo huo, imekuwa vigumu kupata wataalamu wengi waliobobea wa kuweza kuwa madaktari bingwa kwa kuwa ni wachache wanaopata ufadhili kusomea umahiri wa fani.

Ndio maana tunasema, hatua hii ya wizara kuja na mfumo mbadala wa kuwatambua madaktari wenye uwezo, ujuzi na uzoefu wa muda mrefu lakini hawajaweza kuongeza vyeti darasani ni nzuri na itachochea ufanisi wa madaktari wengi.

Tanzania imejaliwa madaktari wengi wenye uwezo mkubwa kutokana na kupata mafunzo mazuri kwenye vyuo vikuu vya tiba na afya vya Muhimbili (Muhas), Bugando, KCMC na taasisi nyingine za afya zinazotoa mafunzo ya uganga.

Ni katika muktadha huo, tunasema tunaunga mkono hatua hii ya wizara kuwatambua na pia kuwapandisha madaraja na kuboresha maslahi yao, madaktari itakaowatambua kimfumo huu.

Hii itakuwa motisha kubwa kwa madaktari wengi ambao hawajabahatika kuwa mabingwa lakini wamekuwa wakifanya kama za kibingwa.

Ni vyema basi madaktari wenye uwezo, ujuzi na uzoefu huo mkubwa lakini hawajatambuliwa wakajiandaa kufanya mitihani ya umahiri ili nao sasa watambuliwe rasmi pale watakapofaulu.

Hatua hii itasaidia kuongeza idadi ya madaktari wanaotambuliwa kama madaktari bingwa na pia motisha kwa ambao wamekuwa wakitumika bila kutambuliwa hivyo na kuboresha huduma.

Tunaungana na wananchi kuipongeza wizara na serikali kwa jumla kwa kubuni mfumo huu na kutumaini kwamba utapokewa vyema na wote.

Hongera wizara kutambua madaktari bingwa.
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

C&P
 
Gazet gani wameriport
 
wanikumbuke na mimi
 
Waziri anatakiwa ajue Medicine haina shortcut na pia haifungamani na Siasa za afya japokuwa yeye ni Daktari Bingwa.

Wawape motisha madaktari wakasome na sio kugawa “Ubingwa” kwa kisingizio cha uzoefu.

Kusoma MMed kunahitaji umakini na kujitoa kwa hali ya juu na sio kutaka sifa mbele ya wapiga kura kama wafanyavyo wanasiasa.

Kwa muktadha huu basi CO nao watunukiwe MD baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu na kupimwa na hiyo mitihani.
 
Kama tunao Uhaba wa Madaktari Bingwa hivi Serikali imeshindwa kujitolea kuwasomesha Madaktari kwa ajili ya kuziba huo upungufu ?.

Uzoefu wa Muda mrefu unamfanyaje Daktari wa level flani kuwa Bingwa ?.

Ni kwa nini tuache Mfumo wa mwanzo unao wachuja na kuwa Bingwa ?.

Kwa style hiyo tutakuwa tume ondoa tatizo au ndio tutapasuliwa Kichwa badala ya Mguu ?.
 
Mimi ndio kilaza ama nini ,kwanini wasipunguze ada watu wakaenda kusoma?(mfano ada ya kusomea Gynaecology ni milion 7 Muhimbili) kwanini wasipewe udhamini wa bure wapige shule?wanasiasa wa Tanzania wanatuua kwa kupenda matokeo ya haraka ,no wonder Taifa stars waliifananisha na Brazil
 
Maamuzi ya serikali ndo yana gharim sana madaktari mtu ameenda kusoma mastaa ya gynacology kwa mika 3 anarudi kituo chake cha kazi kwamiaka zaidi ya 3 hamna recategorization mtu anaamua kuacha kazi na kwenda kufanya private
 
Kwanini hamkushangaa pale Hospitali za kila mkoa zilipoitwa za rufaa wakati hazina dawa, vifaa muhimu, madaktari Bingwa na hata wakawaida hawatoshi na kudhibitisha hilo nenda pale Muhimbili ujionee referals kutoka mikoa yote ya Tanzania ndipo utakapojua siasa ninini...ajabu tena leo hii wanaleta kituko cha kukaa mezani na kupiga kura nani awe Daktari bingwa? hao madaktari wa aina hiyo wana tofauti gani na wafanyakazi hewa waliokuwa wanafanya kazi bila kuwa na vyeti halali pamoja na kwamba wengine walikuwa wana perform vizuri na hawakupata scandal yoyote ya taaluma zao, hebu tuangalie nyuma kuhusu ule uteuzi/upendeleo uliosemwa sana wa wale majaji wasioweza hata kuandika hukumu lakini wakapewa ujaji? kweli bado hatujajifunza kitu?
 
Maamuzi ya serikali ndo yana gharim sana madaktari mtu ameenda kusoma mastaa ya gynacology kwa mika 3 anarudi kituo chake cha kazi kwamiaka zaidi ya 3 hamna recategorization mtu anaamua kuacha kazi na kwenda kufanya private
Bonge moja la point mzee. Zamani ilikuwa waliotoka kufanya MD kutokea CO wanakimbia sana enzi hizo MD ipo kwenye kilele.

Ila kwa sasa kama ulivyosema MMed wanakimbia mno. Ukiondoa recategorization, hata maslahi pia ni madogo ukilinganisha na Private ambapo MMed anaweza vuta hata 5M
 
Ndio maana tunasema, hatua hii ya wizara kuja na mfumo mbadala wa kuwatambua madaktari wenye uwezo, ujuzi na uzoefu wa muda mrefu lakini hawajaweza kuongeza vyeti darasani ni nzuri na itachochea ufanisi wa madaktari wengi

Kwahiyo suala hapa ni kuwa na madaktari wengi na siyo kuatazama utaratibu wa kuwapata kwa kufuata utaratibu wa kimataifa
 
Fani ya afya imevamiwa awamu hii. Walianza na kushusha vigezo vya kusomea uuguuzi, sasa wamekuja kwenye udaktari bingwa

Yote haya yanafanyika chini ya naibu waziri ambaye ni daktari bingwa. Ama kweli kikulacho kinguoni mwako
 
Kama tunao Uhaba wa Madaktari Bingwa hivi Serikali imeshindwa kujitolea kuwasomesha Madaktari kwa ajili ya kuziba huo upungufu ?.

Uzoefu wa Muda mrefu unamfanyaje Daktari wa level flani kuwa Bingwa ?.

Ni kwa nini tuache Mfumo wa mwanzo unao wachuja na kuwa Bingwa ?.

Kwa style hiyo tutakuwa tume ondoa tatizo au ndio tutapasuliwa Kichwa badala ya Mguu ?.
Inasikitisha....
 
Back
Top Bottom