Serikali yaja na mbinu mbadala ya kuwatambua Madaktari Bingwa, wote wenye uzoefu wa muda mrefu kuwa Madaktari Bingwa

Kwa nini niende kufanya Mmed nije kulipwa TGHS G ya 2.1M wakati nikikaa na hiyo hiyo MD na kukomaa na NGOs za HIV wananitoa 3.5M na marupurupu kibao?

Kwa nini nifanye Mmed then niende katavi kulipwa 2.1M ( na yenyewe baada ya kusubiri 3 years since nimalize shule ndio wanaongeza na ambazo wamekupunja for those years hawarefund) badala ya kubaki Muhimbili ambapo walau ni 3.5 M na wanabadili Haraka + vijiwe vya kumwaga?.

Kwa nini nifanye Mmed 3/ 4 years kwa mateso bila udhamini wa maana/ kama uko na wa government unacheleweshwa malipo balaaa badala ya MPH mwaka mmoja then nirudi kazini kuipata vyeo vya uDMO na uRMO na ukurugenzi mbali mbali wizarani?.

Kwa nini hospital za Mission za pembezoni na mashirika mengine huko vijijini wana mabingwa wa kutosha ila hospital za mikoa hazina?.

Kwa nini ni rahisi Dr. Bingwa wa Serikali anakubali kushikizwa hospital za Mission za vijijini ila anakataa za serikali za mikoani?.

Wazoefu kwenye nini? Wamekaa department husika muda gani? Wakiwa wanafanya nini? Wakisimamiwa na nani?.

Kwamba wizara imeona wanaoenda kufanya Mmed baada ya uzoefu wa muda mrefu wanafaulu sana?.

Tujaze idadi kumfurahisha nani?. TCU wamelikubali hili?.

Nilifikiri wanaleta mitihani ya kumantain certificate za kupractice sio huu ujinga wanaopendekeza.

Aliyetoa wazo hilo ni muhujumu uchumi - kupitia kuvuruga afya zetu. Achunguzwe.
 
Kwahiyo suala hapa ni kuwa na madaktari wengi na siyo kuatazama utaratibu wa kuwapata kwa kufuata utaratibu wa kimataifa
Wanaiita njia mbadala...

Wakumbuke kiwa huu uzoefu waouzungumzia ni ule wa level husika tu(Kama ni CO, utabaki uzoefu huo tu na hautaweza kuwa MD hata kama uwe na uzoefu wa muda gani), kwa mantiki hiyo huwezi kuwa bingwa maana haujasoma zaidi ya level hiyo...

Madaktari bingwa wanasotea taalamu zaidi ya walizonazo za wali, na wanasoma kwa deep sana(wana specialize), ila leo hii anatokea mtu anasema jambo liwe hivi bila kuangalia undani wake, mwishowe athari ya maamuzi hayo yatakuwa hadi kwa kiasi kikubwa.

Siasa isiingizwe kwenye masuala nyeti ya kitaaluma/kitaalamu kama suala la Afya.
 
Fani yetu hii ishaingiliwa na wanasiasa

Am sad !
Waziri anatakiwa ajue Medicine haina shortcut na pia haifungamani na Siasa za afya japokuwa yeye ni Daktari Bingwa.

Wawape motisha madaktari wakasome na sio kugawa “Ubingwa” kwa kisingizio cha uzoefu.

Kusoma MMed kunahitaji umakini na kujitoa kwa hali ya juu na sio kutaka sifa mbele ya wapiga kura kama wafanyavyo wanasiasa.

Kwa muktadha huu basi CO nao watunukiwe MD baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu na kupimwa na hiyo mitihani.
 
Kweli mkuu, hapa walitakiwa watoe mitihani ya kumaintain certificate za practise na sio kuwafanya wawe mabingwa
 
KUWATAMBUA MADAKTARI BINGWA

Mhariri 12/07/2019: Maoni

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile ametangaza mpango wa kuwatambua madaktari wenye uzoefu wa muda mrefu kama mabingwa.

Amesema wamebuni mpango huo kuongeza idadi ya madaktari bingwa walio katika hospitali mbalimbali nchini, hususani za mikoa na wilaya.
Katika mpango huo, wizara imeamua kuandaa utaratibu wa madaktari wenye uwezo mkubwa na uzoefu wa muda mrefu, kufanya mitihani maalumu ya kuthibitisha viwango vyao vya ujuzi.

Alisema, mpango huo utafanana na upimaji ujuzi wa wataalamu wa fani ya uhasibu ambao hufanya mitihani ya shahada za umahiri (CPA).

Tumeguswa na hatua hii ya wizara kuongeza wigo wa madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali nchini kupitia mfumo mbadala.

Kwa muda mrefu, madaktari bingwa wamekuwa wakitokana na wanaoenda kusomea shahada za juu za uzamili (Msc) na uzamivu (PhD) katika umahiri wa fani ambayo wamekuwa wakitibia.

Kutokana na mfumo huo, imekuwa vigumu kupata wataalamu wengi waliobobea wa kuweza kuwa madaktari bingwa kwa kuwa ni wachache wanaopata ufadhili kusomea umahiri wa fani.

Ndio maana tunasema, hatua hii ya wizara kuja na mfumo mbadala wa kuwatambua madaktari wenye uwezo, ujuzi na uzoefu wa muda mrefu lakini hawajaweza kuongeza vyeti darasani ni nzuri na itachochea ufanisi wa madaktari wengi.

Tanzania imejaliwa madaktari wengi wenye uwezo mkubwa kutokana na kupata mafunzo mazuri kwenye vyuo vikuu vya tiba na afya vya Muhimbili (Muhas), Bugando, KCMC na taasisi nyingine za afya zinazotoa mafunzo ya uganga.

Ni katika muktadha huo, tunasema tunaunga mkono hatua hii ya wizara kuwatambua na pia kuwapandisha madaraja na kuboresha maslahi yao, madaktari itakaowatambua kimfumo huu.

Hii itakuwa motisha kubwa kwa madaktari wengi ambao hawajabahatika kuwa mabingwa lakini wamekuwa wakifanya kama za kibingwa.

Ni vyema basi madaktari wenye uwezo, ujuzi na uzoefu huo mkubwa lakini hawajatambuliwa wakajiandaa kufanya mitihani ya umahiri ili nao sasa watambuliwe rasmi pale watakapofaulu.

Hatua hii itasaidia kuongeza idadi ya madaktari wanaotambuliwa kama madaktari bingwa na pia motisha kwa ambao wamekuwa wakitumika bila kutambuliwa hivyo na kuboresha huduma.

Tunaungana na wananchi kuipongeza wizara na serikali kwa jumla kwa kubuni mfumo huu na kutumaini kwamba utapokewa vyema na wote.

Hongera wizara kutambua madaktari bingwa.
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

C&P
Naona siasa inagonga hodi kwa madaktari.
 
Kwahiyo suala hapa ni kuwa na madaktari wengi na siyo kuatazama utaratibu wa kuwapata kwa kufuata utaratibu wa kimataifa
Sidhani hata hapo Burundi wanaweza tambua huo udaktari bingwa, take simple logic ni kwamba ni rahisi kueleweka pale unapomchukua Captain wa jeshi na ukamzawadia u DC au akatunikiwa u RC, ubunge or uwaziri lakini huwezi kueleweka Kama utampatia u major general jeshini bila kupitia mafunzo stahiki yanayohalalisha cheo hicho, dunia mzima Ina taratibu za kuongoza taaluma na hazinaga siasa Kama tunavyotaka kufanya
 
Fani ya afya imevamiwa awamu hii. Walianza na kushusha vigezo vya kusomea uuguuzi, sasa wamekuja kwenye udaktari bingwa

Yote haya yanafanyika chini ya naibu waziri ambaye ni daktari bingwa. Ama kweli kikulacho kinguoni mwako

DR.FAUSTINE NI DAKTARI BINGWA WA NINI?
 
Wanaiita njia mbadala...

Wakumbuke kiwa huu uzoefu waouzungumzia ni ule wa level husika tu(Kama ni CO, utabaki uzoefu huo tu na hautaweza kuwa MD hata kama uwe na uzoefu wa muda gani), kwa mantiki hiyo huwezi kuwa bingwa maana haujasoma zaidi ya level hiyo...

Madaktari bingwa wanasotea taalamu zaidi ya walizonazo za wali, na wanasoma kwa deep sana(wana specialize), ila leo hii anatokea mtu anasema jambo liwe hivi bila kuangalia undani wake, mwishowe athari ya maamuzi hayo yatakuwa hadi kwa kiasi kikubwa.

Siasa isiingizwe kwenye masuala nyeti ya kitaaluma/kitaalamu kama suala la Afya.
Walifanya hivihivi kwenye Elimu... Walichagua wenye division IV hadi ya D 2 na kuwapeleka kusomea ualimu wa shule za msingi. Leo wanafunzi Wanamaliza drs la saba lakini wanasoma kwa tabu au hawajui kabisa kusoma,utashangaa wanawasomba wote na wanawaingiza secondary (form I) halafu wanatarajia shule za kata zitoe matokeo mazuri. Siasa za Tanzania ni kwikwi
 
Here we go again. Our lives are at stake here. You can't politicize such a critical profession as medicine. Ni bora tuendelee kuwa na madaktari bingwa wachache kuliko kuwa nao wengi ila wasio na ujuzi bingwa.
 
KUWATAMBUA MADAKTARI BINGWA

Mhariri 12/07/2019: Maoni

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile ametangaza mpango wa kuwatambua madaktari wenye uzoefu wa muda mrefu kama mabingwa.

