Serikali 'yaipiga stop' TANESCO kupandisha bei ya umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali 'yaipiga stop' TANESCO kupandisha bei ya umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtwana, Oct 31, 2012.

 1. mtwana

  mtwana JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 399
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Wizara ya Nishati na Madini imelizuia Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kupandisha bei ya umeme kama lilivyokuwa limepanga kufanya hivyo Januari, mwakani.

  Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Sospeter Muhongo, alisema hayo juzi wakati akihojiwa kwenye kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya ITV.

  “Kumekuwa na madai kwamba, Tanesco watapandisha bei ya umeme ifikapo Januari 2013. Lakini nimewaelekeza Tanesco na Ewura (Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji) wasipandishe bei ya umeme,” alisema Profesa Muhongo.

  Alisema ameielekeza Tanesco isipandishe bei kwa sababu katika deni la dola za Marekeni milioni 250 inazodaiwa, serikali imekuwa ikilisaidia kulipa.

  Profesa Muhongo alisema hadi sasa serikali imekwishatoa dola za marekani milioni 50 kupunguza deni hilo, ambalo limebaki dola za Marekani milioni 200.

  Alisema serikali imepunguza bei ya kuunganisha umeme wananchi ili ifikapo mwaka 2015 asilimia 30 ya Watanzania wawe wanapata nishati hiyo tofauti na sasa, ambapo wanaopata ni asilimia 18.4 tu.

  Profesa Muhongo alisema wizara yake imejipanga kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme kifikie megawati 2,780 kutoka megawati 1,438 zinazozalishwa hivi sasa ifikapo mwaka 2015.

  Alisema uzalishaji huo utaongezeka kutokana na mkakati uliopo wa kuongeza vyanzo vya uzalishaji umeme na kwamba, hivi sasa matumizi ya umeme kwa nchi nzima ni megawati 830.

  “Mgawo wa umeme haupo na wala hautakuwapo, wengine wanaufurahia uwapo kwa sababu zao binafsi za kibiashara na kisiasa. Lakini nawahakikishia wananchi hakutakuwa na mgawo wa umeme,” alisema Profesa Muhongo.

  Akizungumzia suala la gesi, alisema wizara yake imewasilisha sera ya gesi katika Baraza la Mawaziri na rasimu ya sera hiyo imepelekwa kwa wakuu wa mikoa ili wananchi waweze kutoa maoni yao kabla ya kupelekwa bungeni Februari, mwakani.

  Profesa Muhongo alisema rasimu ya sera hiyo imepelekwa katika mikoa, ambayo gesi na mafuta inapatikana na, ambayo inatumia gesi hiyo kwa wingi ni Lindi, Mtwara, Tanga, Pwani, Rukwa (Sumbawanga), Katavi, Mbeya na Arus
  ha.
   
 2. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Haya mambo ni commitment, kwa kweli sasa naamini mgawo ulikuwa unapikwa. Yaani nchi nzima matumizi 830, sasa miezi mitano iliyopita tulikuwa hatuna uwezo wa kuzalisha megawatts 1000: hongera sana Prof Mungu akujalie maisha marefu ili swala la umeme lisiwe tatizo tena. Be blessed again we pray for you.
   
 3. Ufunguo

  Ufunguo JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hongera prof, endeleza kasi uwakomboe watanzania. cheers
   
 4. S

  Shembago JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera Prof
   
 5. P

  Panda Kapesi JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 284
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  Na mimi nampongeza sana prof. Wasiwasi wangu ni kwamba je atadumu kwa kasi hii ya kupambana na mafisadi? Hawatamshughulikia na kumtoa kafara huyu? i'm so worried jamani maana historia ya nchi yetu hii hasa kwa awamu hii haitoi matumaini kwa watu wenye uzalendo. Inabidi mtu aandike wosia kabisa kabla ya kuchukua misimamo kama ya prof! Maana time yoyote wanaweka kukukolimba!
   
 6. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  big up kwako prof!
   
 7. f

  findu fiki JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tunamuombea kwa Mungu azidi kumbariki na kumlinda watu wote wenye nia mbaya washindwe.
   
Loading...