BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,082
Wananchi hawana imani na serikali ndiyo maana wanatoa nyeti ili labda wasaidie kuleta mabadiliko kwa manufaa ya Watanzania wote. Nyeti za serikali zitaendelea kutoka tu mpaka pale Watanzania wawe na imani na serikali iliyipo madarakani ipo pale kwa manufaa ya Watanzania wote na siyo kundi la mafisadi wachache
Date::6/29/2008
Serikali yaingiwa na hofu jinsi mbunge anavyopata taarifa nyeti
Na Kizitto Noya, Dodoma
Mwananchi
SERIKALI inaumiza kichwa kujua mtandao unaotumiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Willibrod Slaa, kupata taarifa zake za siri na kuzianika hadharani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), Philip Marmo amekiri bungeni juzi jioni kuwa, Dk Slaa ana mtandao mkubwa usiofahamika anaoutumia kupata nyaraka za siri za serikali kinyume na taratibu.
Kauli ya Marmo ilifuatia swali la Dk Slaa kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati Kamati ya Bunge ilipokuwa inapitia vifungu kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kuwa ni aina gani ya nyaraka za serikali zinapaswa kuwa siri.
Dk Slaa alitaka kujua endapo nyaraka za serikali ambazo zimejaa kumbukumbu za kifisadi na ambazo wabunge wakiziomba kwa utaratibu wa kawaida wananyimwa, zinapaswa kuwa siri.
Akiwa na nyaraka kadhaa mkononi alizosema kuwa ni sehemu ya zile za serikali zinazopaswa kuwa siri, lakini watu aliowaita wasamaria wema wamempa, Dk Slaa alisema haelewi mantiki ya nyaraka hizo kuwa siri wakati hazina faida kwa taifa.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, mimi naomba kuuliza ni nyaraka gani hasa za serikali zinapaswa kuwa siri. Hata zile ambazo zimejaa uongo? Mimi ninazo hapa na kama
Mheshimiwa Marmo anataka kuwatuma polisi waje wanikamate niko tayari, lakini nyaraka hizi zina maana gani kwa taifa? alihoji Dk Slaa akionyesha nyaraka hizo.
Kwa mujibu wa Dk Slaa wapinzani wanajua umuhimu wa usiri wa nyaraka za serikali, lakini inapofikia mahala mfumo wa serikali unaanza kuporomoka, hawana sababu ya kuogopa kutafuta nyaraka hizo kwa njia ya mkato na kuzitumia kuweka mambo hadharani.
Lakini kama mfumo wa serikali unaanza kuanguka na serikali ikaonyesha nia ya dhati kudhibiti tatizo hilo, sisi ni wazalendo pia hatutazitafuta wala kutoa tena siri za serikali hadharani, alisisitiza.
Akijibu suali hilo kwa upole, Marmo alisema, inaonekana Dk Slaa ana mtandao mkubwa katika kupata taarifa hizo za siri na amekuwa mjanja katika kuzizungumzia kuwa anafahamu kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai.
Dk Slaa ni mjanja sana anajua anachofanya kuwa ni kosa la jinai. Pana jinai hapa na ndio maana hata katika hii nyaraka ya EPA amesema, nimeondoa jina la source (chanzo cha Habari) kwa usalama wake, alisema Marmo akinukuu nyaraka ya siri ya serikali aliyodai kuwa imepatikana kutoka kwa Dk Slaa.
Marmo alisema nyaraka za serikali lazima ziwe za siri na kuwa nazo mtu asiyehusika ni kosa la jinai ingawa kama kuna umuhimu wa mtu kuzipata anaweza kufanya hivyo katika utaratibu unaokubalika.
Aliwataka wabunge wanaotaka kujua mambo ya serikali kupitia nyaraka zake za siri kufuata utaratibu badala ya kutumia njia ya mkato kisha kuanika siri za serikali
hadharani. Mimi naomba tufuate utaratibu, kinyume chake huko ni kuidhalilisha serikali, alisema Marmo.
Kwa muda mrefu sasa Dk Willibrod Slaa na chama chake cha CHADEMA amekuwa akiibua tuhuma mbalimbali za ufisadi ndani ya serikali kwa kutumia nyaraka za siri za serikali.
Baadhi ya tuhuma hizo ni upotevu wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA), rushwa katika upatikanaji wa zabuni ya
kuzalisha umeme wa dharura na Kampuni ya Richmond na mikataba mibovu katika migodi ya madini.
Juzi, Dk Slaa alipingana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika majibu yake kwamba hawezi kuzungumzia suala la Meremeta kwa sababu za ulinzi na usalama.
Dk Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo walimweleza Pinda kuwa Meremeta wanayomtaka azungumzie ni ile ya pili baada ya jeshi kumaliza kazi na kampuni waliyodai kuwa ni 'Meremeta ya kwanza'.
Cheyo alisema alitaka suala la Meremeta kufanyiwa uchunguzi wa kina na kwamba kulihusisha na suala hilo na jeshi sio sawa na kwamba Waziri Mkuu anapaswa kuwatendea haki Watanzania kwa kuzungumzia suala hilo.
Kama kweli kuna Sh12 bilioni Tangold, tunazihitaji kwa ajili ya miradi ya maji, alisema Cheyo.
Hata hivyo, Pinda alishikilia msimamo wake na kugoma kuzungumzia kampuni hiyo yenye makampuni tanzu ya Tangold, Deep Green na Green Finance kwa maelezo kuwa yanahusiana na Jeshi na kwamba yuko tayari kusulubiwa kwa hilo.