Serikali yaipa China kufanya utafiti kujua kiasi cha madini yaliyopo Tanzania

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
#NipasheHabari Wizara ya Madini, inashirikiana na Wizara ya Maliasili ya nchini China, kufanya utafiti wa kufahamu kiasi cha madini yanayopatikana nchini.

Najiuliza ivi mchina kweli huo utafiti hadi kwisha na madini yatakuwa yameisha

====

Wizara ya Maliasili ya China kutafiti kiasi cha madini nchini

Naibu Waziri wa Madini, Staslaus Nyongo, aliyaeleza hayo jana jijini Dar es Salaam muda mfupi baada kumpokea Naibu Waziri wa Maliasili wa China, Zhong Ziran na wataalam wa Jiolojia waliowasili nchini kwa lengo la kutoa mafunzo na kufanya utafiti wa madini.

Amesema Tanzania na China zimeendelea kushirikiana katika maeneo mbalimbali hivyo wataalam hao wamekuja nchini kwa siku tano ili kukutana na wajiolojia wa madini kwa ajili ya kutoa mafunzo na kufanya utafiti wa kufahamu kiasi cha madini yaliyopo nchini.

“Leo tumepokea ugeni kutoka China unaoongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili ambaye anahusika pia na madini lengo kubwa ni kubadilishana uzoefu, kujifunza kutoka kwao, kufahamu mbinu za kisasa wanazotumia lakini pia tumewaomba watusaidie kushirikiana na wataalam wetu kufanya utafiti ili kufahamu kiasi cha madini yaliyopo nchini,”Nyongo amesema.

Ameeleza kuwa, baada ya kufanyika utafiti wa kina kwa kutumia teknolojia za kisasa, watatafuta wawekezaji ikiwamo nchi ya China ambayo imesema ipo tayari kuwekeza katika sekta hiyo.

Amesema pia ugeni huo upo nchini kwa ajili ya kufanya mikutano kwa ajili ya uwekezaji wa sekta ya madini ambayo awali ilifanyika chini China.

“Ujumbe huu kwetu ni fursa kwa sababu tutaweka mpango wa pamoja kwa ajili ya kushirikiana katika kuboresha sekta ya madini ikizingatiwa kuwa wao wamesema wapo tayari kuwekeza,” Nyongo amesema.

Naye Naibu Waziri wa Maliasili wa China, Zhong Ziran, ameishukuru kwa ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na China na kusema wameshawishika kuja nchini kutokana na sera na sheria nzuri zilizowekwa na serikali hasa katika sekta ya madini.

“Huu ni muendelezo wa ushirikiano uliopo katika nchi hizi mbili, tunapenda na kushawishika kuendelea kuja Tanzania kwa sababu ya amani na vivutio vilivyopo, tunaamini ujio wetu utakuwa wa manifuaa kwetu sote,” Zinar amesema.

Chanzo: Nipashe
 
#NipasheHabari Wizara ya Madini, inashirikiana na Wizara ya Maliasili ya nchini China, kufanya utafiti wa kufahamu kiasi cha madini yanayopatikana nchini./ https://bit.ly/2VvB9sN

Najiuliza ivi mchina kweli huo utafiti hadi kwisha na madini yatakuwa yameisha
Labda Mchina, maana Wazungu wanazo data siku nyingi sana.
 
Hivi huyo aliwapa hiyo order serious au usanii kwa mgongo wa kupika data na upigaji ngoja niende Google nikafuatilie hawa USA maana ndio wana data kamili tangu 80
 
Back
Top Bottom