Serikali yaja na mbinu mbadala ya kuwatambua Madaktari Bingwa, wote wenye uzoefu wa muda mrefu kuwa Madaktari Bingwa

Wanaiita njia mbadala...

Wakumbuke kiwa huu uzoefu waouzungumzia ni ule wa level husika tu(Kama ni CO, utabaki uzoefu huo tu na hautaweza kuwa MD hata kama uwe na uzoefu wa muda gani), kwa mantiki hiyo huwezi kuwa bingwa maana haujasoma zaidi ya level hiyo...

Madaktari bingwa wanasotea taalamu zaidi ya walizonazo za wali, na wanasoma kwa deep sana(wana specialize), ila leo hii anatokea mtu anasema jambo liwe hivi bila kuangalia undani wake, mwishowe athari ya maamuzi hayo yatakuwa hadi kwa kiasi kikubwa.

Siasa isiingizwe kwenye masuala nyeti ya kitaaluma/kitaalamu kama suala la Afya.



Wamevuruga elimu ya Tanzania kwa kupeleka failures kusomea ualimu sasa leo wanahamia kwa madaktari sijui kesho itakuwa kwa uhasibu na uhandisi!!!
 
Sidhani hata hapo Burundi wanaweza tambua huo udaktari bingwa, take simple logic ni kwamba ni rahisi kueleweka pale unapomchukua Captain wa jeshi na ukamzawadia u DC au akatunikiwa u RC, ubunge or uwaziri lakini huwezi kueleweka Kama utampatia u major general jeshini bila kupitia mafunzo stahiki yanayohalalisha cheo hicho, dunia mzima Ina taratibu za kuongoza taaluma na hazinaga siasa Kama tunavyotaka kufanya



Nina mashaka yawezekana hata vifaa vinavyowekwa mahospitalini pamoja na madawa navyo vimepitia michakato ya namna hii kwasababu tu lengo ni kuonekana vipo bila kujali kama vinakidhi viwango
 
Walifanya hivihivi kwenye Elimu... Walichagua wenye division IV hadi ya D 2 na kuwapeleka kusomea ualimu wa shule za msingi. Leo wanafunzi Wanamaliza drs la saba lakini wanasoma kwa tabu au hawajui kabisa kusoma,utashangaa wanawasomba wote na wanawaingiza secondary (form I) halafu wanatarajia shule za kata zitoe matokeo mazuri. Siasa za Tanzania ni kwikwi


Mkuu is as if we tulikuwa pamoja, nimecomment the same thing kabla sijasoma post yako, ipo haja waache kabisa huu upumbavu wao
 
Kwa nini niende kufanya Mmed nije kulipwa TGHS G ya 2.1M wakati nikikaa na hiyo hiyo MD na kukomaa na NGOs za HIV wananitoa 3.5M na marupurupu kibao?


Kwa nini nifanye Mmed then niende katavi kulipwa 2.1M ( na yenyewe baada ya kusubiri 3 years since nimalize shule ndio wanaongeza na ambazo wamekupunja for those years hawarefund) badala ya kubaki Muhimbili ambapo walau ni 3.5 M na wanabadili Haraka + vijiwe vya kumwaga?.

Kwa nini nifanye Mmed 3/ 4 years kwa mateso bila udhamini wa maana/ kama uko na wa government unacheleweshwa malipo balaaa badala ya MPH mwaka mmoja then nirudi kazini kuipata vyeo vya uDMO na uRMO na ukurugenzi mbali mbali wizarani?.

Kwa nini hospital za Mission za pembezoni na mashirika mengine huko vijijini wana mabingwa wa kutosha ila hospital za mikoa hazina?.

Kwa nini ni rahisi Dr. Bingwa wa Serikali anakubali kushikizwa hospital za Mission za vijijini ila anakataa za serikali za mikoani?.

Wazoefu kwenye nini? Wamekaa department husika muda gani? Wakiwa wanafanya nini? Wakisimamiwa na nani?.

Kwamba wizara imeona wanaoenda kufanya Mmed baada ya uzoefu wa muda mrefu wanafaulu sana?.

Tujaze idadi kumfurahisha nani?. TCU wamelikubali hili?.

Nilifikiri wanaleta mitihani ya kumantain certificate za kupractice sio huu ujinga wanaopendekeza.

Aliyetoa wazo hilo ni muhujumu uchumi - kupitia kuvuruga afya zetu. Achunguzwe.



You are a brain
 
nonsense kabisa,wasiopewa huo ubingwa si utawaondolea confidence?



Ukiona haya ujue kuna mtoto wa kigogo anataka kupenyezwa kwenye ubingwa, halafu baada ya muda wanakuja na mameno tulifanya makosa tumeamua kusahihisha, ni kama yale ya vyuo vya waalimu wengine wanasoma miaka miwili wengine mitatu wengine vyuo vikuu wakiitwa vilaza na mifumo mingine vurugu tupu!!!
 
Huyo waziri aanzishe hospitali zake na azifanyie huo upumbavu awaache madaktari wetu waendelee kwa utaratibu wa kimataifa
 
Kwanini hamkushangaa pale Hospitali za kila mkoa zilipoitwa za rufaa wakati hazina dawa, vifaa muhimu, madaktari Bingwa na hata wakawaida hawatoshi na kudhibitisha hilo nenda pale Muhimbili ujionee referals kutoka mikoa yote ya Tanzania ndipo utakapojua siasa ninini...ajabu tena leo hii wanaleta kituko cha kukaa mezani na kupiga kura nani awe Daktari bingwa? hao madaktari wa aina hiyo wana tofauti gani na wafanyakazi hewa waliokuwa wanafanya kazi bila kuwa na vyeti halali pamoja na kwamba wengine walikuwa wana perform vizuri na hawakupata scandal yoyote ya taaluma zao, hebu tuangalie nyuma kuhusu ule uteuzi/upendeleo uliosemwa sana wa wale majaji wasioweza hata kuandika hukumu lakini wakapewa ujaji? kweli bado hatujajifunza kitu?

Hakuna jambo gumu mbele ya siasa.
 
Back
Top Bottom