Amesema wamebuni mpango huo kuongeza idadi ya madaktari bingwa walio katika hospitali mbalimbali nchini, hususani za mikoa na wilaya.
Katika mpango huo, wizara imeamua kuandaa utaratibu wa madaktari wenye uwezo mkubwa na uzoefu wa muda mrefu, kufanya mitihani maalumu ya kuthibitisha viwango vyao vya ujuzi.

Alisema, mpango huo utafanana na upimaji ujuzi wa wataalamu wa fani ya uhasibu ambao hufanya mitihani ya shahada za umahiri (CPA).

Tumeguswa na hatua hii ya wizara kuongeza wigo wa madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali nchini kupitia mfumo mbadala.

Kwa muda mrefu, madaktari bingwa wamekuwa wakitokana na wanaoenda kusomea shahada za juu za uzamili (Msc) na uzamivu (PhD) katika umahiri wa fani ambayo wamekuwa wakitibia.

Kutokana na mfumo huo, imekuwa vigumu kupata wataalamu wengi waliobobea wa kuweza kuwa madaktari bingwa kwa kuwa ni wachache wanaopata ufadhili kusomea umahiri wa fani.

Ndio maana tunasema, hatua hii ya wizara kuja na mfumo mbadala wa kuwatambua madaktari wenye uwezo, ujuzi na uzoefu wa muda mrefu lakini hawajaweza kuongeza vyeti darasani ni nzuri na itachochea ufanisi wa madaktari wengi.

Tanzania imejaliwa madaktari wengi wenye uwezo mkubwa kutokana na kupata mafunzo mazuri kwenye vyuo vikuu vya tiba na afya vya Muhimbili (Muhas), Bugando, KCMC na taasisi nyingine za afya zinazotoa mafunzo ya uganga.

Ni katika muktadha huo, tunasema tunaunga mkono hatua hii ya wizara kuwatambua na pia kuwapandisha madaraja na kuboresha maslahi yao, madaktari itakaowatambua kimfumo huu.

Hii itakuwa motisha kubwa kwa madaktari wengi ambao hawajabahatika kuwa mabingwa lakini wamekuwa wakifanya kama za kibingwa.

Ni vyema basi madaktari wenye uwezo, ujuzi na uzoefu huo mkubwa lakini hawajatambuliwa wakajiandaa kufanya mitihani ya umahiri ili nao sasa watambuliwe rasmi pale watakapofaulu.

Hatua hii itasaidia kuongeza idadi ya madaktari wanaotambuliwa kama madaktari bingwa na pia motisha kwa ambao wamekuwa wakitumika bila kutambuliwa hivyo na kuboresha huduma.

Tunaungana na wananchi kuipongeza wizara na serikali kwa jumla kwa kubuni mfumo huu na kutumaini kwamba utapokewa vyema na wote.

Hongera wizara kutambua madaktari bingwa.
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

C&P
kuna wale walioondolewa kwa tuhuma za vyeti feki , wako mabingwa wa5 ninaowajua , hawa nao watakuwemo kwenye kampeni hii ?
 
Dr Faustine alisoma Mmed ya Haematology and blood transfusion.

Dr Faustine achana na huo mpango wako fanyia kazi kwanza jambo hili; Kuna CO ambayo walisoma MD mpaka sasa hivi hawajafanyiwa recategorization yan mtu amesoma MD ila analipea 550,000/- na ni zaidi ya miaka mitano. Kuna mtu alisoma CO kutoka CA tangia mwaka 1992 mpaka leo anasomeka CA. Kuna daktari alimaliza Mmed miaka minne iliyopita mshahara ukawa wa Md for four years akaamua kusepa private. Kuna MD mmoja alisoma akitotokea CO huu ni mwaka wa sita analipwa mshahara wa CO. Kwa Dr Faustine anza na hili achana na huo upuuzi
 
Kinacho fuatia baada ya zoezi hilo ni kuua taaluma ya tiba na hospitali zetu kukosa thamani. He chama cha madaktari wamehusishwa? Wanasiasa kuweni na aibu kwa taaluma. Nayo wizara ya ujenzi wapandisheni mafundi mchundo kuwa wahandisi.
 
Wanafananusha CPA Kweli Dah ??
Waziri anatakiwa ajue Medicine haina shortcut na pia haifungamani na Siasa za afya japokuwa yeye ni Daktari Bingwa.

Wawape motisha madaktari wakasome na sio kugawa “Ubingwa” kwa kisingizio cha uzoefu.

Kusoma MMed kunahitaji umakini na kujitoa kwa hali ya juu na sio kutaka sifa mbele ya wapiga kura kama wafanyavyo wanasiasa.

Kwa muktadha huu basi CO nao watunukiwe MD baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu na kupimwa na hiyo mitihani.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom