Hansard
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 842
- 247
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu Wanahabari, Kama mnavyofahamu hadi leo Tarehe 09 Januari,2016 zoezi la kuchagua Mameya katika Jiji la Dar es Salaam, Manispaa ya Ilala na Manispaa ya Kinondoni bado halijakamilika.
Sababu zinazotolewa ni mbili:
(i) Kutokana na Mvutano wa vyama vya siasa juu ya Uhalali wa Wajumbe wanaotakiwa kushiriki katika zoezi la kupiga kura
(ii) Kutokea Mapingamizi ya Kisheria Mahakamani, lakini sababu kubwa ikiwa ni kupata ufafanuzi wa sababu ya awali.
Ndugu Wanahabari, Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka, 1977 na Katiba ya Zanzibar ya mwaka, 2010, Muundo wa Serikali za Mitaa Zanzibar na Muundo wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara si jambo la Muungano.
Aidha, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287, Kifungu cha 35(1)(e) kimebainisha Wabunge wa Viti Maalum kuwa Wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri za Wilaya. Hata hivyo kifungu hicho kinaweka bayana kama ifuatavyo:
35(1)(e) “Any Member of Parliament whose nomination originated from organs of Political Parties within the area of jurisdiction of the District Council”
Kifungu hiki kinatoa ruhusa kwa Wabunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuingia na kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Madiwani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa katika ngazi ya Wilaya.
Kwa upande wa Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizopo chini ya Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288, Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Serikali za Mitaa (Local Government Laws (Miscelleneous Amendments),Namba 13 ya Mwaka 2000 Kifungu cha 19(2)(d) kinaelezea suala la Wabunge wa Viti Maalum na ushiriki wao kwenye Mabaraza ya Madiwani ya Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji.
Kifungu hicho kinatamka ifuatavyo:
(d) “Any other Member of Parliament whose nomination originated from organs of Political Parties within the area of jurisdiction of the Council”
Kwa kuzingatia vifungu hivi vya Sheria za Serikali za Mitaa yaani Sura 287 na Sura 288, Wabunge wa Viti Maalum wanakuwa Wajumbe wa Baraza la Madiwani kwa misingi ya mapendekezo ya Chama cha Kisiasa husika; lakini, lazima mchakato wa kupatika kwao uwe ulianzia kwenye Mamlaka hiyo ya Serikali za Mitaa kwa mfano Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji husika.
Ndugu Wanahabari, Kutokana na maelezo niliyotoa, kwa namna yoyote ile haiwezekani kwa Mbunge au Mbunge wa Viti Maalumu kupiga kura nje ya Halmashauri ya Wilaya aliyokuwepo wakati anapendekewa na Chama chake cha siasa wakati wa zoezi la kuchukua fomu za kutaka kupendekezwa na chama chake ili kupata nafasi ya uongozi. Napenda kuviasa vyama vya siasa kuheshimu sheria zilizopo ili kujenga, kukuza na kudumisha demokrasia lakini pia kuondoa na kuepusha migogoro na mivutano isiyo ya lazima baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Ndugu Wanahabari, nakuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kabla tarehe 16/01/2016 Chaguzi zote katika Manispaa za Ilala, Manispaa ya Kinondoni ziwe zimefanyika.
Imetolewa na:
George B. Simbachawene (Mb)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
09/01/2016