Serikali Yaipongeza TotalEnergies Marketing Tanzania Limited Kwa Uwekezaji Mkubwa, Kujenga Uwezo wa Technology Transfer, na Kutoa Ajira Kwa Watanzania

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
40,442
2,000
TotalEnergies News Feature- Nipashe.jpg


Serikali imeipongeza Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies, kwa kuunga mkono juhudi za Tanzania kujenga Tanzania ya viwanda kwa kujenga viwanda, kutoa ajira, na kuleta teknolojia kwa Watanzania, ambapo kabla ya ujenzi wa kiwanda cha vilainishi, Tanzania ilikuwa ina aagiza lubricants kwasababu tulikuwa hatuna kiwanda cha kutosheleza soko, lakini sasa kupitia TotalEnegies, Tanzania inajitosheleza kwa lubs na ziada tutauza nje, hivyo ku sevu fedha nyingi za kigeni, inayotumika ku import, and earn more forex kwa export.

Pongezi hizo, zimetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaudi Kiguhe, aliyekuwa mgeni rasmi, kwenye uzinduzi wa vilainishi vipya vya magari na mitambo vya kampuni ya TotalEnergies, uliofanyika jana jijini Dars es Salaam.

Naibu Waziri amesema, vilainishi hivi vinatumia teknolojia ya kisasa kuvitengeneza,lakini sasa ni Watanzania wamejengewa uwezo sio tuu kwa kupatiwa fursa za ajira bali pia kupatiwa uwezo wa tech transfer kutoka kwao, kuileta Tanzania.

Pia ameipongeza TotalEnergiy kwa Tanzania mpaka sasa, ni TotalEnergy ndio the biggest investor, mradi wake wa EACOP ndio the biggest FDI in Tanzania ever, kuliko mradi mwingine wowote, labda hiyo bandari ya Bandari ya Bagamoyo ije au LNG plant, hivyo kiwanda la lub kimeongeza investments za Total Tanzania.

Kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited ambayo awali ilijulikana kama Total Tanzania Limited mezindua vilainishi hivyo kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ya TotalEnergies kwa mwaka 2021, yenye kaulimbiu: Tujienge kesho pamoja.

Hii ni awamu ya tatu ya wiki ya huduma kwa mteja ya TotalEnergies tangu ianzishwe mwaka 2019. TotalEnergies inaendelea kuonyesha dhamira yake kwa Tanzania kwa kuwakaribisha wateja wao ili kushiriki maono yao ya mustakabali wa kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited nchini.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni, Jean-Francois Schoepp alisema kuwa, "Kama baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa "Ikiwa maendeleo ya kweli yatatokea, ni lazima wananchi washirikishwe." Pia tunaamini kwamba TotalEnergies Marketing Tanzania Limited itaendelea kukuwa zaidi endapo tutawashirikisha wateja wetu wateja wetu na kuwa tayari kukidhi mahitaji kikamilifu.”

Wafanyakazi wa TotalEnergies Marketing Tanzania Limited wakiongozwa na mkurugenzi mkuu, Bw. Jean-Francois Schoepp walitoa huduma kwa wateja waliotembelea kituo cha TotalEnergies East Oysterbay siku ya Jumatatu na kupata fursa ya kusikiliza maoni ya wateja, kuboresha mahusiano na wateja wao kwa nia ya kuziba mapengo yoyote yaliwepo na kuweza kujenga TotalEnergies Marketing Tanzania Limited kwa pamoja na wateja wao. Zaidi ya hayo, wateja walipata nafasi ya kucheza gurudumu la bahati katika kituo hicho na walijishindia zawadi kadhaa zikiwemo fulana, chupa za maji, kofia, bidhaa za kutunza magari kama vile baridi na air freshener, na vocha ya zawadi zilizowawezesha kununua bidhaa zozote katika duka la Cafe Bonjour lilipo kituoni hapo.

Kampuni ya mafuta ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited ambayo awali ilijulikana kama Total Tanzania Limited imehitimisha wiki ya huduma kwa wateja ya TotalEnergies kwa mwaka 2021, kuwaahidi Watanzania kampuni hiyo itashirikiana kikamilifu na Watanzania, kuijenga Tanzania bora zaidi na kuahidi kufanya makubwa Tanzania.

Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Jean-Francois Schoepp aliyasema hayo katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa wateja, iliyohitimishwa katika Ofisi za TotalEnergies, Masaki jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Huku akinukuu kauli ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Jean-Francois Schoepp amesema Nyerere alisema "Maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu, na sio maendeleo ya vitu, ili kupata maendeleo ya kweli ni lazima wananchi washirikishwe."

Hivyo ameahidi kwamba TotalEnergies Marketing Tanzania Limited itafanya makubwa Tanzania, kwa kuwashirikisha Watanzania, wakiwemo wateja wa TotalEnergies, katika mipango mkakati wa kampuni, na kuwataka wafanyakazi kuendelea kujituma kwa bidii hata ikibidi kufanya kazi ya ziada ili kukidhi mahitaji ya jamii kikamilifu.

Katika wiki hii, wafanyakazi wa TotalEnergies Marketing Tanzania Limited wakiongozwa na mkurugenzi mkuu, Bw. Jean-Francois Schoepp walitoa huduma kwa wateja waliotembelea vituo mbalimbali vya TotalEnergies zaidi ya 100, vilivyotapakaa nchini kote Tanzania na kupata fursa ya kusikiliza maoni ya wateja, kuboresha mahusiano na wateja wao kwa nia ya kuziba mapengo yoyote yaliwepo na kuweza kujenga TotalEnergies Marketing Tanzania Limited kwa pamoja na wateja wao.

Zaidi ya hayo, wateja walipata nafasi kutoa maoni yao kuhusu huduma za Total Energies na kucheza gurudumu la bahati katika vituo hivyo na walijishindia zawadi kadhaa zikiwemo fulana, chupa za maji, kofia, bidhaa za kutunza magari kama vile baridi na air freshener, na vocha ya zawadi zilizowawezesha kununua bidhaa zozote katika maduka la Cafe Bonjour yaliyopo kwenye kila kituo.

Akiyataja miongoni mwa makubwa ambayo TotalEnergies inapanga kuyafanya Tanzania, Mkurugenzi Jean-Francois Schoepp, amesema kufuatia changamoto za upatikanaji umeme wa uhakika, TotalEnergies imejipanga kusaidia Tanzania kufua umeme, na imejipanga kufikia mwaka 2050, itakuwa inatumia nishati jadilifu (renewable energy) ambazo ni rafiki wa mazingira zikiwemo umemejua, umeme upepo na umeme jotoardhi.

Mpaka kwa nchini Tanzania, kampuni ya TotalEnergies ndio inayoongoza kwa mtandao mkubwa wa vituo vya usambazaji mafuta ambapo inavyo vituo zaidi ya 100 nchini Tanzania, ambapo baadhi ya vituo vinamilikuwa na kampuni na kuendeshwa na kampuni kwa mtindo wa COCO, (Company Owned, Company Operated) vingine vinamilikiwa na kampuni lakini vinaendeshwa na Watanzania kwa mtindo wa CODO, (Company Owned, Dealer Operated) lakini vituo vingine ni TotalEnergies, imewajengea uwezo Watanzania, hivyo vinamilikiwa na kuendeshwa na Watanzania kwa mtindo wa DODO, (Dealer Owned, Dealer Operated).

TotalEnergies ndio kampuni inayoongoza kwa uwekezaji wenye thamani kubwa Tanzania, kuliko uwekezaji mwingine wowote wowote Tangu Tanzania imepata uhuru, Mradi wake wa Bomba la mafuta ghafi, kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga, nchini Tanzania, ndio mradi mkubwa wa uwekezaji nchi Tanzania kuliko mradi mwingine wowote.

Na hiki kiwanda cha vilanishi cha TotalEnergies, Lubricant and Oil Blending Plant (LOBP) ndicho kiwanda kikubwa kuliko vyote cha vilainisha kwa nchi za Afrika Mashariki, kati na Kusini, kikitumia tekinojia ya kisasa na kutoa sio tuu ajira kwa Watanzania, bali Watanzania wamejengewa uwezo wa kitaalamu na ndio wanaoendesha kiwanda.

Paskali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom