Serikali yaingiwa na hofu jinsi mbunge anavyopata taarifa nyeti

Hatuna waziri mkuu...!!!!!!

Badala ya waziri mkuu wetu kusimamia haki,kukemea maovu, kufichua maozo na kuisafisha serikali yake, yeye ameamua kutoa viapo vya kujitundika ili kuficha maozo.! Huyu mkuu ni mwoga na siyo mpiganaji!!ameona ni heri wananchi wake wafe kwa kukosa huduma muhimu na kudhulumiwa haki na mali zao!!kuliko kupambana na mafisadi .
Kwa kifupi hawa siyo viongozi tuowahitaji wakati huu mgumu tunapopambana na dhuluma kutoka ndani na nje ya nchi.

Sasa kama hawa ndiyo viongozi wetu wa kiafrika ambao wananyuti na kusalimu amri mbele ya mafisadi je wataweza kusimama kidete na kutuongoza kwenye mapambano yetu na ukoloni mambo leo????

Hongera Dr.Slaa kwa ushujaa na uzalendo!!!

Tuko pamoja nawe.

-Wembe.
 
Serikali lazima iwe na siri. Kazi ya Bunge ni kusimamia Serikali. Huwezi kusimamia chombo ambacho kinakuficha siri. Rules za Bunge zina provisions za kufunga milango ya Bunge ku handle situation kama hiyo. Na kama hiyo haitoshi, kama wanaona kama kuna Wabunge hawafai kupewa siri, bado kuna committee ambayo ilibidi iende chemba ikathibitishe madai ya Pinda. Siri ni kwangu na wewe, siri sio kwa Bunge.

THE STANDING ORDERS, 2001
MADE PURSUANT TO THE PROVISIONS OF ART. 89 (l) OF THE CONSTITUTION.


Motion for the withdrawal of stranger, 45 (3) d

The following Motion may be submitted without notice; that is: Motion for the withdrawal of strangers from the Assembly;

Authority to withdraw strangers from the Assembly 115 (1)

At any time when he thinks fit to do so, the Speaker may order the withdrawal of strangers from any part of the Assembly debating Chamber and its precincts, and may order the doors of the Assembly debating Chamber to be closed.

The Defence and Security Committee, 98 (1) b and c

The Defence and Security Committee ... its responsibilities shall be as follows:-

(b) To consider matters pertaining to defence and security of citizens and National Security.

(c) To consider any other matter which shall be referred to it by the Speaker.
 
Kama UFISADI unapaswa kuwa SIRI basi hiyo maana ya neno lenyewe inabidi ibadilishwe au SERIKALI yenyewe (au CHAMA TAWALA wanavyopenda kujiita) wanaratibu, wanashiriki, wanabariki kwa namna moja UFISADI huu unaoendelea kuitafuna NCHI YETU.
WATUMISHI wetu wa UMMA wanastahili PONGEZI za aina yake kuyafichua haya ingawa kwa kiasi fulani wanachelewa mno kufanya hivyo. Tunawaomba waendelee kwa kasi zaidi.
 
Hongera sana Dr Slaa,

hili suala nilishawahi kulisema hapa JF............kwa nini watu wafanye ufisadi na documents associated ziwe classified as Secret?...........huu ni upumbavu.

Secrets should be kwa manufaa ya umma na si vinginevyo...........statements za Mizengo Pinda zinakatisha tamaa beyond belief...............it appears mafisadi fought for this PM position............now they have it!!!........guys lets forget abt mafisadi......atleast for now.........honestly ni vita ngumu sana.............kwa sababu mafisadi now have got all means necessary for their cover.....

taaaaaaaaratibu nimeanza kufikiria na kuamini kuwa hata kama Lowassa ni fisadi lkn wamemtoa kafara kwa ajili ya kumuweka mtu wao wakuwafanyia 'kazi' yao........ yani JK anazidi kujianika
 
Mi naona ili kukabiliana nao hawa mafisadi...tuanze kuwatenga,kuwanyanyapaa kwa vitendo na sio maneno tena na wajione kuwa watanzania hawawapendi,, tuanzie makanisani ..misikitini..mitaani, kwenye Bar,mahotelini kila sehemue tutumie njia zozote hata kuwazomea,kuwasema wazi wazi,kuwanyoshea vidole huku tukionyesha vicheko vya kejeli..

nafikiri tukifanya hili itawachoma vibaya na raha haitakuwepo tena mioyoni mwao na kama hawatahama nchi basi watanyooka na kutubu kwa watanzania wote,na hii itakuwa fundisho kwa wengine vifisadi vinavyochipukia....tulifanye hili jambo liwe completely unethical kama kubaka mtoto na kama ukifanya ivyo uwe tayari kukosa raha katika nchi yako.............

tuwatenge hawa watu..makelele yetu hawayagusi hata nukta,,,makelele ya wabunge hayawakoseshi usingizi hata kidogo..na sasa ivi mpaka PM nae anawatetea ndio kabisaaa....ndugu zangu silaha iko mikononi mwetu sasa .tusiongee tena watazoe maneno yetu....lets do it now '' ACTION'' yani labda wasiwe wanatoka nje ya nyumba zao wawe wanakaa ndani tu..hapo ndio watapona........tuwafanye wawe wafungwa katika nchi yao...adabu watashika hawa
 
Back
Top Bottom